Mtu anayetumia mashoto au malia kitaamu nini kinasababisha!!!

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Habari members,

Nina kijana wangu mdogo wa miezi 10, hivi karibuni nimegundua ni mashoto, hasa ninapojaribu kumpa kitu huwa anatanguliza mkono wake wa kushoto, nimemchunguza zaidi nimegundua hata mguu wake wenye nguvu zaidi ni wa kushoto. Mimi mwenyewe na mama yake wote ni malia, lakini Bibi yake ni mashoto. kwahiyo nikajua tu amerithi kutoka kwa Bibi yake.

Sasa wataalam ukiacha hili suala la kwamba linatokana na urithi. Kitaalam ni nini kinatokea katika mwili wa mtu tangu anazaliwa mpaka kinachomfanya awe mashoto au malia?. Au labda kuna tofauti yoyote ya kitaalam ndani ya mwili wa mtu anayetumia mashoto na yule anayetumia malia.
 
Bayo

Senior Member
Jul 2, 2009
195
34
aisee m mwenyewe nna mashoto... Hv huwa n nn kinasababisha kweli... Mwenye mautundu atutupie hapa
 
mbweta

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
600
77
wakati yupo tumbon alilalia mkono au upande wa kulia na kufanya mashoto huwe free na kuwa na nguvu.
 
Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,770
10,513
Binafsi nimezaliwa natumia mkono wa kulia..kutokana na matatizo yaliyonipata miaka miwili iliyopita ilinilazimu kujifunza kutumia mkono wa kushoto hasa katika kuandikia.ilinichukua takribani miezi 6 kufanikiwa kuandikia kushoto bila matatizo.sasa naweza kutumia mkono wowote katika kuandika...kukusaidia swali lako nakushauri uendea tovuti ya wikipedia usearch "left handedness" pia kwa ufahamu wa ziada "ambidextrous" ni kwa watu wawezao kutumia mikono yote miwili.igoogle utapata mengi usiyoyajua
 
Daffi Jr

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
3,830
905
Kitaalam watu wanaotumia mikono ya kushoto na kulalia upande huo inasemekana wana akili sana!!!!ngoja nicheck zile data vizuri
 
Puppy

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,966
2,396
Kama ni natural born Left handed ujue umezaa Genious.. Mpe nafasi ya kuwa independent wakati unamkuza, mwache achague mwenyewe lolote lile, halafu we ndio umrekebishe kama kachagua baya na uwe tayari kumpa maelezo maana wanadadisi kweli... After his/her early teens utagundua nilichokuambia kuwa ni genious..

Watu wengi maarufu duniani (maarufu kwa changes walizoleta), more than 75% ni left handeds.. Eg. Obama na wengine wengi.

Honger Kwa Kuzaa Genious
 
Edson

JF-Expert Member
Mar 7, 2009
9,709
4,512
nimezalliwa nikiwa natumia mkono wa kushono katika mambo yote..baada ya kuanza shule baba yangu akawa hataka kabisa nitumei mkono huo maana alikuwa anachukia hasa wakati wa kula mimi nilkuwa natumia mkono huo na yeye alikuwa anakasirika na kunipiga....nilipoanza darasa la kwanza(sikupita chekechea mimi) mzee wangu alikuja shelni na kumwambia mwalimu wangu kuwa nitumia mkono wa kulia kuandika na ahakikishe natume mkon wa kulia...nilipigwa sana na yule mwalini maana nilikuwa siwezi kabisa....kutoka na kichapo kile nilijitahidi kujifunza na hatimae kufanikiwa kutumia mkono wa kulia japo nikiandika kwa mkono huu wa kulia mwandiko wake huwa mbaya sana...lakini nikiandika kwa kutumia kushoto yangu mwandiko wangu ni mzuri sana....sasa hivi naandika kwa kutumia miko yote...ila mpira na vitu vingine natumia kushoto.......

pamoja na kusoma kote huku sijui hii mashoto na malia inakuwaje.....
 
DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Kama ni natural born Left handed ujue umezaa Genious.. Mpe nafasi ya kuwa independent wakati unamkuza, mwache achague mwenyewe lolote lile, halafu we ndio umrekebishe kama kachagua baya na uwe tayari kumpa maelezo maana wanadadisi kweli... After his/her early teens utagundua nilichokuambia kuwa ni genious..

Watu wengi maarufu duniani (maarufu kwa changes walizoleta), more than 75% ni left handeds.. Eg. Obama na wengine wengi.

Honger Kwa Kuzaa Genious

Nashukuru sana kwa hizo baraka. Labda watutaambia humu ukweli wa hilo swala.
 
Don Mangi

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,198
831
ubongo umegawanyika katika hemispheres mbili, left side na right side, watu wanaotumia upande wa kulia control huwa inatoka left side of the brain, sasa ukija kwa left handers control inatoka right side of the brain. Ambayo watu left handers ni special cases mostly ether by inheritance au genetical make up kama ilivyo swala la mapacha...
What to note is that wazazi wengi huwa wanawadescourage watoto wao wanapojua ni mashoto THIS IS NOT RIGHT inakuja kumsababishia matatizo mengi sana ikiwemo tatizo la kumbukumbu na ugumu wa vitu kama mahesabu...So cha kufanya ni kumuacha na kumtafutia vifaa ambavyo vina encourage left handedness mfano mlango wa chumba chake uwekwe tofauti na mingine, na baadhi ya vifaa kama mikasi iliyotengenezwa maalum kwa left hand people...watu wengi wa namna hiyo huwa wana uwezo mkubwa ,sana katika sayansi, mahesabu kama hawatakuwa discouraged na pia wana uwezo mkubwa sana kimichezo na hasa kama ni wasichana wanakuwa na extraordinary capacity of learning
Kwa maelezo zaidi unaweza kunicheki au uliza swali ambalo unahisi unahitaji msaada
 
Don Mangi

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,198
831
Pia nimesahau kukushauri ukampime maendeleo ya Child motor development, madaktari wa watoto wanaifahamu hii ili waweze ku approve kama ni left hander coz wengine hukuta siyo left hander lakini upande wa kulia una slow coodination system...madaktari wa watoto wanajua kuipima hii vizuri sana
 
Nashukuru sana kaka. umetupa mwanga angalau. sasa kuna mambo mengine kama wakati wa kula, au kusalimiana. ukimwacha kabisa si anaweza akajikuta anatumia mashoto, na hili tunajua watu wengi hawapendi.

Pili mashuleni huwa wanapata tabu sana wanapokuwa wanaandika darasani, hasa ukizingatia wengi wanatumia kulia. sababu wakati wanaandika darasani au wakati wa mitihani huwa wanapinda upande wa kulia na wale wanaoandikia kulia wanapinda kushoto. sasa hii huwa inawaleteaga tabu, wakati mwingine wanadhaniwa kama wanadesa. au kuhisi kwamba anamsumbua jirani yake anayetumia malia.
 
Don Mangi

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,198
831
Nafkiri hili jambo ni kuwafanya watu wawe aware tu, mfano akianza shule uwe karibu na walimu wake uwaelezee hilo jambo na uwasisitizie ilivyo mbaya wakim discourage kuutumia huo mkono wake coz nina real example za watu waliozuiliwa kutumia kushoto na walipata tabu sana sasa hivi wakitaka kushika kitu kama mouse ya comp wanahangaika kweli, I would not love it to happen to your child too. Cha muhimu ni akiwa mkubwa unamuelezea vitu muhimu kama kusalimia na kula ajitahidi lakini sio kwa kumlazimisha kwa nguvu kufanya hivyo
 
DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Pia nimesahau kukushauri ukampime maendeleo ya Child motor development, madaktari wa watoto wanaifahamu hii ili waweze ku approve kama ni left hander coz wengine hukuta siyo left hander lakini upande wa kulia una slow coodination system...madaktari wa watoto wanajua kuipima hii vizuri sana

Nahukuru sana kaka kwa ushauri. nitafanya hivyo.
 
Giroy

Member
Dec 17, 2008
82
7
Kama ni natural born Left handed ujue umezaa Genious.. Mpe nafasi ya kuwa independent wakati unamkuza, mwache achague mwenyewe lolote lile, halafu we ndio umrekebishe kama kachagua baya na uwe tayari kumpa maelezo maana wanadadisi kweli... After his/her early teens utagundua nilichokuambia kuwa ni genious..

Watu wengi maarufu duniani (maarufu kwa changes walizoleta), more than 75% ni left handeds.. Eg. Obama na wengine wengi.

Honger Kwa Kuzaa Genious

nina watoto wawili wa kiume wote wanatumia kushoto miguu na mikono ha ha kumbe nina jamaa wa nguvu.nawaombea wawe na mafanikio.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom