Mtu mweusi akinyanyaswa na wazungu huko Marekani ni Dhambi, ila Mtu mweusi akinyanyaswa na Waafrika wenzake huku Afrika siyo dhambi

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
Hivi karibuni kuna Mtu mweusi ametendwa vibaya huko Marekani kitendo kilichozusha fujo Kubwa, huku watu wakikemea kitendo hicho. Lakini cha ajabu ndani ya Afrika Waafrika wenyewe wakinyanyasana kwa kiasi kikubwa sana.

Vitendo Vya kunyanyasani ndani ya Afrika ni jambo la kawaida lakini cha hakuna nguvu ya pekee ya kukemea vitendo hivi. Tumeshuhudia mambo mengi ya kikatili wanayo fanyiwa watu tena matendo haya yanatendwa na watu wenye mamlaka. Kuna watu wanauawa wengine wanatekwa, wengine wananyanyaswa kwa namna mbali mbali, lakini hakuna nguvu ya pekee ya kukemea matendo hayo.

Huko Afrika ya kusini serikali ya makaburu iliwanyanyasa sana Waafrika, kiasi kwamba Waafrika wote tuliungana kukemea vitendo hivyo, cha ajabu matendo Yale Yale yaliyotendwa na makaburu leo Waafrika wanayatenda tena kwa hali ya juu,kiasi kwamba tumewazidi wale tuliokuwa tunawakeme.

Muda Fulani najiuliza inamaana tunachukia kutendewa vibaya na wazungu huku tukifurahia kutendeana vibaya sisi kwa sisi?

IMG-20191227-WA0024.jpeg
 
Umeona nilichokiona naishi South Africa zaidi ya mwaka 20 huu Hali mbaya sna ubaguzi kati mweusi na mweusi upo juu na hali ni mbaya sna tatizo ni km tumeufumbia macho...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko Afrika ya kusini serikali ya makaburu iliwanyanyasa sana Waafrika, kiasi kwamba Waafrika wote tuliungana kukemea vitendo hivyo, cha ajabu matendo Yale Yale yaliyotendwa na makaburu leo Waafrika wanayatenda tena kwa hali ya juu,kiasi kwamba tumewazidi wale tuliokuwa tunawakeme.
Actually waafrika ni makatili kuzidi Makaburu na wazungu! Nkurunzinza, Mobutu JIWE, Museveni, Kagame, Bokasa Jameh , Kenyeta, Mogadishu, Misri etc etc. Miafrika mikatili USIOMBE!
 
Unafiki, ujinga, upumbavu, ushabiki wa vyama au kikundi flan, uonga, hiv ndio vinavyotusumbua
 
Back
Top Bottom