Mtu anapona ukimwi kwa njia ya miujiza ? Ndiyo.

hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,430
2,000
Njia za Mungu hazichunguziki. Hakuna linaloshindikana kwake yeye aaminiye kua Mungu yupo na Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi. Ukimkiri kwa kinywa chako hata ukimwi hautakaa ndani yako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mwakaboko

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,895
2,000
Bibie Nasema ikiwa hao Wachungaji Kennedy au Kakobe, wanaweza kuwaombea Watu wenye Virusi vya HIV na wakapona basi itakuwa ni jambo la maana itabidi wagonjwa wote wenye hivyo Virusi vya HIV waende kwa Wachungaji hao wawili Kennedy au Kakobe, mimi hicho kitu hakiwezi kuniingia akili hata kama Wanaofanya hayo wachungaji itakuwa ni kweli mimi siwezi kuamini kabisa basi kutakuwa hakuna haja ya kwenda mtu hospitali ukiumwa tu nenda kwa Mchungaji Kakobe au Mchungaji Kennedy akuombee ili upone ninafikiri na uongo wa hali ya juu na huenda kwa hao Wachungaji ikwa hadithi ya kama ya Babu wa lolindo .
Mimi napingana na wewe katka hili, uponyaji upo ndugu yangu, mimi yamenitokea na sasa ni mwaka wa ishirini na tatu tangu nilipoombewa na Tatizo langu la ugonjwa likaisha, of-course sikuombewa na wajasiliamali bali na wenye Imani thabiti katika jina la Yesu Kristo. UPONYAJI UPO KWAKE AAMINIYE

kumbuka Mungu wetu hajaribiwa, ukienda kwa lengo la kujaribu inakula kwako, kwa 7bu amekataza kumjaribu isipokuwa kwa sadaka tu Wakristo tumeruhusiwa kumjaribu, wewe mungu wako sijui anafundisha vipi ktk hili.
 
mathcom

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,399
1,195
Nijibu ndiyo kwa sababu nimeongea uso kwa uso na KENNEDY MGOYEZI,anayeishi mkoani Arusha;ambaye ni shuhuda mmojawapo baada ya kutazama video ya shuhuda za waliopona ukimwi kwa njia ya maombezi kwenye YOUTUBE;nilipo tembelea www.bishopzacharykakobe.org
Tunahitaji data za watu waliokuwa HIV positive before maombezi na baada ya maombezi vipimo vikaonesha HIV negative
kama kuna mahali data hizi zipo basi tuanzie hapo na sio kwenye video!!!
 
MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,489
2,000
Mimi napingana na wewe katka hili, uponyaji upo ndugu yangu, mimi yamenitokea na sasa ni mwaka wa ishirini na tatu tangu nilipoombewa na Tatizo langu la ugonjwa likaisha, of-course sikuombewa na wajasiliamali bali na wenye Imani thabiti katika jina la Yesu Kristo. UPONYAJI UPO KWAKE AAMINIYE

kumbuka Mungu wetu hajaribiwa, ukienda kwa lengo la kujaribu inakula kwako, kwa 7bu amekataza kumjaribu isipokuwa kwa sadaka tu Wakristo tumeruhusiwa kumjaribu, wewe mungu wako sijui anafundisha vipi ktk hili.
Mkuu mwakaboko hakuna cha miujiza wala nini hiyo ni mbinu za Wachungaji ni mambo ya Uganga wa Kienyeji na uonga ndani yake Miujiza alifanya bwana YESu waliobakia hao wanafanya kiini macho cha hawa Wachungaji kutaka kuwavuta watu katika Makanisa yao wanayoongoza hao Wachungaji ni mambo ya uganga na uongo ndani yake nimeweka Video hapo juu hujaona wewe? Ebu angalia hizo video kisha utagunduwa uongo wa Wachungaji wanavyoongopea Wafuasi wao.
 
