Mtu "huyu" anaweza kuwa "kete" nzuri sana kwa Wapinzani, inahitaji nguvu kidooogo!!

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Mtu huyu anaweza kuwa kete nzuri sana kwa wapinzani. Sababu zifuatazo

1. Uchumi kashauvuruga na hakuna dalili za kuukarabati, kila mtanzania analia,hapewi jibu la kitaalamu,bali anaambiwa yeye ni mpiga dili. Wapinzani wahakikishe "wanakaza" na kuifafanua hata pointi ndogo kabisa tena kwa lugha ya kawaida

2.Sekta ya Umma;
Sio siri,tangu Uhuru,watumishi hawa hawajawahi kunyanyasika kama kipindi hiki,na dalili zinaonyesha wataendelea kufanyiwa hivyo,wanashambuliwa hadharani bila kufata taratibu,haki zao zinaminywa na wanafukuzwa kama vibarua wa muhindi, ni vyema hawa nao wakasemewa vizuri na ikibidi idara za tafiti za vyama ziunde kitengo maalum cha kukusanya na kuchambua matatizo yao kikanda na kitaifa,kisha kuyasemea kwa kina na mapana.Ni wazi watu hawa kwa kuwa ni wasomi,ni vigumu sana kusahau madhila yaliyowakumba.

3.Wanafunzi

Hawa nao hawajanusurika na dhahama za awamu hii,hasa wa elimu ya juu,wamekosa mikopo,na wanaopata wanaipata kwa manyanyaso.Idara za vijana zijiimarishe kuwasemea na kusemea watu walio katika elimu ya juu.Tafiti zifanyike za kina ili kujua undani wa matatizo yao,undani wa mambo ya bodi ya mikopo na kisha kupaza sauti kubwa,uundwe umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu wenye wasemaji wazuri ambao wataangazia mambo haya na kuyasema kwa uwazi,umoja huo ujikite ndani ya vyuo na hata nje kwa ajili ya ushawishi.

4.Suala la njaa.

Hili nalo lisemewe katika kanda zote,sio makao makuu pekee,sauti zipazwe kutoka kanda zote,waathirika wa njaa watembelewe na viongozi wa kanda na ikibidi mifano halisi itolewe huko huko mashambani. Hii italenga kura na wananchi wa vijijini,na pia watafahamishwa kwamba Bajeti ya pembejeo imeshushwa mpaka bilioni 10 kutoka bilioni 78,ujumbe huu uwafikie wananchi hasa wa vijijini wanaotegemea kilimo,na pia waambiwe ghala la taifa pia halina chakula cha kutosha na Bajeti waliyopewa ielezwe,ziundwe idara za tafiti kuhusu kilimo na maji na afya zikilenga haswa kushughulika na kura na wananchi wa vijijini,ziwe na takwimu za kutosha kwa ajili ya hotuba,takwimu hizo zigawanyike kikanda,kwenye kahawa ,takwimu zake ziwepo,pamba,takwimu ziwepo.....na ziwe katika lugha rahisi.

5. Wafanyabiashara:

Hawa ni wahanga wa hii awamu,ufanywe utafiti mkubwa kuhusu kero zao,ufanyiwe uchambuzi,na waelezwe kinaga ubaga kwa njia rahisi kuhusu shida wanazopata na nini chanzo,hii ianzie kwa wamachinga mpaka wale wakubwa na waelezwe kwamba suluhu ipo, kikosi kazi kizikusanye kero zao,kizichambue kitaalamu kwa lugha rahisi tayari kwa kutumika field.

6.Tabia binafsi na haiba ya mtu huyu.

Hii nayo unaweza kufanyiwa tafiti kwa kukusanya kauli za mtu huyu,kuita kikosi cha wanasaikolojia wakazichambua kitaalamu,na kisha,kila baada ya muda jamii inapewa tafsiri ya kitaalamu ya mtu huyu na wahusika.

6:Ufuatiliaji wa matukio kila siku.

Kila siku anapozungumza,lazima atazua tafrani,basi wawepo wa kuchukua kauli zake za kila siku na kuzipa mapana yake na athari zake kijamii

Mengine mtaongezea kadri mnavyoona jinsi gani mtu huyu anaweza kuwa kete nzuri

UPDATE.

Matunda ya utafiti wa mzee makongoro Mahanga umelibomoa Baraza la mawaziri baada ya dk possi kuondolewa. Utafiti wa kikatiba,vyama vya upinzani viwekeze kwenye tafiti za kiuchumi,kijamii na kisiasa,pia na sheria

Hata tena: Dodoma wanavurugana ......
 
Jussa,Mazrui,na "babu" pamoja na maalim wajikite kwenye tafiti za muungano na mambo ya Zanzibar,na wajipe muda kila Mara kuyasemea
 
Pia zitafutwe au zitengenezwe kada za "mavoluntia" wanachuo wa kada mbalimbali watakaokuwa wanajitolea kipindi cha likizo kufanya kazi katika ofisi za vyama,hii itaandaa viongozi wajao na pia itasaidia katika tafiti kwa kadri kila kanda ilivyojipangia maeneo ya kutafiti
 
Kuitoa CCM ni kazi rahisi sana kama atapatikana mtu sahihi 2020 kupambana na Mh Magu..

Kama upinzani utarudia yale yale ya 2015 kwa kumsimamisha mgombea yule basi binafsi sitopiga kura...
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza.

Hata kujipa matumaini hewa wakati unafahamu uko mbioni kufa pia ni vizuri na haki yako.
 
Back
Top Bottom