Mtu mnafiki utamtambuaje?

vamda

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
858
533
Ndugu wana JF. Tunapoishi duniani huwa tunazungukwa na watu wa aina tofauti; wengine wema na wengine wabaya. Napenda kufahamishwa ili niweze kumtabua mtu mnafiki
 
Ukitaka kuwa na amani katika maisha yako usijali nani yuko real au nani mnafiki,binadamu walio wengi ni wanafiki.Ukitafuta nani wa kweli nani mnafiki unaweza kushangaa umebaki peke yako.Wengi waliotuzunguka wanatuchekea hiyo basi tu lakini ukijua wanavyotuwazia utaogopa.
Ni kweli kabisa ila kuna wengine wamezidi bana ukigeuza mgongo tu wasengenywa mwe!!
 
Ndugu wana JF. Tunapoishi duniani huwa tunazungukwa na watu wa aina tofauti; wengine wema na wengine wabaya. Napenda kufahamishwa ili niweze kumtabua mtu mnafiki

... Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
(Matthew 7.5)

"Thou hypocrite, first cast out the beam out of thine own eye; and then shalt thou see clearly to cast out the mote out of thy brother's eye."
(Matthew 7.5)

Au, unawezaje kumwambia mwenzako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi katika jicho lako, na huku huioni boriti iliyoko katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako.
(Luke 6:42)

ZIJUE TABIA ZA MNAFIKI!

Bwana Yesu alitoa hotuba moja kali sana pale alipokuwa amekusanya makutano wengi nae akapanda katika mlima na kuanza kuwafundisha watu.

Katika mafundisho yale Bwana Yesu aliwagusa watu aliowaita WANAFIKI, kwa kiingereza wanaitwa HYPOCTRITES.

Mnafiki kwa lugha rahisi ni mtu anaejifanya kuwa na tabia fulani nzuri lakini kiuhalisia tabia hyo hana.

Mathayo 6, Bwana Yesu amejaribu kusema baadhi ya wanafiki katika makutano yale.

1. Watu wajifanyao wema
Bwana Yesu anasema "Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni"

Kuna watu kwenye jamii zetu ni wanafiki sana kwa kujifanya wao ni wema sana katika jamii ili waonekano wao ni wema na bora kuliko wengine. Tena kwa makusudi wanajifanyisha wema huo ili watu wawasifu na kuwapigia makofi.

Kuna watu wako tayari hata kwenye makanisa wafanye mambo ili tu waumini wamuone kuwa yeye ni bora na ni mwema kuliko wengine. Kuna watu hawako tayari kuwasaidia masikini/wenye uhitaji lakini wako tayari kuchangia kwenye hafla za watu ili wajulikane wao ni wema mbele ya jamii.

Kuna watu nakwambia wako tayari kufanya kazi ya Mungu makanisani ili tu wasifiwe na watu na wasiposifiwa hiyo kazi hawaihitaji, nakwambia wewe ni mnafiki. Na hakuna neno linauma kama kuambiwa wewe ni mnafiki. Lakini ukweli ndiyo huo kama unataka kufanya mambo ili uonekane machoni pa watu wewe ni mnafiki na huna thawabu mbele za Mungu. Saidia maskini na wajane na wahitaji pasipo kutaka uonekane machoni pa watu maana yeye aonaye siri anakuona na atakupa thawabu.

2. Kwenye kutoa sadaka
Ndugu yangu kuna watu hadi kwenye kutoa sadaka wanataka watu wengine wajue kwamba jamaa katoa sadaka kiasi gani leo! Yesu akasema mstari wa 2, "Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu"

Kumbe kuna mijitu inatoa sadaka ili watu wawatukuze kuwa jamaa katoa fedha nyingi. Kuna watu nakuambia hata kwenye sadaka za changizo fulani fulani wanataka watoe sadaka zao zisikiwe na kila mtu ili tu jamaa atukuzwe.

Nakwambia wewe ni mnafiki, na huna thawabu mbele za Mungu.
Kwenye sura hiyo ya sita yameelezwa mengi kuhusu wanafiki. Ndugu yangu jiepushe kuwa mnafiki. Kuna mambo mengi ya kiungu waweza kuyafanya kimya kimya na ukapata thawabu.

Usifanye ili watu wakuone. Usimnunulie mchungaji au Padri wako kitu fulani na utake watu wajue ili wakusifu kwamba nawe ni mtoaji! Wewe ni mnafiki tu. Fanya kimya kimya na ninakuhakikishia Mungu wa mbinguni atakupa thawabu.
Katika jamii zetu wanasiasa ni kati ya watu wanafiki sana siku za hivi karibuni. Wanazungumza kuhusu amani lakini wanachokimaanisha sicho hata kidogo.

Wanasiasa kwenye majukwaa wana hubiri amani wakishuka wanaenda kupanga mikakati ya kuwagawa watu kwa sababu ya makabila, dini na maeneo watokako. Wana siasa mnaofanya hivyo ninyi ni wanafiki tu, hamna lolote. Na Mungu aliye hai atawalipa na udhalimu wenu. Na ninawaambia fungu lenu halimo katika watanzania wanaotaka amani ya Taifa hili na mbingu ziwakemee.

Mungu akubariki sana.
 
Ukitaka kuwa na amani katika maisha yako usijali nani yuko real au nani mnafiki,binadamu walio wengi ni wanafiki.Ukitafuta nani wa kweli nani mnafiki unaweza kushangaa umebaki peke yako.Wengi waliotuzunguka wanatuchekea hiyo basi tu lakini ukijua wanavyotuwazia utaogopa.

Dah! kweli.
 
Ndugu wana JF. Tunapoishi duniani huwa tunazungukwa na watu wa aina tofauti; wengine wema na wengine wabaya. Napenda kufahamishwa ili niweze kumtabua mtu mnafiki

Hatimizi ahadi! Mwongo!! (hizi ni miongoni mwa dalili)
 
... Mnafiki wewe! Ondoa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako na hapo ndipo utaona waziwazi kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilichoko jichoni mwa ndugu yako.
(Matthew 7.5)

"Thou hypocrite, first cast out the beam out of thine own eye; and then shalt thou see clearly to cast out the mote out of thy brother's eye."
(Matthew 7.5)

Au, unawezaje kumwambia mwenzako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi katika jicho lako, na huku huioni boriti iliyoko katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako.
(Luke 6:42)

ZIJUE TABIA ZA MNAFIKI!

Bwana Yesu alitoa hotuba moja kali sana pale alipokuwa amekusanya makutano wengi nae akapanda katika mlima na kuanza kuwafundisha watu.

Katika mafundisho yale Bwana Yesu aliwagusa watu aliowaita WANAFIKI, kwa kiingereza wanaitwa HYPOCTRITES.

Mnafiki kwa lugha rahisi ni mtu anaejifanya kuwa na tabia fulani nzuri lakini kiuhalisia tabia hyo hana.

Mathayo 6, Bwana Yesu amejaribu kusema baadhi ya wanafiki katika makutano yale.

1. Watu wajifanyao wema
Bwana Yesu anasema "Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni"

Kuna watu kwenye jamii zetu ni wanafiki sana kwa kujifanya wao ni wema sana katika jamii ili waonekano wao ni wema na bora kuliko wengine. Tena kwa makusudi wanajifanyisha wema huo ili watu wawasifu na kuwapigia makofi.

Kuna watu wako tayari hata kwenye makanisa wafanye mambo ili tu waumini wamuone kuwa yeye ni bora na ni mwema kuliko wengine. Kuna watu hawako tayari kuwasaidia masikini/wenye uhitaji lakini wako tayari kuchangia kwenye hafla za watu ili wajulikane wao ni wema mbele ya jamii.

Kuna watu nakwambia wako tayari kufanya kazi ya Mungu makanisani ili tu wasifiwe na watu na wasiposifiwa hiyo kazi hawaihitaji, nakwambia wewe ni mnafiki. Na hakuna neno linauma kama kuambiwa wewe ni mnafiki. Lakini ukweli ndiyo huo kama unataka kufanya mambo ili uonekane machoni pa watu wewe ni mnafiki na huna thawabu mbele za Mungu. Saidia maskini na wajane na wahitaji pasipo kutaka uonekane machoni pa watu maana yeye aonaye siri anakuona na atakupa thawabu.

2. Kwenye kutoa sadaka
Ndugu yangu kuna watu hadi kwenye kutoa sadaka wanataka watu wengine wajue kwamba jamaa katoa sadaka kiasi gani leo! Yesu akasema mstari wa 2, "Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu"

Kumbe kuna mijitu inatoa sadaka ili watu wawatukuze kuwa jamaa katoa fedha nyingi. Kuna watu nakuambia hata kwenye sadaka za changizo fulani fulani wanataka watoe sadaka zao zisikiwe na kila mtu ili tu jamaa atukuzwe.

Nakwambia wewe ni mnafiki, na huna thawabu mbele za Mungu.
Kwenye sura hiyo ya sita yameelezwa mengi kuhusu wanafiki. Ndugu yangu jiepushe kuwa mnafiki. Kuna mambo mengi ya kiungu waweza kuyafanya kimya kimya na ukapata thawabu.

Usifanye ili watu wakuone. Usimnunulie mchungaji au Padri wako kitu fulani na utake watu wajue ili wakusifu kwamba nawe ni mtoaji! Wewe ni mnafiki tu. Fanya kimya kimya na ninakuhakikishia Mungu wa mbinguni atakupa thawabu.
Katika jamii zetu wanasiasa ni kati ya watu wanafiki sana siku za hivi karibuni. Wanazungumza kuhusu amani lakini wanachokimaanisha sicho hata kidogo.

Wanasiasa kwenye majukwaa wana hubiri amani wakishuka wanaenda kupanga mikakati ya kuwagawa watu kwa sababu ya makabila, dini na maeneo watokako. Wana siasa mnaofanya hivyo ninyi ni wanafiki tu, hamna lolote. Na Mungu aliye hai atawalipa na udhalimu wenu. Na ninawaambia fungu lenu halimo katika watanzania wanaotaka amani ya Taifa hili na mbingu ziwakemee.

Mungu akubariki sana.
Ahsanteeeeeeeeeee
 
kama wewe siyo mnafiki basi una ugonjwa wa perfectionism ambao pia ni hatari sana! ktk sayari hii ambaye simnafiki hakuna.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom