Mtu anayedhaniwa kuwa na virusi vya Corona apatikana katika Uwanja wa Jomo Kenyatta, Kenya

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Taarifa zinaeleza kuwa mtu mmoja anayeshukiwa kuwa na virusi vya Corona nchini Kenya amepelekwa hospitalini.

Mshukiwa huyo amefikishwa hospitali kuu ya rufaa ya Kenyatta. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa mtu huyo aliwekwa karantini alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Hapo Jana Kenya iliitahadharisha raia wake kwenda mji wa Wuhan China, mpaka pale mlipuko wa virusi hivyo utakapodhibitiwa.

Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ilisema ilikuwa na mawasiliano na raia wake waliokwama katika mji wa Wuhan, mji ambao ni kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo, ambao uko kwenye uangalizi maalum.

''Ubalozi unafahamu kuwa kuna raia wa Kenya 85 mjini Wuhan ambao wamesajiliwa ubalozini hivyo unafuatilia kwa karibu hali hiyo,'' wizara ilieleza kwenye taarifa yake hapo jana.

Kwenye mtandao wa Twitter , wakitoa ujumbe wao wa #KenyansInWuhan, wakenya waliokwama mjini Wuhan walitoa wito kwa serikali yao iwaondoe kwenye mji huo.

''Ni masikitiko tu kwa nchi yetu. Wiki ya pili sasa kwenye mji huu na hakuna lolote linalofanyika,'' aliandika kwenye ukurasa wa Twitter Cornelius Mulili.

''Hali hapa ni mbaya. Ilichofanya serikali yetu ni kutia taarifa kwa vyombo vya habari pekee. Sitaki kueleza tunachokipitia hapa kimwili na kiakili,'' alieleza Rono Kipkorir.

Tahadhari ya kusafiri imekuja siku chache baada ya maafisa nchini Ivory Coast kubaini mgonjwa aliyekuwa na dalili zinazofanan na mtu mwenye virusi vya corona. Haijathibitishwa kama mgonjwa huyo ana virusi hivyo.

Kenya ina moja kati ya viwanja vilivyo na pilikapilika nyingi barani Afrika na imeongeza umakini katika uangalizi wake. Inawapima abiria wote kutoka China.
 


Coronavirus: Scare as Kenyan student admitted at Kenyatta hospital for coronavirus
 
Hapo JKNIA hali ikoje, wachina wanapimwa kweli?? Mana leo nlipanda mwendokasi asubuhi,ile hali nliyoiona mule nikaiwaza corona nikasikitika tu
 


Omamo issues alert to Kenyans to avoid non-essential travel to China
following coronavirus outbreak
 
katika movies anazotoa mzungu hasa za maafa huwa 100% ni reality na huwa ni kama message kwa binadamu,kwa maana kilishatokea au kinaandakiwa kutokea.
kwa atakae fatilia hii movie au anaeijua hii series movie ya the last ship atakjwa amenielewa nini kinaendelea china na kisipodhibitiwa mapema ni nini kitafata
14508780183_1f996a095e_b.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom