Mtu mwenye deni la trillioni 100 ni tajiri kuliko mwenye bilioni 100 kwenye akaunti yake, kuna mtu anabisha?

Utajiri unapimwa kwa assets(mali) ulizonazo, kwa ufupi kabisa ASSETS = LIABILITIES + EQUITY....... Yaaani Mali(asset)zako ni jumla madeni yako(liability) + mtaji wako(Equity)

Mkopo ni LIABILITY lakini sio mbaya kama unavyodhani, ntaeleza hapa.

Kukopa kiTAJIRI ni pale unakopa then unaconvert part kubwa ya mkopo kuwa assets(mali) mf: biashara, mitambo, ardhi, majengo, hatimiliki etc. na sehem ndogo kuwa matumizi ya kawaida.

Kukopa kiMASKINI ni pale unapokopa then unaconvert part kubwa ya mkopo kuwa matumizi ya kawaida(expenses) mf: matanuzi na bata, kutoa misaada, safari za gharama, manunuzi ya vitu vinavyokwisha thamani haraka etc. na sehem ndogo kuwa mali.

So kujibu swali lako, mwenye deni la Trillioni 100 ni tajiri kuliko mwenye cash Billioni 100 kama alikopa kiTAJIRI kwa sababu atakuwa na mali zenye thamani kubwa kuliko mwenye cash ya Bil.100.

Ukitaka kuelewa hili, chunguza vitabu vya mahesabu vya makampuni makubwa na matajiri wote unaowajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maelezo yako kidogo hayajanyooka. Utajiri wa mtu unapimwa kwa NET WORTH yake at one moment in time, ambayo ni TOTAL ASSETS - TOTAL LIABILITIES. Kwa swali hilo huwezi kuwa na jibu la uhakika kwani hatujaambiwa kuwa kama wana assets zingine beside cash na wamezipataje

Bloomberg Billionaires Index
 
Kati ya bakkressa na Serikali ya Tanzania nani ana deni kubwa? Na je, si kweli kwamba kuna wakati serikali huwa inakosa hata senti kwenye akaunti yake baada ya kulipa mishahara ya watumishi?
Ndio maana huwa kuna limits zimewekwa,(Debt to GDP ratio) kuna limit ukivuka unaingia kwenye hatari ya kutokopesheka,Ugiriki ilishawakuta hii,Sasa aje mtu akwambie kipindi kile Ugiriki ina deni la $2trilion na Saudi Arabia yenye Surplus ya $800billion kwenye reserve account,eti Ugiriki ni bora kuliko Saudi Arabia??.Utakuwa finacial analyst wa hovyo hujawahi tokea duniani.Kuna vitu vya kuangalia kabla ya kumkopesha mtu mwenye madeni
1.Madeni yake anayalipa?(sio kwamba yupo kwenye hatari ya kufilisiwa)
2.Kama anayalipa vizuri,je ana uwezo wa kulipa madeni mapya akikopeshwa(Hapa tunaangalia a/c transactions na balances baada ya kulipa madeni).
Haya mambo sio black and white kama tunavyodhani.Mfano kuna ile issue ya Mo dewji kumnyima Kingwangala mkpo wa pikipiki.Inawezekana kabisa Mo alifanya analysis zake akaamua kutompa kwa sababu ambazo ni sahihi kabisa..Hivi ndio mambo huwa.
Ila kama unataka kopesha kwa kutumia imani,jiandae kwa lolote
 
Mifano yako hailingani na mada husika kabisa!.

Yani unamlinganisha Bakhressa (Mtu binafsi) anayeweza firisika muda wowote watu wakamgawana mali zake na Serikali (Taasisi) isiyoweza firisika ikagawanwa mali zake!..

Hebu nikuulize swali tena
ushawahi sikia Serikali imefirisika!?. Ushawahi sikia Serikali imefirika wananchi wakagana mali zake!?..

Serikali ni TAASISI HAIWEZI FIRISIKA lakini Bakhressa ni MTU BINAFSI muda wowote ANAFIRISIKA ile kampuni ikauzwa kwa highest bidder!..
Hahaha, mbona ugiriki ilifilisika hadi wakapewa bailout na EU
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom