Cha kushangaza zaidi inasemekana kuwa sura yake ya kisogoni haikuweza kula wala kuongea chochote na hata ikijaribu kuongea maneno yalikuwa hayasikiki.
-----
Edward Mordake wa Uingereza alizaliwa mwaka 1887 akiwa na sura mbili, moja ya kawaida na nyingine ilikuwa kisogoni mwake. SUra hiyo ya pili ilikuwa haiwezi kuona, kula wala kuongea kwa sauti, isipokuwa ilikuwa ikitabasam pale alipokuwa na furaha na kulia pale alipokuwa na huzuni.
Madaktari walishindwa kugundua nini cha kufanya lakini mwenyewe alitaka wamfanyie upasuaji wa kumuondoa, kitendo ambacho kilikuwa kigumu kwao. Mwenyewe alikuwa akisema kuwa nyakati za usiku sura hiyo ilikuwa ikimnong'oneza maneno ambayo mtu anaweza kuyaongea akiwa kuzimu tu.
Mwaka 1910 alifariki na habari zinasema kuwa aliamua kujiua.