Mtu mzima anapaswa kunywa maji kiasi gani kwa siku? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu mzima anapaswa kunywa maji kiasi gani kwa siku?

Discussion in 'JF Doctor' started by Ork, May 4, 2012.

 1. Ork

  Ork Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  JF Doctors!
  Naomba kujua kiasi cha maji kinachotakiwa mwilini kwa mtu mzima kwa siku.

  Nauliza hivyo kwa sababu leo nimekunywa maji lita Tatu na nusu (from 8am hadi 8pm).

  Naombeni majibu yenu
   
 2. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,185
  Likes Received: 1,903
  Trophy Points: 280
  Maji hunywewa kulingana na Uzito

  Sasa Tufanye Mahesabu kidogo.

  Mfano: Mwenye uzito wa 75kg

  ¤Badili 75kg kwenda kwenye Aunsi.. Na aunsi 1=31.25 ml

  sasa kupeleka kwenye Aunsi zidisha 75 mara 2.2
  75x2.2=165 aunsi

  ¤Tafuta nusu ya Aunsi kwa kugawanya na 2
  165/2 ambapo ni sawa na 82.5

  ¤Sasa gawanya kwa Mfululizo utakaotaka kuufuata Kunywa Maji kwa Siku. Kama ni Mara 3,5,au 8 sasa Tuchukue mfululizo wa Mara 8. 82.5/8 sawa na 10.3 aunsi

  ¤Badili Aunsi kuwa Miligramu
  1Aunsi=31.25
  10.3 x 31.25=322Ml

  Kwahiyo mwenye Uzito wa 75kg anatakiwa kunywa Maji 322ml Mara 8 kwa Siku.

  GOOD LUCKY.
   
 3. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Anzia lita tatu hadi tano au zaidi!
   
 4. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Total liquid intake iwe seven pints, at least four of those should be water.
   
 5. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Pints ndiyo ujazo wa debe au pipa?Wengi hatujui vipimo vya Uk.
   
 6. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Kama alivyokujibu RGFOREVER ndivyo inavyopaswa kuwa, usifanye tofauti, lakini mhimu ni kuhakikisha ukishakunywa maji, basi maji yanatakiwa yabaki mwilini walau masaa 2 mpaka 2 na nusu kabla ya kwenda kukojoa, utafanyaje?, bonyeza link ifuatayo ukajifunze zaidi, usisite kuuliza tena: jitibu kwa kutumia maji | maajabu ya maji
   
 7. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  mkuu lita 5 utaishiwa madini na viinilishe vyote mwilini.maximum iwe ni lita 3.5 ndani ya masaa 24.
   
Loading...