Mtu kupigwa na kuchomwa moto mbele ya askari mwenye silaha nzito, nini maana yake? Tuna Jeshi dhaifu?

Hiyo video mimi nimeikuta tu, hata hivyo binadamu sote ni ndugu katika level flani, sasa kama unaamini kumchoma mto mwizi ni haki kwanini wabunge hawapeleki muswada bungeni ili sheria ipitishww na watu wawe wanachomwa moto kwa mujibu wa sheria? Bado adhabu ya moto ni kali sana, na pia hata wewe unaweza ukachomwa moto kwa wizi wa kusingiziwa, kumbe hata hujaiba, ila wahuni wakifika hawaulizi kaiba nini na kamuibia nani, wao ni leta tairi, petrol, wanakulipua, ipo siku utayakumbuka haya maneno kipindi unaiva kama mshikaki huku ukijiona kwa kosa la kusingiziwa, remember these words.
Acha tu mkuu, bora ukutane na simba msituni kuliko binadamu wa aina hii aisee!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi wezi wameisha mpaka leo!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawajaisha na hawawezi kuisha maana hayo ndiyo maisha ya Dunia yalivyo,

Mimi nimejibu hivyo sikuwa na maana ya kutetea kitendo cha kujichukulia sheria mkononi na kuchoma mtu moto kwa kisingizio kuwa ni mwizi la hasha! Lengo langu la kusema kuwa hali hii ipo enzi na enzi ni kutokana na baadhi ya wachangiaji kuanza kupotosha kwa kusema kuwa Wananchi wamechoka ndio maana matukio haya yanatokea kwa sasa, wanataka kutuaminisha kuwa uchomwaji wa waharibifu wa wizi umeanza ndani ya utawala wa JPM.

NB: Kujiamulia kuchoma moto mtu si sahihi mimi kuna Ndugu yangu alipigiwa yowe mnadani kuwa ni mwizi, na akaanza kupokea kichapo kutoka kwa raia wenye hasira kali, kipindi hicho mimi nilikuwa mdogo sana na niliposikia kuwa kuna mwizi anapigwa nilishangilia sana kwa kusema ngoja akomeshwe. Alipokea kichapo haswa, lakini huwezi amini ile ilikuwa mbinu ya wezi kumlainisha baada ya kutafuta kila namna ya kumwibia pesa zake bila mafanikio, walichoamua ni kumwita mwizi ili aweze kuchapika alainike na wachukue pesa kuikaini. Na walifanikiwa kwani baada ya kichapo kuanza tu wao walilenga kuchapa mkono ulokuwa unalinda mfuko wenye pesa.

Bahati nzuri huyu ndg yangu Mungu alimuokoa, ilikuwa ni bahati tu, kwasababu kwa kipindi kile ukishapigwa yowe ya mwizi mnadani ilikuwa ni lazima afe na kuchomwa. Kwa wenyeji wa Mwanza mnada wa Igoma enzi za early and late 90'S watakubaliana nami.
 
Aisee, mimi kuna vibaka wawili kipindi nipo chuo walinifanyia huo uhuni kwenye moja wapo ya kumbi za starehe, bahati nzuri mabaunsa wa club waliingilia kati na kunitoa nje na kuanza kunijoji pamoja na yule kibaka aliyenituhumu kwamba mimi nimemuibia, ikabainika sikuwa na hatia na kiliichoniokoa ni jinsi nilivyokuwa smart, sikufanania kabisa na walichonituhumu, ila ni Mungu tu alisaidia, vinginevyo sijui ingekuwaje, maana wadau hawakutaka hata kunisikiliza, wao ni kunikaba, kunivuta na kunisukuma, hadi leo nasikia uchungu na hasira sana jinsi nilivyodhalilika, ni miaka mingi sana imepita ila bado nina uchungu sana akilini
 
Wakati nikiwa mdogo niliwahi kushuhudia aliedaiwa kuwa mwizi akichomwa moto nadhan alikufa maana sikuweza kuendelea kuangalia.

Hukumu ya kifo tena kwa kuchomwa moto haiwezi kuendana na kosa ni kweli kuibiwa kuna umiza lakini adhabu ya kuchomwa moto hadi kufa siungi mkono hata msemeje.
Utajiridhisha vipi huyo anaepigwa ana hatia kweli? Wengine husingiziwa tu, pia adhabu ya kuiba inaendana iwe ni kumuua, tena kwa moto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwizi haki yake ni kuuwawa we unaetetea hujawahi kuibiwa, huku mtaani kwetu wezi wanatulaza macho mtu umetafuta mali kwa shida halafu yeye anakuja kuiba na pengiza anaweza kukujeruhi halafu unamtetea hujajuwa uchungu wa kuibiwa. Ndo maana jpm alisema majambazi wanyang'anywe silaha haraka haraka. Hadi mda huu naandika sijalala nasubiri kulala SAA 10 alfajiri halafu wewe unasema wasichomwe. We p.u.m.b.u kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ambae hajawahi kuibiwa hawezi jua uchungu wake , afu mwizi mwenyewe hanaga huruma ukiingia kumi na nane zake nawe umeumia sa huruma ya nn kwake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unanitukana kwa lipi hapo wakati hizo video ni original na sio za kutengeneza, jamii zilizostaarabika haziwwzi kumbananisha binadamu mwenzao katikati ya tairi na kumchoma moto akiwa hai na kumbanika kama mshikaki huku akilia kwa uchungu, halafu kuna linjemba linajifanya chief cook lunamshik mguu? Sawa kuiba ni kosa lakini hiyo adhabu ni kali mno jamani; hivi umeshawahi hata kujiunguza na sufuria walau hata kwa bahati mbaya mkuu? Yale maumivu sasa just imagine mtu uchomwe moto namna hiyo?! Pia kuna hatari ya kufanya mix-up na kumchoma mtu asie na hatia, na ndio maana kuna mahakama! Binafsi ningekuwa huyi askari ningehakikisha nasimamia haki, na haki ya huyo mtuhumiwa wa wizi ni kwenda kushtakiwa na kujibu mashtaka mahakamani!
Point nayoogopaga ni kumix ili kuhusu kusema adhabu ni kali hiyo hakuna kabisa hata yy hutupa adhabu kali anapotuchukulia vitu ulivyovihangaikia usiku na mchana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vingine vinatia hasira sana, serikali imekupa mafunzo ya kijeshi, ikakununulia na silaha nzito uitumie kulinda maisha ya watz, hata mwizi ni raia na ana haki ya kufika mahakamni kujibu mashtaka, nimejisikia hasira sana kuona huyu askari akishindwa kufyetua risasi hewani, na atakaemgusa sheria inamruhusu kumfumua ubongo!

==========================
Update: Possibly hapakuwa na mwizi kwenye pikipiki iliyochomwa kama heading ya video kwenye youtube inavyosema.

ushawahi kuibiwa na wakakupa na kipigo.waki kuibia utakuja kuongea haya
 
Sitetei wezi, ila adhabu ya kumchoma mtu moto ni kali sana na haikubaliki, kama mmeamua kumhukumu kifo extra-judicially kwa wizi basi mpigeni jiwe moja zito la kichwa afe papo hapo na sio kumtesa binadamu mwwnzeno kwa kiwango cha mateso makali namna hiyo, daah!
Lengo la adhabu ni kufanya watu waogope hicho kitu unafikiri kifo ni kitu cha ajabu sana kama ni kifo kila mtu atakufa acha afe kwa maumivu makali ili wengine wajifunze waone kufanya kazi ni bora kuliko kuiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom