Mtu Pekee aliyekataa teuzi wakati wa Magufuli ni ndugu Maswanya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
4,078
2,000
Katika Historia, ndugu Ally Masoud Maswanya ndio Mtu pekee alikataa Uteuzi wa Rais Magufuli.

Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya lakini siku ya kwenda kuapa hakutokea. Walipompigia simu akaape, akasema yupo Ofisini anadeal na wateja wake.

Alikuwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo kanda ya Ziwa. Sijui sasa hivi yupo wapi na anafanya nini.

1617205337199.png

Pia Soma: Mkuu wa Wilaya Mteule wa Mbozi, Ally Masoud Maswanya ajiuzulu
 
This is...

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
2,854
2,000
Siyo lazima wote tufanye kazi serikalini kama wanasiasa! Sekta binafsi ina mchango mkubwa sana kwenye uchumi.
Hakuna mahali nmesema ni lazima kila mtu afanye kazi serikalini.

Km ambavyo ni vigumu wote tukawa sekta binafsi.

Unaweza kuwa serikalini au sekta binafsi inategemea na malengo yako,au mazingira,hali ya elimu inaweza kusababisha uwe kati sehemu hizo mbili.

Siyo sahihi kusema UDC siyo potential.Siyo potential kwako kwa mwingine ni fursa adhimu .
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
12,034
2,000
Katika Historia, ndugu Ally Masoud Maswanya ndio Mtu pekee alikataa Uteuzi wa Rais Magufuli.

Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya lakini siku ya kwenda kuapa hakutokea. Walipompigia simu akaape, akasema yupo Ofisini anadeal na wateja wake.

Alikuwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo kanda ya Ziwa. Sijui sasa hivi yupo wapi na anafanya nini.

Pia Soma: Mkuu wa Wilaya Mteule wa Mbozi, Ally Masoud Maswanya ajiuzulu
Huyu na watu wa namna hiyo lazima alikuwa na baggage fulani ambayo hakutaka ijulikane. Tatizo lake ni kwamba aliupenda uDC ndipo akateuliwa, ila baada ya kuteuliwa akagundua kuwa ana mifupa kwenye kabati lake ambayo hataki ijulikane, na wakati huo akawa hawezi kuondoa jina lake kwenye uteuzi tena, ndipo akaamua kutohudhuria uapishwaji. Mtu kabla ya kuteuliwa, huwa unapewa taarifa kuwa mkuu anataka kukuteua kwenye nafasi fulani, je unaiweza. Mteuliwa mtumianiwa lazima akiri kuwa kweli anaweza kuimudu nafasi ie kabla uamuzi wa mwisho haujafanyika.

Sasa kama yeye alisema anaiweza nafasi ile, halafu siku ya mwisho ndipo miguu ikaganda, basi alikuwa na matatizo ambayo hatutayajua!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom