Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,505
Mtu mmoja Athanas Telemka ameuawa kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto, na kundi la watu waliokuwa wakifanya vurugu kwenye kijiji cha Kazila, kata ya Mwazye wilayani Kalambo, wakichoma moto nyumba na kupora mali, kwa kisingizio cha kumsaka aliyemuua mwanamke mmoja mkazi wa kijiji hicho kwa njia ya kishirikina, na kuishia kumuua mzee huyo aliyekuwa akiwazuia kufanya vurugu hizo zilizosababisha uharibifu mkubwa.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bw. Zelote Steven akihudhuria mazishi ya marehemu Telemka, akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, akiongea na wananchi wa kijiji cha Kazila amesema tayari jeshi la polisi linawashikilia watu tisa wakiwemo wenyeviti wa vitongoji viwili vya Kalemba na Sangu, waliosemekana kuwa vinara wa vurugu hizo zilizosababisha nyumba zaidi ya tano kuchomwa moto na mali kuporwa.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kazila akiwemo afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw Alfred Kalumbwe, wamesema vurugu hizo zilianza mara baada ya mazishi ya mwanamke mmoja mkazi wa kijiji hicho, na kusemekana kuwepo kwa mwananchi mmoja aliyehusika na kifo hicho kwa njia ya kishirikina, na ndipo walipoanza kumsaka hata hivyo alifanikiwa kutoroka, na wao kuishia kuchoma nyumba moto na kupora mali yakiwemo mazao mbalimbali.
Chanzo: ITV