Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 4,462
- 8,079
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.
Ndugu wana JF wenzangu na watanzania wenzangu, ili chama cha CCM kiweze kushindwa katika uchaguzi mkuu wa 2025 au 2030, yanahitajika mambo matatu.
1) Kwanza: kinahitajika chama imara cha upinzani chenye sera nzuri, zinazoeleweka na kutekelezeka. Chama hicho kiwe na sura ya kitaifa, kiwe na viongozi wakweli, wenye maono na misimamo thabiti ya kuikomboa nchi. Kiwe na mifano hai ya utekelezaji wa sera zake kupitia chama husika ili kiweze kuaminika machoni mwa watanzania wengi.
2) Pili: Anahitajika kuchaguliwa mgombea ambae hana makandokando ya uongo, uoga, unafiki na mwenye uwezo wa kweli wa kusimamia sera za chama chake bila kuyumbishwa na mtu yoyote iwe ndani ya chama au nje ya chama.
3) Tatu: Tume huru isiyoegemea upande wowote wa kisiasa. Tume iwe na viongozi kutoka vyama mbali mbali vya kisiasa na kiraia ili kujenga sura ya utaifa katika tume hiyo.
Ni hayo tu ninayoyaona mimi, katika kuijenga Tanzania bora zaidi ya kesho.
Asanteni sana.

a) Sio mtu useme chama chetu kina misingi ya demokrasia wakati mwenyekiti wa chama ambacho kingekuwa mfano wa demokrasia hiyo ana miaka 20 madarakani.
b) Sio mtu useme chama chetu ni cha maendeleo, wakati wanaoendelea katika chama ni mwenyekiti wa chama taifa na genge lake, huku chama chenyewe kikiwa hakina hata ofisi ya kufanyika mkutano wa ndani.
c) Sio mtu useme chama chetu kitasimamia utawala bora na haki, huku ndani ya chama chenyewe hakuna anaeweza kuongelea lolote mbele ya mwenyekiti wa chama au makamu wake.
2) Pili: Anahitajika kuchaguliwa mgombea ambae hana makandokando ya uongo, uoga, unafiki na mwenye uwezo wa kweli wa kusimamia sera za chama chake bila kuyumbishwa na mtu yoyote iwe ndani ya chama au nje ya chama.
a) Sio kiongozi anakuwa na kauli za kilaghailaghai kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa, na kiuongozi (kama tunavyoona hapo chini pichani) bila kujali madhara yatokanayo na ulaghai huo. Mtu wa aina hii ni ngumu kuchaguliwa maana watanzania wa sasa sio wale wa 2001, kule Zanzibar ambapo watu walikufa, kujeruhiwa na kufungwa, huku muhusika aliepiganiwa (aliekuwa katibu mkuu wa chama, na mgombea wa upinzani) akiwa Saudia Arabia kula tende na maswaiba zake. Mgombea akiwa hana msimamo thabiti wa kusimamia sera au hoja zake mwenye, basi hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Marekani ikija kusimamia uchaguzi bado ataangukia pua tu.