Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Mtu mmoja amekufa na kaya zaidi ya 350 hazina makazi katika kata ya Magaoni jijini Tanga kufuatia nyumba zao kujaa maji na kusababisha hasara kubwa ya mali na vyakula kwa waathirika.
Baadhi ya nyumba ambazo zimejaa maji hadi katika usawa wa madirishani ambapo waathirika waliokutwa katika eneo la tukio wameiomba serikali kuliangalia kwa kina suala hilo kwa sababu baadhi yao wamehifadhiwa kwa a mjirani nyakati za mchana lakini usiku hawajui mahali pa kujisitiri.
Kuhusu kifo cha mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Amani Gelege, Mwenyekiti wa Mtaa wa Usagara jijini Tanga ambapo eneo lake kuna kaya zaidi ya saba zimehifadhiwa katika baraza za nyumba za wasamaria wema amesema wakati wa uhai wake marehemu Amani alijaribu kupita katika barabara ya Somaiya yenye maji mengi ndipo alipoona maji yamemzidia akaamua kuteremka na kumezwa na maji.
Kufuatia hatua hiyo Mbunge wa Jimbo la Tanga mheshimiwa Mussa Mbaruk amesema kutokufanyika kwa vikao vya Baraza la Madiwani kwa sababu ya mgogoro wa kutafuta nafasi ya Meya kumechangia kushindwa kuwa na kamati ya huduma za dharura.