Mtu Mwenye Aleji na Pesa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza anawaumiza vichwa madaktari ambao hawajui imekuwaje mtu mmoja akawa na aleji na karibia kila kitu duniani kuanzia pesa, vyakula na hata maji.
Yvonne Simon mwanamke wa nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 33 amewashangaza madaktari kwa jinsi alivyo na aleji nyingi kuliko kawaida.

Yvonne ambaye ni mama wa mtoto mmoja ana aleji na wino unaotumika kwenye pesa za noti hali ambayo imemfanya awe anavaa glovu kabla ya kuzishika pesa ili kuepuka mwili wake kuvimba na ngozi yake kutoa vipele.

Mbali ya noti, Yvonne pia ana aleji na pesa za sarafu hivyo wakati wote anapokuwa hana glovu zake karibu hulazimika kutumia kadi za benki anaponunua au kulipa kitu.

Aleji zake hazijaishia kwenye pesa tu, Yvonne ana aleji na maji ya mvua, wakati wote hulazimika kutembea na mwamvuli ili kuepuka kunyeshewa na mvua.

Hata vyakula navyo husababisha madhara kwa mwili wake, miongoni mwa vyakula ambavyo ana aleji navyo ni samaki,maziwa, chai, kahawa, uji, mafuta ya alizeti, vitunguu, nyanya, machungwa, pipi,chocolate na vyakula vinavyotokana na ngano.

Yvonne pia ana aleji na pafyumu na vitu vyenye dhahabu au shaba.

Alianza kusumbuliwa na aleji hizo alipokuwa na umri wa miaka minane na tangu wakati huo hadi leo amekuwa akiishi maisha ambayo si ya kawaida.

Yvonne ameishafanyiwa uchunguzi na madaktari wengi katika kutafuta tiba ya aleji zake ili aweze kuishi maisha ya kawaida yenye furaha lakini hadi sasa hakuna matibabu yaliyofanikiwa kuziondoa aleji zake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom