Mtu anaweza kununua views, comments, likes na subscribers. Zijue sababu na vikwazo

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,014
Nimekuwa nikishangaa sana kiasi kufikia mpaka kuona aibu kwamba naishi na jamii ambayo ipo nyuma sana kwenye maswala ya teknolojia. Haya mambo ya kununua youtube views katika ulmwengu huu yapo tangu zaidi ya miaka 10 lakini inatia aibu kwamba hata baadhi ya wasomi wameuwa wabishi,

Watu kununu aviews sio jambo la ajabu kabisa hasa katika kipindi hiki cha ulimwengu uliopiga hatua ya kushangaza katika nyanja ya teknolojia ya internet.

NJIA MAARUFU ZA KUNUNUA VIEWS HIZI HAPA

1. VIEWS WA KWELI AMBAPO MWANADAMU ANAUSIKA MOJA KWA MOJA KUTAZAMA VIDEO.


Kuna mitandao inayounganisha watu kufanyiwa kitu fulani na watu wanaoweza kufanya kituhicho kwa malipo ya pesa, sasa katika hii mitandao huwa kuna wadau wanataka video zao za yotube zitazamwe na watu wenye shida ya pesa, sio kutazama tu bali hata kulike, ku comment na ku subscribe. Mfano wa mitandao ninaojua kuna unaoitwa microworkers ambao ni mtandao pendwa kwasababu ya gharama zake za chini sana, Mtu anaweza kutoa nafasi za kazi kwa watu hata laki 1 ambao anahitaji watazame video yake kwa malipo ya kiasi atachokipangilia. Kwa lugha nyepesi ni kama vile unatembea barabarani umebeba begi lina sarafu za shilingi 100 nyingi, ukikutana na mtu barabarani unamwambia acheki video yako umpe hio 100,

Uzuri wa hizi views ni kwamba youtube wanajua kabisa hizi ni views orijino, huwa hawazichuji, Mfano ni huu hapa katika mtandao niliotaja, Mtu anatoa kiasi cha dola 0.1 sawa na shilingi 200 hivi endapo utatazama video yake, ku like, ku comment na kushea, ukisoma maelezo ya ziada kuna namna ya kumtumia ushahidi (hakuna pesa ya bure)

1621770665262.png




2. VIEWS WA MAROBOTI ( SOFTWARE & SHAMBA LA SIMU & SMM PANELLS)

Sifa ya hizi views ni wana bei chee, unaweza kununua hata views elf 1 kwa shilingi elf 2 tu, Ila hatari ya hawa views ni kwamba kuna mifumo ya youtube imewekwa ili kutambua hizi views na kuzichuja, Na hatari nyingine ni kwamba hawa views wanaweza kuifanya video yako isitokee kwenye matokeo ya mwanzo hata ikiwa na views wengi, hapausishangae kukuta video ambayo ina views 200 ipo kwenye matokeo ya juu huku video yenye views elf 20 walionunuliwa haipo hata kwenye amatokeo 10 ya mwanzo, Ila ndo hivyo tena watu nao wamekuwa wajanja zaidi kukwepa panga la youtube, huku ni 50/50 views wanaweza kutambulika ni wa kweli ama wakatambulika ni wa maroboti na kuhatarisha usalama wa video yako kushuka chini zaidi na kama ulikuwa unalipwa na youtube wanaweza kusitisha kabisa malipo wakijua unatumia views hizi za kijanja.

Software -

Kuna software kama Diabolic traffic, hii wanakupa kabisa na proxies (IT watanielwa) hapa utaweza kutengeneza views feki, hii software inauzwa kwa kulipia huduma ya kila mwezi takribani laki 3, kuna nyingine zipo kama hii hii unapata hata kwagharama ndogo, Nimeweka hii kwasababu nliwahi kuuona utendaji kazi wake kwa macho yangu, Kikwazo hapa ni kwamba ukienda mbali sana basi ni views milioni 1 tu.

1621771600320.png

SHAMBA LA SIMU

Hapa mtu anakuwa na simu nyingi sana anaanza kuzipa maelekezo ya kutazama views, mfano mdogo ni huu, kuna mashamba ya views kunasimu nyingi zaidi

1621770915147.png 1621770993757.png

SMM PANELS


Hawa wanatoa huduma nying zaidi kwa bei chee, huku utanunua hata views, likes, followers wa instagram na facebook, Pia utanunua hata views, comments, likes, subscribes za youtube, n.k

Mfano ni huu mtandao >> HUU << ,

unanunua views elf 1 kwa takribani shilingi elf 3 na unachagua kabisa ziingie kwa spidi yani ndani ya saa moja, ziingie kwa siku nzima taratibu, ziingie kwa kunyunyizia , n.k

1621774530418.png




KWASABABU GANI WATU HUNUNUA VIEWS

1.Kuonekana ni maarufu

kwa mafano msanii wa chini ambae hata kufikisha views elf 1 ni kazi, basi anaweza kununua views hata laki moja ili aonekane ni maarufu bila kujali hasara atayopata kifedha.

2. Kupata vigezo vya kuanza kulipwa na youtube

Youtube huwa wanalipa, Kama ulikuwa hujui ndo nakujuza, Yale matangao yanayotokea kabla ya video kuanza, Hayawekwi bure, Kuna malipo wanapa mtu mwenye video ili awaruhusu kuweka tangazo lao kabla video yake haijaanza kuchezwa.

Sasa ili uanze kulipwa huwa kuna vigezo ni lazima ufikishe, Vigezo hivi ni kwama channel yako ya youtube inabidi iwe na subscribers zaidi ya elf 1 na iwe na jumla ya masaa elf 4 ambayo watu wote wameyatumia kuangalia videos zako zote,

Hivi vigezo vyote vinanunulika kwa njia nlizotaja ama za ziada.

Pia imekuwa biahsara kwa kuwauzia hizi account watu wasio na haya maarifa na wana haraka ya kuanza kulipwa mapema na yooutube, Nimeshuhudia accounts hizi zinauzwa laki 8 kwenye magroups ya wahitaji ambao mara nying huwa ni wasnii wanaochipukia, waandishi wa habari ama muhitaji yoyote,

3. Kufanya video iwe kwenye matokeo ya juu

MMfano una biashara ya nguo na u nataka kuzipormote upitia youtube, Umeweka video yako youtube ila ina views 10 tu na hata watu wakisechi "maduka mazuri ya nguo" video yako haipo hata kwenye matokeo 10, Hapo ndipo watu wanaweza kununu views, likes, comments, subscribes, n.k ili video ipande iwe hata ndani ya video 3 za mwanzo ili watu waione, watu wakiina video yako wanaweza kuja dukani kwako na wakawa wateja wa kudumu.

4. Kutengeneza pesa

Hapa napo hapatofautiani na pointi namba 3, Kuna platforms za udalali mitandaoni sikuhizi zinaitwa affiliate marketing, Masoko ya mtandaoni kama Amazon humpa daalali link ya bidhaa flani, na endapo mtu akinunua kupitia link hio basi dalali ana chake, sasa kuna watu wanatumia njia hizo nlizotaja point namba 3 ili kufanya video zao zionekane kwenye matokeo ya juu, Mfano mtu akisechi "TV nzuri" na akaingia kutazama video iliyowekwa na dalali na akanunua hio tv kwa milioni 2, na dalali akapewa gawio la laki 1, sasa kama wat 10 wamenunua kupitia hio link dalali ashapigaa bao hapo, hata kama alitumia laki 2 kununua views tayari ana faida.

JE, NI KWELI DIAMOND ANANUNUA VIEWS.

1621773824602.png


Hakika hii ni maada ambayo nimekutana nayo sehemu nyingi ila sikubahatika kumkta mtu alietoa jibu sahihi zaidi ya uzushi tu bila tafiti.

NO, HAPANA!!! Diamond hanunuie views,

Diamond anachofanya ni PROMOTION mitandaoni,

Huko facebook na instagram mtu yeyote anaweza kutengeneza promosheni kwa kutengeneza tangazo la sponsored, nadhani wengi tunakutana nayo tunapotumia facebok au instagram. Biashara ni matangazo wadau, na mziki wa hapa kwetu nao umegeuka biashara,

Haya matangazo ya sponsored mtu yoyote anaweza kutengeneza na uzuri ni kwamba unachagua kabisa lifikie watu wa mkoa gani, watu wa rika ipi, watu wanaopenda vitu gani, watu wa jinsia gani, n.k Ila unatakiwa kulipia maana hakuna cha bure, mfano unaweza kulipia elf 5 tangazo lako lifikie watu wa iringa na arusha ambao wana umri wa miaka 18 hdi 30 na ni jinsia ya kike, n.k

Unaweza kukutana na Tangazo la sponsoored la Diamond ukiwa unatumia facebook utakuta kuna picha ya cover ya mziki wake mpya na kuna maandishi kaweka yanasomeka Nakuomba utembelee youtube kutazama mziki wangu mpya......Je hii ni views??? Jibu ni hapana, Hapa katangaza tu, Sasa jukumu ndio linakuwa lako sasa aidha kupuuza ama kwenda youtube na kutazama huo mziki mpya na hapo ndio itakuwa imehesabika kama views, Kiufupi haina tofauti na njia nyingine kama wasanii wanavyoendaga kituo cha redio ili kutambulisha miziki yao mipya,

ila kwa sasa teknolojia imekuwa pana na watu wengi tunamiliki smartphone, kwa hio watu wamejiongeza!! akimaiza kutambulisha ngoma yake kwenye radio habweeki ama kuridhika !! anazamia na huku facebook na instagram kutujulisha kwamba katoa ngoma mpya.

Na kitu kingine niwaambie tu hiz views sio ujivuni ndugu zangu, Views ni pesa, Youtube wana mfumo wao wa malipo wa views unaitwa Adsense, hawa waandishi wa habari wanaoweka video zao youtube nao msidhani wanaweka bure, huwa wanalipwa. Mfano kwa views milioni 1 mtu anaweza kuchukua kama dola elf 1500 sawa na milioni 3 na laki kadhaa, views ni pesa.

..........................MWISHO ............................
 
Hahahahah hii ya shamba simu nitaiapply angalau kachaneli kangu kapate subscription 1000
 
Wenzetu huko simu ikipitwa na wakati anaitupa tu au anagawa, huku bongo hadi upate hizo simu elf 1 ni bora uwe umenunua viwanja
Hahahah sio lazima ninunue mkuu

Nikikutana na wana naomba simu zao naingia YouTube zao kwa bando langu na subscribe kazi Kwisha
 
Hahahah sio lazima ninunue mkuu

Nikikutana na wana naomba simu zao naingia YouTube zao kwa bando langu na subscribe kazi Kwisha
Yes ni fursa nzuri pia, Na unaweza kutengeneza kabisa group lako kufanya hii ishu.

Unatengeneza kama accounts zako tano za youtube, unawaambia watu kwenye group wa subsscribe na kucheki video flani ndefu ili upate kigezo cha account kufikish masaa elf 4.

Acount zikiwa zimefikia vigezo vya kupokea pesa we unaziuza unapata mshiko
 
Somo zuri, nimepata kitu mkuu japo sijajua You tube wanawalipa hao wenye viewer nyinginkwa namna gani? Nini hasa kigezo cha Malipo hayo?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom