Mtu gani uliwahi kukutana naye mara moja tu hujakutana naye tena mpaka leo unatamani umuone kwa mara nyingine

Mapico

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
556
1,270
Habari zenu.

Nianze na kuwapa pole na mihangaiko ya hapa na pale pamoja na tuchukue hadhari na Coronale kwa kuzingatia kanuni za Afya.

Leo nimemkumbuka sana rafiki yangu aliedumu kwa masaa 2 tu mwaka 2014 .Ila mpaka leo sijamuona tena, nilikuwa nasafiri ya kwenda Bagamoyo shamba via Mlandizi Road; sasa kuna Costa na Noah za kwenda huko uzuri, nilipanda Costa.

Nikakaa siti zile za nyuma kabisa za tuta mali yako, mabonde changamoto. Nafika kukaa tu pembeni yangu, nikamkuta huyu mdada mzuri na mcheshi tukasalimiana baada ya muda tukazoeana kama tunajuana miaka mingi.

Baada ya story nyingi tukafika Bagamoyo tukaagana bila kuachiana contact. Nilikuwa nawahi shamba kwenye mananasi maana mzigo ulikuwa unahitajika sokoni haraka.

Basi nikampotezea hapo mpaka leo sijamuona tena. Jina lake anaitwa Bernadetha Lutengi alipokuwa anaishi ni maeneo ya Nia Njema Secondary Bagamoyo. Sijui huko wapi.

Unaweza ku-share mtu ambaye ulikutana naye mara moja unatamani ukutane naye tena.
 
sijawahi labda huyo "Coronale"
Capturey.JPG
 
Kuna mwanafunz mwenzangu tulikutana ndan ya bus ilikuwa n likizo (December 2017) wakati huo nikiwa kidato Cha 5, yeye pia akiwa kidato Cha 5, safari hiyo ilikuwa n Dar to Songea wote tulikuwa seat karibu tulipiga story tulizoeana mno kwa mda huo mfupi Ila tuliachan njombe yey akashuka pale me nkaendelea na safar mbaya zaidi hatukupean mawasiliano, kwahyo tangu hapo had sasa hivi sijakutana nae Tena Ila namkumbuka na natamani mno tukutane Tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom