Mtu Pekee aliyekataa teuzi wakati wa Magufuli ni ndugu Maswanya

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,093
2,000
mara nyingi teuzi zake mkuu alizifanya kuwa asante kwa kumsaidia jambo fulani na hiyo tabia ni common sana kwa wasukusy na kiuhalisia wake ni rushwa poa kama alivyosema kwenye ile pesa ya kung'arisha viatu, inshort ukimfanyia jambo zuri kwake msukuma lazima akupe zawadi/rushwa na niseme kidogo kwa upande wa akina mama ni copy & paste
Siyo busara sana kuuhusisha usukuma na huyo marehemu wenu.

Kama una hoja ya msingi against him sema against him siyo wasukuma.
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,093
2,000
Mimi naona kama wanaotegemea mabadiliko makubwa kutoka kwa huyu rais mpya wanaweza kupata mabadiliko cosmetic ya presentation lakini wakabaki kupewa u Magufuli uleule.

Samia Suluhu Hassan akiwa VP alishawaambia watu kwamba waichague au wasiichague CCM, itashinda tu.
Watu walikuwa wamefikia kiwango cha mwisho cha kumchukia Jiwe.

Hivyo hata wangepata rais mwingine mjinga mjinga kama Makonda au Nape wangeshangilia tu kwa kuhisi kuwa huenda akawa tofauti na jiwe.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,606
2,000
Katika Historia, ndugu Ally Masoud Maswanya ndio Mtu pekee alikataa Uteuzi wa Rais Magufuli.

Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya lakini siku ya kwenda kuapa hakutokea. Walipompigia simu akaape, akasema yupo Ofisini anadeal na wateja wake.

Alikuwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo kanda ya Ziwa. Sijui sasa hivi yupo wapi na anafanya nini.

Pia Soma: Mkuu wa Wilaya Mteule wa Mbozi, Ally Masoud Maswanya ajiuzulu
Walimuandama sana baada ya hapo...!!
 
Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,190
2,000
Katika Historia, ndugu Ally Masoud Maswanya ndio Mtu pekee alikataa Uteuzi wa Rais Magufuli.

Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya lakini siku ya kwenda kuapa hakutokea. Walipompigia simu akaape, akasema yupo Ofisini anadeal na wateja wake.

Alikuwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo kanda ya Ziwa. Sijui sasa hivi yupo wapi na anafanya nini.

Pia Soma: Mkuu wa Wilaya Mteule wa Mbozi, Ally Masoud Maswanya ajiuzulu
Waliagiza Afukuzwe kazi ..nadhani atakuwa yuko anafanya mambo yake mengine ...aliona Mbali
 
The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,770
2,000
Hakuna mahali nmesema ni lazima kila mtu afanye kazi serikalini.

Km ambavyo ni vigumu wote tukawa sekta binafsi.

Unaweza kuwa serikalini au sekta binafsi inategemea na malengo yako,au mazingira,hali ya elimu inaweza kusababisha uwe kati sehemu hizo mbili.

Siyo sahihi kusema UDC siyo potential.Siyo potential kwako kwa mwingine ni fursa adhimu .

1. Kwa wengine na pengine kwako, Yes, ni fursa adhimu, lakini kwa Maswanya na wengine haikuwa fursa adhimu bali ilikuwa ni kuji - downgrade...

2. Lakini factor kubwa ambayo pengine iliwafanya wengine kukataa teuzi za Mwendazake Magufuli, ni ugumu wa kufanya kazi chini yake..

Kwanza huyu jamaa anaanza na wewe anapokuteua tu kwa kukusimanga na kukuona bila yeye, huwezi kuishi au kupata fedha za kukuwezesha kupata mahitaji yako ya kila siku...

Ukitaka kuelewa na kuthibitisha hili, tafuta fursa au "inner circle sources" upate kujua Rais Samia Suluhu Hassani (akiwa VP) alivyokuwa anapata wakati mgumu kufanya kazi na Mwendazake..

This Mama made resignation attempts In two different occasions...

This is a vivid evidence that, it was quite difficult to work under the late President John P. Magufuli...

Kwa hiyo, si ajabu sana kuanza kujua sasa kuwa, kumbe baadhi ya watu walikuwa wanakataa teuzi zake...!!
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,647
2,000
Huyu na watu wa namna hiyo lazima alikuwa na baggage fulani ambayo hakutaka ijulikane. Tatizo lake ni kwamba aliupenda uDC ndipo akateuliwa, ila baada ya kuteuliwa akagundua kuwa ana mifupa kwenye kabati lake ambayo hataki ijulikane, na wakati huo akawa hawezi kuondoa jina lake kwenye uteuzi tena, ndipo akaamua kutohudhuria uapishwaji. Mtu kabla ya kuteuliwa, huwa unapewa taarifa kuwa mkuu anataka kukuteua kwenye nafasi fulani, je unaiweza. Mteuliwa mtumianiwa lazima akiri kuwa kweli anaweza kuimudu nafasi ie kabla uamuzi wa mwisho haujafanyika.

Sasa kama yeye alisema anaiweza nafasi ile, halafu siku ya mwisho ndipo miguu ikaganda, basi alikuwa na matatizo ambayo hatutayajua!!
Kama kabla hujayeuliwa huwa una kulishwa, juzi Dr.Mpango alikuwa anajifanya kushangaa nini?
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,981
2,000
Ukiajiriwa, unatajiwa kazi zako. Halafu pana kipengele cha: na kazi zingine utakazopangiwa na mwajiri wako...

I guess uteuzi unaangukia kwenye kazi nyingine utakazopangiwa na mwajiri wako.... Doesn't it?
Sijaelewa unachokizungumzia kinahusianaje na nilichokiandika hapo.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,981
2,000
Watu walikuwa wamefikia kiwango cha mwisho cha kumchukia Jiwe.

Hivyo hata wangepata rais mwingine mjinga mjinga kama Makonda au Nape wangeshangilia tu kwa kuhisi kuwa huenda akawa tofauti na jiwe.
Kama ilivyo sasa...baadhi ya watu wanafurahi kweli as if atakuwa tofauti sana na waliomtangulia.

I’ve been around the block for a minute.

Nakumbuka jinsi Kikwete alivyoingia madarakani na matumaini ambayo watu walikuwa nayo.

Ari mpya. Nguvu mpya. Kasi mpya. 2005 hiyo.

2010 ikaja maisha bora kwa kila Mtanzania.

By 2015 anapomaliza muda wake, mimi sikuona chochote kikubwa alichokifanya zaidi ya kutuhumiwa mambo ya ufisadi tu.

Sitegemei kikubwa na kilicho tofauti kwa Samia.
 
Mara nyingi anapoingia rais mwingine watu wanakuwa na matumaini mapya hivyo suala la watu kufurahia ni lazima wafurahie.

Suala la mabadiliko inategemea sasa na rais mwenyewe atafanya nini kuleta hayo mabadiliko ya watu.

Mathalani miaka 10 ya mzee Kikwete ilikuwa na changamoto nyingi sana za serikali kushindwa kutoa huduma sawa sawa kwa wananchi japokuwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja ulikuwa ukiimarika.

Utawala wa Jiwe ulikuja kuzalisha changamoto mpya kwa watu kukosa ajira kwa kiwango kikubwa japo huduma zilianza kuimarika kidogo.

Nachokiona kitabadilika kwenye serikali hii ni lugha tu ya namna ya kuwasiliana na wananchi kutoka kwenye Amri kuja kwenye maombi tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom