Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto na watu waliokuwa wakifanya vurugu mkoani Rukwa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Mtu mmoja Athanas Telemka ameuawa kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto, na kundi la watu waliokuwa wakifanya vurugu kwenye kijiji cha Kazila, kata ya Mwazye wilayani Kalambo, wakichoma moto nyumba na kupora mali, kwa kisingizio cha kumsaka aliyemuua mwanamke mmoja mkazi wa kijiji hicho kwa njia ya kishirikina, na kuishia kumuua mzee huyo aliyekuwa akiwazuia kufanya vurugu hizo zilizosababisha uharibifu mkubwa.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bw. Zelote Steven akihudhuria mazishi ya marehemu Telemka, akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, akiongea na wananchi wa kijiji cha Kazila amesema tayari jeshi la polisi linawashikilia watu tisa wakiwemo wenyeviti wa vitongoji viwili vya Kalemba na Sangu, waliosemekana kuwa vinara wa vurugu hizo zilizosababisha nyumba zaidi ya tano kuchomwa moto na mali kuporwa.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kazila akiwemo afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw Alfred Kalumbwe, wamesema vurugu hizo zilianza mara baada ya mazishi ya mwanamke mmoja mkazi wa kijiji hicho, na kusemekana kuwepo kwa mwananchi mmoja aliyehusika na kifo hicho kwa njia ya kishirikina, na ndipo walipoanza kumsaka hata hivyo alifanikiwa kutoroka, na wao kuishia kuchoma nyumba moto na kupora mali yakiwemo mazao mbalimbali.

Chanzo: ITV
 

chendelela

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
932
1,000
Ndugu zangu hawa wamekuwa na ujasiri wa ajabu sana kuua hawaoni shida,ee Mungu hiki kizazi tunakwenda wapi!
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
8,553
2,000
kuna vijiji kama vile serikali hakuna na pia hawana hata hofu ya Mungu wanajichukulia sana sheria mkononi kwa mambo jambo lolote lile..
 

Geofrey Maseta

JF-Expert Member
Nov 24, 2015
1,116
2,000
Yaani hicho kijiji toka kitambo story zao huwa ndo hzo hzo ...1994 niliwahi fika hicho kijiji napo nilishuhudia mauaji ya watu watano wakiuawa kwa imani za kishirikina baada ya kaburi la kijana mmoja aliyefariki cku jana yake kufukuriwa na mwili kukutwa nje ya kaburi ....daah ile vulugu sinta kaa isahau
 

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,926
2,000
Yaani hicho kijiji toka kitambo story zao huwa ndo hzo hzo ...1994 niliwahi fika hicho kijiji napo nilishuhudia mauaji ya watu watano wakiuawa kwa imani za kishirikina baada ya kaburi la kijana mmoja aliyefariki cku jana yake kufukuriwa na mwili kukutwa nje ya kaburi ....daah ile vulugu sinta kaa isahau
mwe!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom