Mtu anayejenga gorofa bila kusimamisha nguzo za zege (columns), ni imara kweli?

AMADOGO

Senior Member
Jul 1, 2015
108
78
Samahanini wadau naomba kujua hivi kujenga gorofa bila kusimamisha nguzo za zege zile. Uimara wake ukoje?

Engineer anadai kwa aina ya udongo ukiwa na matofali imara yakajengwa kwa kulaza inatosha.

Ni kweli inaweza kuwa imara? Eneo ni tambarare.

Naombeni mawazo yenu
 
Ni muhimu kuwa na columns lakini haina maana huwezi jenga jengo bila nguzo.

Usipoweka nguzo maana yake uzito wa nyumba utabebwa na matofali, hivyo unapaswa uwe na ukuta imara kweli kweli wenye unene sahihi.
 
1. Huyo injinia umejiridhisha ni injinia kweli?

Maana siku hizi hata darasa la saba au watu wenye diploma za ujenzi wanajiita mainjinia. Kujirisha mwambie akupe muhuri wake wa ERB kama asipokupa mwambie cheti na uhakikishe kiwe cha degree ya civil engineering.

2. Je hilo jengo ghorofa ngapi?

3. Je kuna structural analysis yeyote aliyo fanya ili kuthibitisha anachosema? Kama anayo amekupa? Je kama amekupa ina muhuri wa mhandisi aliye sajiliwa na bodi ya wahandisi Tanzania?

4. Je huyo injinia wako alikushauri ufanye soil analysis ili kujua nature ya udongo kabla hajaja na hilo jibu alilo kupa?

Naomba nijibu maswali yote ili tuendelee.
 
Yaweza kua umemwambia apunguze gharama na yeye ameona kutoweka nguzo ni option ya kupunguza gharama
Hii option ingekua na maana kama huyo injinia wake angefanya haya.

1. Kwanza aje na gharama za option zote yaani ujenzi wa colums na ujenzi wa bila columns. Kisha aseme kama kuna tofautinua bei je ni significant? Maana usije kuta una sevu buku nane kisha unasema unakwepa gharama!

2. Pili aje na detailed technical analysis ya hizo option mbili na atuambie kwamba ndio tuna sevu gharama lakini je usalama wa watu watakao tumia hilo jengo kwa miaka 50+ ijayo upoje?

Maana usije kuta tuna sevu gharama alafu tuna hatarisha uhai wa watu!
 
Hii option ingekua na maana kama huyo injinia wake angefanya haya..

1. Kwanza aje na gharama za option zote yaani ujenzi wa colums na ujenzi wa bila columns. Kisha aseme kama kuna tofautinua bei je ni significant? Maana usije kuta una sevu buku nane kisha unasema unakwepa gharama!

2. Pili aje na detailed technical analysis ya hizo option mbili na atuambie kwamba ndio tuna sevu gharama lakini je usalama wa watu watakao tumia hilo jengo kwa miaka 50+ ijayo upoje?

Maana usije kuta tuna sevu gharama alafu tuna hatarisha uhai wa watu!
Ulichoandika ni logic naamini wote engineer na mleta uzi wataconsider
 
Wahandisi tupeni miongozo

Mimi naona inawezekana hili Jengo lilijengwa na Wajerumani mwaka 1916 mpaka leo lipo.

Iringa Boma.

20211206_190544.jpg
 
Wahandisi tupeni miongozo

Mimi naona inawezekana hili Jengo lilijengwa na Wajerumani mwaka 1916 mpaka leo lipo.

Iringa Boma.

View attachment 2035113
Kwa sababu hilo jengo limejengwa iringa haimaanishi jengo linaweza jengwa sehem yeyote hapa duniani.

Kinacho detarmine sustainability ya jengo sio "limesha wahi kujengwa iringa" bali ni nature ya udongo pamoja structural design iliyo fanywa na injinia (namaanisha injinia sio fundi wa mtaani).
 
Wanasema akina nani?

Na wame tumia kigezo gani kusema haisumbui sana?
Sijatumia formula ya darasani,ila kwa uzoefu gorofa moja itashikiliwa na kuta imara za chini; utakapoenda gorofa ya pili, itategemea muendelezo wa gorofa ya kwanza kutokea kwenye msingi, ambapo kiunganishi ni nguzo kutoka chini
 
Back
Top Bottom