Mtu kupigwa na kuchomwa moto mbele ya askari mwenye silaha nzito, nini maana yake? Tuna Jeshi dhaifu?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
23,366
2,000
Vitu vingine vinatia hasira sana, serikali imekupa mafunzo ya kijeshi, ikakununulia na silaha nzito uitumie kulinda maisha ya watz, hata mwizi ni raia na ana haki ya kufika mahakamni kujibu mashtaka, nimejisikia hasira sana kuona huyu askari akishindwa kufyetua risasi hewani, na atakaemgusa sheria inamruhusu kumfumua ubongo!


==========================
Update: Possibly hapakuwa na mwizi kwenye pikipiki iliyochomwa kama heading ya video kwenye youtube inavyosema.

==========================
Update:
Niwaambie tu ukweli sasa hivi, waTanzania wengi ni 'SADDISTS', yaani ni watu ambao tuna-enjoy kumuona binadamu mwingine akiwa katika maumivu makali. Huwa tunasingizia kwamba tuna hasira za kuibiwa lakini ukweli ni kwamba lile tukio la kumpiga mtuhumiwa wa mwizi na kumchoma moto ni namna moja wapo ya kujiburudisha, ni mshawasha kwetu na huwa tunashangilia kama tunavyoshangilia mechi ya mpira, hili ni tatizo la kisaikolojia. Kwa SADDIST kile kitendo cha kumuumiza na kumtesa binadamu mwsnzake huwa kinampa 'high' (ulevi) wa namna fulani na akikosa kwa muda mrefu huwa anapata 'AROSTO', na ndio maaa opportunity ya kumtesa binadamu mwenzake inapojileta (mtuhumiwa wa wizi) huwa anaitumia nafasi hiyo ipasavyo ili kusatify wicked cravings alizonazo, basi atajifanya anahasira sana na kumpiga na kumtesa na kumchoma moto yule mtuhumiwa bila kuhoji chochote, basi wakati yule mtu anavyoteseke na kuumia yeye ndio anapata burudiko la hali ya juu moyoni mwake..., angali jinsi warumi (Romans) walivyokuwa wanaugua huu ugonjwa, walichukua mateka wa kivita na wafungwa kisha kuwatupa ulingoni (colloseum) na kuwapambanisha na wanyama wakali kama simba na chui, na wao walikaa majukwaani na kushangilia kama mechi ya mpira, waliienjoy sana kuona binadamu anateseka na kuumia, someni zaidi kuhusu huu ugonjwa wa 'SADDISM'.
 

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
23,366
2,000
sijui mnaonaga raha gani kupotosha
Hiyo video nimeiangalia kwa macho yangu, hivi askari unaruhusu raia akusogelee na kuishika silaha yako? Wewe ni askari kweli, tena wanakusukuma? Kisheria unaruhusiwa kufyatua risasi hewani, na kama bado watakusogelea kukuzonga unahaki ya kuwafumua ubongo wote!
 

Wanu

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
352
250
Mwizi haki yake ni kuuwawa we unaetetea hujawahi kuibiwa, huku mtaani kwetu wezi wanatulaza macho mtu umetafuta mali kwa shida halafu yeye anakuja kuiba na pengiza anaweza kukujeruhi halafu unamtetea hujajuwa uchungu wa kuibiwa. Ndo maana jpm alisema majambazi wanyang'anywe silaha haraka haraka. Hadi mda huu naandika sijalala nasubiri kulala SAA 10 alfajiri halafu wewe unasema wasichomwe. We p.u.m.b.u kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom