Mtu kujitokeza na kusema taarifa walikuwa nazo hata kabla ubalozi wa marekani haujasema!!!!

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,199
1,346
Kwa kweli nashindwa kuelewa intension ya viongozi wetu kwa watanzania ni nini hasa?.

Watu wanatoa security alert mwingine anajitokeza hadharani na kuongea simple simple tu.

Mh magufuli baba yetu tunakusubiria useme neno kuhusu ijipi sirro na makonda.

Kauli zao huku mitaani zinaonekana ni za dharau sana na kisiasa sana.

Mtu anasema taarifa walikuwa nazo, mbona hawakuzitolea tahadhari?

Au walikuwa wanasubiria majanga yatokee ndio waseme?

Umuhimu wa taarifa kama hizo ni kutoa tahadhari kwa jamii.
 
IMG-20190619-WA0011.jpeg
IMG-20190619-WA0009.jpeg
 
Sawa hawa wangese kama walikua na taarifa wangetoa. Ni tahadhari tu kuliko kuacha hadi yatokee mje hapo na makamera yenu muanze kuongea ungese
 
Tusidharau sana kazi ya vyombo vya usalama. Kuna madhara sana kumwonyesha mhalifu kuwa unajua mbinu zake. Kuepusha unnecessary public panic bora Kufanya countermeasures kimya kimya ili wahalifu wasijue move inayofuata. So kwa mtazamo wangu, am okay na hiyo statement.
 
hizo taarifa mnazotaka zitolewe na polisi kwa kadri wanavyozipata mjue kabisa madhara ya taharuki inayoweza kuwakumba raia baada ya kupewa hizo taarifa yanaweza kuwa makubwa kuliko hata madhara ya shambulio lenyewe.. pia mjue matishio ya mashambulizi polisi au usalama wanayapata karibu kila siku na wanajua namna ya ku deal nayo huko huko kimya kimya bila kuleta taharuki zisizo za lazima kwa raia
 
Wakati mwingine ni vizuri kuwajuza wahalifu ili watambue kuwa wanafahamika! Tatizo lenyu wadanganyika mmezoea ushirikina na vitendo vya gizani kama wachawi.

Kuna mmoja hapa alikuja na mbwembwe zake uchwara za TISS kwamba ni wajuzi wa kuficha siri! Hakufahamu kuwa chombo cha intelligence kina wajibu pia wa kutafuta taarifa na kuzisambaza! (Whether genuine or propagandas).
 
Kipi bora? Vyombo vya usalama kutangazia watu uwezekano wa ugaidi kutokea ili watoe habari kwa vyombo husika wanapowaona watu wanaowashuku ni waovu, au ni kwa vyombo vya usalama kuficha hizo habari wakifikiri hao waovu hawatajua wameshajulikana? Swali kubwa zaidi nalojiuliza ni kwamba imetokeaje ubalozi wa Marekani (ambao una wafanyakazi wachache tu) ukaweza kugundua uwezekano wa huo mpango ovu kabla ya vyombo vyetu vya usalama (ambavyo vina wataalamu wengi) kugundua? Naamini yanatakiwa marekebisho ya haraka sana katika utendaji kazi wa vyombo vyetu vya usalama (hasa polisi). Siku hizi hapa Tz watu wengi sana wanapoona jambo ovu limetokea au linapangwa kufanyika, wanajiweka pembeni. Wanasema wazi ukiripoti polisi unaweza kuja kusumbuliwa kwenda kutoa ushahidi mahakamani, au pengine hao watu waovu wanaweza kushirikiana na polisi "kumgeuzia kibao" aliyetoa ripoti.
 
hizo taarifa mnazotaka zitolewe na polisi kwa kadri wanavyozipata mjue kabisa madhara ya taharuki inayoweza kuwakumba raia baada ya kupewa hizo taarifa yanaweza kuwa makubwa kuliko hata madhara ya shambulio lenyewe.. pia mjue matishio ya mashambulizi polisi au usalama wanayapata karibu kila siku na wanajua namna ya ku deal nayo huko huko kimya kimya bila kuleta taharuki zisizo za lazima kwa raia
Mbona huwa wanatoa taarifa za kiinteligensia kutahadhalisha na kukataza mikutano ya chadema tu. Na hakuna taharuki
 
Kwa kweli nashindwa kuelewa intension ya viongozi wetu kwa watanzania ni nini hasa?.

Watu wanatoa security alert mwingine anajitokeza hadharani na kuongea simple simple tu.

Mh magufuli baba yetu tunakusubiria useme neno kuhusu ijipi sirro na makonda.

Kauli zao huku mitaani zinaonekana ni za dharau sana na kisiasa sana.

Mtu anasema taarifa walikuwa nazo, mbona hawakuzitolea tahadhari?

Au walikuwa wanasubiria majanga yatokee ndio waseme?

Umuhimu wa taarifa kama hizo ni kutoa tahadhari kwa jamii.
Tanzania ni salama kabisa
 
Back
Top Bottom