Mtu mwingine katika biashara ya vitu vidogovidogo mbalimbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu mwingine katika biashara ya vitu vidogovidogo mbalimbali

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by marandu2010, Sep 23, 2010.

 1. marandu2010

  marandu2010 JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 1,177
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  habari wakuu,
  naomba mnisaidie mawazo ya jinsi ya kuifanya biashara ya duka la vitu mbalimbali kwa kumwajiri mtu mwingine bila yeye kukuibia,,ni swali ambalo mimi linaniumiza kichwa,,maana wengine huweka vitu vyao na kuviuza wakikwambia biashara ngumu.

  naomba mtu mwenye uzoefu wa kuanya biashara hii kwa kumwajiri mtu mwingine anisaidie jinsi anavyofanya,,ikumbukwe mimi niko mbali na nimebanwa na shughuri nyingine na siwezi kuwa natembelea kule mara kwa mara.pia nimeamua kuifanya biashara hii kutokana na vile ujazo wa mfuko wangu kuwa ni mdogo.

  natanguliza shukrani zangu kwa wakuu watakaonisaidia katika hili.
   
 2. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  swali zuri lakini gum. Mfanya kazi ni mtu muhimu sana katika maendeleo ya biashara. "Kidole kimoja hakivunji chawa". unakumbuka? Usipomuamini ni mtihani kwenu nyote. maswali matatu yafuatayo ni ya kujiuliza wakati shaka inapoanza. 1. Je kunakishawishi gani au sababu ya kumfanya mtumishi aibe. 2. Je nafasi ipo ya kuiba? 3. Tabia na akili ya mfanya kazi. je mtu kama yeye anaweza kufanya kitu hicho kibaya. Wafanya kazi ni muhimu sana ukiwahishimu, uwathamini nadhani mbinu nzuri za kujenga uhusiano.

  Muhimu: Tengeneza daftari la duka. Ukinunua kitu cha kuweka dukani, unaandika tarehe, bidhaa, thamani yake na idadi yake. Kwa mfano Terehe 9/23/2010 Vikombe 12 Shs 120.00 kiwastani gharama na vitu alivonunua. Hii itakusaidia kujua gharama za duka na faida kila mwisho wa mwezi. Hivo utajua unaendelea au umesimama au unarudi nyuma. Na mfanya kazi atakupa mawazo ya kuendelea. Bila hivyo, kichwa kitaakuma mpaka lyamba.
   
 3. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
  Kwanza mwamini huyo mfanyakazi wako. Ni muhimu kuifanya hiyo biashara wewe mwenyewe kukuwezesha kujua trend ya mauzo mkiwa pamoja na huyo mfanyakazi, tufanye mwezi mmoja. Fanya projection ya mauzo unayotegemea kuyafanya kila mwezi kwa miezi 6. Mpatie hayo matarajio ya mauzo huyo mfanyakazi. Kama kutakua na tatizo ya mauzo kwenye kila mwezi baada ya miezi sita unaweza tafuta muda tena wa kukaa pamoja na mfanyakazi wako uone biashara inaendaje... Ni muhimu sana kumoonyesha mfanyakazi wako kwamba unamuamini na yeye aamini hivyo hivyo. Kama anapata cha juu nje ya projection zako hayo ni maruppurupu yake na yatamfanya apende zaidi kazi yake. Kila la kheri mkuu!
   
Loading...