Mtu kupigwa na kuchomwa moto mbele ya askari mwenye silaha nzito, nini maana yake? Tuna Jeshi dhaifu?

Mwizi haki yake ni kuuwawa we unaetetea hujawahi kuibiwa, huku mtaani kwetu wezi wanatulaza macho mtu umetafuta mali kwa shida halafu yeye anakuja kuiba na pengiza anaweza kukujeruhi halafu unamtetea hujajuwa uchungu wa kuibiwa. Ndo maana jpm alisema majambazi wanyang'anywe silaha haraka haraka. Hadi mda huu naandika sijalala nasubiri kulala SAA 10 alfajiri halafu wewe unasema wasichomwe. We p.u.m.b.u kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Dawa ya mwizi ni kiberiti
 
Hiyo video nimeiangalia kwa macho yangu, hivi askari unaruhusu raia akusogelee na kuishika silaha yako? Wewe ni askari kweli, tena wanakusukuma? Kisheria unaruhusiwa kufyatua risasi hewani, na kama bado watakusogelea kukuzonga unahaki ya kuwafumua ubongo wote!
Askari vikaza kama wewe hatuwahitaji kabisa kwenye jeshi letu,nyie ndo mnaharibu image ya jeshi la polisi...huyo askari anaakili sana,wakati mwingine busara ni muhimu kutumika kama alivyofanya huyo askari...ukiangalia hao raia hakuna aliyekuwa na lengo la kumdhuru askari na yeye alilijua hilo
 
Asalam Alaikum ndugu

Sitaongea sana lakini mwenye haki ya kutoa adhabu ya moto kwa binadamu ni Mwenyezi Mungu pekee na wala sio sisi binadamu. Kumchoma binadamu mwenzako haijahalalishwa katika kitabu chochote cha dini. Na kutii sheria ya nchi husika ni moja ya ibada.
 
Vitu vingine vinatia hasira sana, serikali imekupa mafunzo ya kijeshi, ikakununulia na silaha nzito uitumie kulinda maisha ya watz, hata mwizi ni raia na ana haki ya kufika mahakamni kujibu mashtaka, nimejisikia hasira sana kuona huyu askari akishindwa kufyetua risasi hewani, na atakaemgusa sheria inamruhusu kumfumua ubongo!

==========================
Update: Possibly hapakuwa na mwizi kwenye pikipiki iliyochomwa kama heading ya video kwenye youtube inavyosema.

Jee ulitaka kuwepo na double murder ili tuweze kuwalaumu polisi? Kwanza mambo haya hutokea wakati polisi hawapo na wanapopewa taarifa na kukuta hali hiyo unatarajia wafanye nini?
 
Hiyo video nimeiangalia kwa macho yangu, hivi askari unaruhusu raia akusogelee na kuishika silaha yako? Wewe ni askari kweli, tena wanakusukuma? Kisheria unaruhusiwa kufyatua risasi hewani, na kama bado watakusogelea kukuzonga unahaki ya kuwafumua ubongo wote!
Angekamua traiga nayo tena mngesema katumia nguvu nyingi!!! Kazi ipo sijui ni lipi jema kwenu
 
Hiyo video imeonyesha udhaifu wa hali ya juu, lets leave it at that.
kwahiyo ulitaka sisi tulokuwa pembeni tupigwe risasii kisa pikipiki inayochomwa? kwani pikipiki na uhai kipi kikubwaaa? hata ka kaonesha udhaifu vipi asingeweza za mdhuru mtu kisa pikipiki ilochomwa
 
Askari vikaza kama wewe hatuwahitaji kabisa kwenye jeshi letu,nyie ndo mnaharibu image ya jeshi la polisi...huyo askari anaakili sana,wakati mwingine busara ni muhimu kutumika kama alivyofanya huyo askari...ukiangalia hao raia hakuna aliyekuwa na lengo la kumdhuru askari na yeye alilijua hilo
Umeongea pumba gani? Nilichosema ni kwamba askari huyo amepewa dhamana ya kulinda raia na mali zao! Na ameshindwa kwa namna ya aibu na ya kufedhehesha, period!
 
Jee ulitaka kuwepo na double murder ili tuweze kuwalaumu polisi? Kwanza mambo haya hutokea wakati polisi hawapo na wanapopewa taarifa na kukuta hali hiyo unatarajia wafanye nini?
Wazuie kinachoendelea, na atakae kataa kutii amri halali ya askari na kuhatarisha usalama wa askari ashughulikiwe kwa mujibu wa kanuni za kiaskari, ikiwemo kupiga risasi hewani ili kutawanyisha wahalifu, kumbuka waliochoma moto hiyo pikipiki ni wahalifu!
 
kwahiyo ulitaka sisi tulokuwa pembeni tupigwe risasii kisa pikipiki inayochomwa? kwani pikipiki na uhai kipi kikubwaaa? hata ka kaonesha udhaifu vipi asingeweza za mdhuru mtu kisa pikipiki ilochomwa
Sasa unapomzonga zonga askari aliyekupa amri halali ya kukuzuia kuharibu mali kinyume na sheria kanuni zipo wazi, sasa kama hazijui basi sijui niseme nini tena..
 
Back
Top Bottom