Mtu mwenye maradhi ya Moyo anaweza kufa wakati wa kufanya mapenzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mtu mwenye historia ya ugonjwa wa moyo anaweza kufa wakati wa tendo hilo kwasababu moyo wake utafanya kazi ngumu kuliko wakati wa kawaida
Sababu za mara kwa mara za magonjwa ya moyo, hususan kwa wanawake wenye zaidi ya miaka 50 na wanaume wenye miaka arobaini ni shinikizo la damu , uvutaji wa sigara, kisukari, kiharusi na magonjwa mengine.

Sababu nyingine ambayo mara nyingi husababisha magonjwa ya moyo ni msongo mkubwa wa mawazo.
Mshtuko wa moyo wakati wa tendo la ndoa mara nyingi unawakumba wanaume kuliko wanawake, utafiti unaonyesha.

Lakini tendo la ndoa ni kichocheo adimu cha mshutuko wa moyo .
Ni visa 34 tu vya mshtuko wa moyo kati ya 4,557 hutokea wakati au ndani ya saa moja ya kujamiiana na 32 ya wale walioathiriwa walikuwa wanaume.

Sumeet Chugh, wa Taasisi ya Moyo ya Cedars-Sinai Heart Institute alisema utafiti wake ni wa kwanza kutathmini shughuli za ngono kama sababu inayowezesha kusababisha mshutuko wa moyo.Utafiti wake huo ulichapishwa katika ripoti ya BBC Novemba 2017

Utafiti wake huo uliwasilishwa katika mkutano wa American Heart Association wakati wa kutathmini vichocheo vinavyosababisha mshtuko wa moyo .

Hatua hiyo hutokea wakati moyo unapopata matatizo na kuacha kupiga . Mtu hupoteza fahamu na kukosa kupumua Iwapo hatofanyiwa utaratibu wa CPR ili kumuokoa
Mshutuko wa moyo ni tofauti na shambulio ambalo hukumba moyo na kuzuia damu kuufikia
 
Back
Top Bottom