Mtu mweusi aliyekamatwa na kuvutwa nyuma ya farasi ashitaki mamlaka ya jiji la Texas akidai fidia ya dola milioni 1

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Nelly.jpg

Mtu mmoja mwenye asili ya Kiafrika ameishitaki Mamlaka ya jiji la Texas baada ya polisi waliomkamata kumfunga kamba na kumvuta nyuma ya farasi, akitaka kulipwa fidia ya dola milioni moja (sawa na zaidi ya shilingi bilioni 2) akisema kuwa alihisi kunyanyaswa na woga baada ya kukamatwa.

Katika shauri lililofunguliwa wiki iliyopita katika Mahakama ya Kaunti ya Galveston kwa niaba ya Donald Neely mwenye umri wa miaka 44, kitendo cha polisi kinadaiwa kumsababishia Neely maumivu ya kimwili na kihisia. Picha za tukio hilo lililotokea zaidi ya miezi 14 iliyopita zinamwonesha Neely akiwa amefungwa kamba zilizounganishwa na pingu akitembea nyuma ya afisa wa polisi aliyekuwa juu ya farasi, kama ilivyokuwa wakati wa biashara ya utumwa.

Neely, ambaye hakuwa na pahala pa kuishi wakati huo, alikamatwa akiwa amelala kando ya njia na kushtakiwa kwa makosa ya uzururaji na kupelekwa katika eneo kituo cha muda kilichokuwepo katika eneo hilo.

Katika video moja iliyorekodiwa kutoka katika kamera ya polisi, afisa mwingine anasikika akisema kuwa kumtembeza Neely mtaani nyuma ya farasi akiwa amefungwa kamba kunaweza kuonekana kama jambo baya.

Shauri hilo linailaumu mamlaka ya mji pamoja na idara ya polisi kwa uzembe, ikisema kuwa afisa huyo wa polisi alitakiwa kufahamu kuwa kumkamata Neely 'kama mtumwa' si jambo zuri. Hata hivyo, taarifa ya Mkuu wa Polisi imesema kuwa mbinu hiyo ya kukamata ni nzuri na inafaa kutumika katika mazingira fulani.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa afisa huyo wa polisi hakutakiwa kutumia mbinu hiyo kwani idara ya polisi ilibadili mbinu zake za ukamataji na kuacha kutumia mbinu hiyo wakati fulani. Uchunguzi wa Idara ya Polisi umesema kuwa afisa huyo wa polisi hakufanya makosa yoyote.

Maafisa wa jiji la Texas hawakutoa tamko lolote kuhusiana na shauri hilo, wakati likitarajiwa kutajwa mwezi Januari 2021.
Chanzo: Al Jazeera
 
Sorry hatupatikani kwa sasa jaribu tena kupost baadae kwa sasa tuko bize na uchunguzi oh samahani namaanisha uchaguzi
 
Wazungu hawawezi kuacha biashara ya utumwa na kuuwa watu weusi hata wasemeje.
 
Wazungu hawawezi kuacha biashara ya utumwa na kuuwa watu weusi hata wasemeje.


Cha ajabu huyo huyo mtu mweusi anamthamini mzungu kuliko mwarabu,.mzungu ni dhahabu kwa mtu mweusi hata amnyee na kumharishia usoni mwake sawa tu, isitoshe mtu mweusi anaamini mzungu hakufanya biashara ya utumwa,


Sipati picha angelifanya mwarabu weeeee mbona zingefika page mia na kuendelea 🤣🤣🤣🤣 mitusi kama yote.
 
Back
Top Bottom