Last edited by a moderator:

BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,875
1,250
Mkuu Mzizimkavu na wenzako,fahamuni kwamba Mungu aliyeweza kufanya ''NABII MUSA ALIONA,FIMBO KAVU YA HARUNI IMECHIPUKA NA KUTOA MACHIPUKIZI;NA KUCHANUA MAUA;NA KUZAA MATUNDA YA MALOZI MABIVU,SIKU YA PILI YAKE KATIKA HEMA YA MUNGU;ILI KUKOMESHA MANENO YA WATU ![BIBLIA KITABU CHA HESABU 17:5-10].Kabla ya Bwana Yesu,miujiza ilitendeka na baada Kristo miujiza imeendelea kutendeka kila mahali ulimwenguni.Sikubaliani kamwe na msemo wa samaki mmoja akioza basi tenga zima limeoza;na kusema kuwepo wachunaji matapeli,basi wote ni wachungaji wasanii au wajasilimari.Nyakati zetu,wapo watumishi wa Mungu waaminifu wengi duniani,na Mungu anawatumia kuponya magonjwa yote kama UKIMWI na kila namna ya udhaifu kwa ishara,maajabu na miujiza kama nyakati za mitume na manabii wa Biblia Takatifu!!! Mwisho,nimepeleleza kwa muda haya,katika makanisa na huduma mbalimbali !
 
mwakaboko

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,895
2,000
nadhani hujanielewa nilichoandika. MUNGU HUYU ninamwaabudu mimi ndiye huyo huyo anaendeleza uuambaji wake, wengine watasema kuwa tumesikia akitenda miujiza na wengine watasema nikiini macho, mimi daima mimi nitasema ni BWANA amefanya maana yeye amesema JINA LANGU LIATAKAPO TAJWA KWA AJILI YA KuTENDA JAMBO BASI MIMI NITASIMAMA UPANDE WANGU na KUTENDA kile ambacho neno limetumwa kutenda. SISI wengine ndugu yangu tumemuona YESU akitenda jambo katika maisha yetu, NIMEMUOMBA ANIVUSHE AMENIVUSHA MPAKA SASA NAAMINI NI YEYE AMETENDA, kumbuka mpaka leo yeye bado ni MUNGU ANAYETENDA KWAKE YEYE AAMINIYE.

Lakini hata hivyo nisikubishie sana, kwa sababu kuamini neno imani zinatofautiana ktk ukuaji wake (sorry kama nimeongea lugha usioijua hapo). Manabii wa uwongo pia wapo. Tatu mimi sijui wewe unamuabudu MUNGU yupi, naomba nikuulize Je, unaamini ktk MUNGU BABA, MWANA na ROHO MT.? MUNGU nimwaminiye mimi ni yule anayejitambulishe kwa jina la MIMI NIKO, AMBAYE NIKO- kama ndiye huyo nawe wamwamini amini kuwa anaponya

Mkuu BAOBAO Usifananishe Miujiza Ya Nabii Musa aliyopewa

na Mwenyeezi Mungu kwa Firauni ukafafanisha na Miujiza ya Wachungaji hicho kitu sikubaliani nacho kabisa Nabii musa

alikuwa ni mtume wa Mwenyeezi Mungu Wachungaji wengi wao ni waongo wazinzi,wezi, wadanganyifu itakuwaje wawe

na miujiza? Ni uongo wa hali ya juu Hakuna miujiza ya kutibu Ukimwi hicho kitu sahau kabisa. Miujiza alifanya Bwana

YESU na wale Mitume wake 12 watu waliobakia ni matapeli wanafanya uganga pamoja na uongo wachungaji wengi

wanatumia uganga wa kienyeji kuwaongopea Waumini Eti wana miujiza kumbe ni amambo ya uganga wakienyeji na uongo ndani yake. mii pia ninaweza kufanya miujiza kama wanavyofanya wachungaji.

nadhani hujanielewa nilichoandika. MUNGU HUYU ninamwaabudu mimi ndiye huyo huyo anaendeleza uuambaji wake, wengine watasema kuwa tumesikia akitenda miujiza na wengine watasema nikiini macho, mimi daima mimi nitasema ni BWANA amefanya maana yeye amesema JINA LANGU LIATAKAPO TAJWA KWA AJILI YA KuTENDA JAMBO BASI MIMI NITASIMAMA UPANDE WANGU na KUTENDA kile ambacho neno limetumwa kutenda. SISI wengine ndugu yangu tumemuona YESU akitenda jambo katika maisha yetu, NIMEMUOMBA ANIVUSHE AMENIVUSHA MPAKA SASA NAAMINI NI YEYE AMETENDA, kumbuka mpaka leo yeye bado ni MUNGU ANAYETENDA KWAKE YEYE AAMINIYE.

Lakini hata hivyo nisikubishie sana, kwa sababu kuamini neno imani zinatofautiana ktk ukuaji wake (sorry kama nimeongea lugha usioijua hapo). Manabii wa uwongo pia wapo. Tatu mimi sijui wewe unamuabudu MUNGU yupi, naomba nikuulize Je, unaamini ktk MUNGU BABA, MWANA na ROHO MT.? MUNGU nimwaminiye mimi ni yule anayejitambulishe kwa jina la MIMI NIKO, AMBAYE NIKO- kama ndiye huyo nawe wamwamini amini kuwa anaponya
Mkuu mwakaboko Mungu ninaye muamini mimi ni yule Mwenyeezi Mungu aliyeziumba mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake wanyama ,Miti, wadudu,na banadamu . Na Mungu ninayemuabudu mimi ndiye yule

Mwenyeezi Mungu aliyewatuma Manabii na Mitume wake Ibrahim,Isaaka ,Yakubu,Mfalme Daudi,mfalme Suleyman,Nabii

Musa Bwana YESU,Na Mtume Muhammad rehema za mwenyeezi mungu ziwe juu yake na amani.Simuamini mi Mungu

katika nafsi 3 yaani Mungu Baba,Mungu Mwana,na mungu roho takatifu mungu watatu katika nafsi moja Mungu huyo

kwangu mimi anakuwa ni mungu feki kazi kwako na imani yako.
 
Last edited by a moderator:

HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
829
1,000
Hii inanikumbusha mcheshi Dave Chapelle alikuwa akiongea kuhusu kitabu cha The Secret, sijui kama unakifahamu. Basically, kinasema kwamba kitu chochote unachokitaka utakipata, ila inabidi u-visualize na uamini kwamba utakipata. Usipokipata ni kwasababu hukuwa na imani. Sasa Dave Chapelle akatoa mfano wa mtoto anaekufa na njaa kwenye kambi la wakimbizi aambiwe avisualize sahani ya chakula, na hicho chakula kitakuja tu. Kisipokuja, basi walikuwa hawaamini.

Sikatai kwamba miujiza haitokei, lakini huwezi kutegemea miujiza ya mungu ije kuokoa watu kwenye majanga. Miujiza ingekuwa inatokea kila siku isingekuwa miujiza tena.Kama unaamini mungu aliumba wanadamu, dunia, na mbingu nadhani unaweza kuamini kwamba mungu alitupa akili za kutatua matatizo yetu pia. Kama unavyoona nchi zingine watu hawasubiri mungu awashushie miujiza ili wapone ukimwi na magonjwa mengine hatari. Wanatumia akili zao kuvumbua madawa, na wanatumia akili zao kuepuka magonjwa. Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba.

Wachungaji wengi Tanzania wanaexploit waumini wakijua kuwa wako desperate. Wame give up, wanasubiri miujiza ya mungu, na ndio maana wanabaki kuhubiri kuhusu siku za mwisho, uponyaji, na kutoza sadaka kibao huku wakisema siku za mwisho zinakuja! Wote tutaenda paradiso, shida zenu mtaziacha duniani. At the end of the day mchungaji anapanda hummer anaelekea nyumbani kwenye ghorofa lake. Inakuja hiyo? Wachungaji wanaexploit imani za waumini wakijua kwamba huwezi kupima imani, wanatumia neno la mungu kusema mungu hajaribwi, na ukiombewa usipopona, basi ulikuwa huamini. Imani yako ndio tatizo, si mungu, therefore hakuna aliye responsible for your fate except you. Na ndio watu kama Babu Loliondo walivyotajirika.

Inawezekana huyo aliyepona ukimwi alipata false positive tests, au kweli ni miujiza. We will never know. Tunachojua ni ukimwi upo , tunajua unvyoambukizwa, kinga zipo, tujilinde.

Nijibu ndiyo kwa sababu nimeongea uso kwa uso na KENNEDY MGOYEZI,anayeishi mkoani Arusha;ambaye ni shuhuda mmojawapo baada ya kutazama video ya shuhuda za waliopona ukimwi kwa njia ya maombezi kwenye YOUTUBE;nilipo tembelea www.bishopzacharykakobe.org
 
BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,875
1,250
Baba Ibrahimu alimjibu tajiri mmoja kuwa wawasikilize Musa na manabii;maana hata akitoka peponi au mtu akisema amefufuka hawatashawishiwa na ushuhuda huo;kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo. Na hata leo,siyo watu wote wataamini uponyaji wa magonjwa kama Ukimwi kwa njia ya miujiza;hata watu wakionesha kabla na baada vyeti vya vipimo vyao. Mtu asiyeamini,hata kama atakutana uso kwa uso na aliyepona ukimwi mwenyewe kwa njia ya muujiza;bado anaweza asimwamini,kama Bwana Yesu alivyoelezea katika Injili ya LUKA 16:19-31.
 
HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
829
1,000
If it helps you sleep better at night, then go ahead and believe it was a miracle. I will not simply accept that someone was cured by miracle without asking questions first. That does not mean I'm faithless, it just means I'm not a blind sheep.
Baba Ibrahimu alimjibu tajiri mmoja kuwa wawasikilize Musa na manabii;maana hata akitoka peponi au mtu akisema amefufuka hawatashawishiwa na ushuhuda huo;kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo. Na hata leo,siyo watu wote wataamini uponyaji wa magonjwa kama Ukimwi kwa njia ya miujiza;hata watu wakionesha kabla na baada vyeti vya vipimo vyao. Mtu asiyeamini,hata kama atakutana uso kwa uso na aliyepona ukimwi mwenyewe kwa njia ya muujiza;bado anaweza asimwamini,kama Bwana Yesu alivyoelezea katika Injili ya LUKA 16:19-31.
 
Chokochoko

JF-Expert Member
Oct 15, 2011
438
250
duuh nafikiri kama imani yako0 itakua imebase kwenye kupambana na dawa mbadala pamoja na ARV bila kuvuruga timetable labda
ndiomiujiza ya kuishi bila0 ku8ugua huo ugonjwa itatendeka
 
Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
31,034
2,000
BAK miaka kama 6 kabla ya leo kuna kijana wa dada yangu alipimwa pale kcmc (kcmc kuna mdogo wangu anafanya kazi na ndiye aliyeshughulikia vipimo vyote) na akawa na hiv+ na cd4 zikawa zimeshuka sana japo alikuwa hajaanza dawa alikuwa ndani ya ushauri na dawa za kutibu yale magonjwa yaliyokuwa yanamsumbua kwa wakati huo mojawapo likiwa ni kifua ambacho ilibidi akatiwe kibong'oto hosp, tulichofanya sisi ni kuomba tu, ilikuwa kila saa tisa za usiku tunaashana watu kama watatu hivi ambao kila mmoja alikuwa mkoa tofauti, hivyo tunaanza maombi kweli tuliomba sana, Mungu alisikia maombi yetu, baada ya miezi kama mitatu alienda kupima tena pale kcmc ikawa - hawakuwaamini ikabidi akapimwe tena kule kibongo'oto hosp. wakakuta pia - hawakuamini wakatoa damu mshiba wa mkono wa kushoto na wa kulia ili kuhakikisha kweli ikawa -. Na hadi leo ni mzima ameoa na ana mtoto mmoja.

so mbele ya Mungu kila kitu kinawezekana BAK. (samahani .......sha na cha.... zinanishinda sana)

...labda kuna makosa yalifanyika katika vipimo vyake na hivyo kuonekana kama alikuwa HIV+ wakati si hivyo. Nimeshaona kesi nchi mbali mbali ambazo wahusika waliambiwa wako HIV+ kumbe kuna makosa yalifanyika na baadaye baadhi yao waliamua kufungua mashtaka dhidi ya hospitali na madaktari waliowapa hitimisho ambalo halikuwa kweli. Vinginevyo siamini kama unaweza kuponywa kimiujiza.
 
Last edited by a moderator:

msellegx

Member
Apr 18, 2013
11
45
There is nothing like kupona UKIMWI kwa kuombewa...niletee mgonjwa nimpime nijirdhishe ana mdudu thwn leteni huyo muombeaji...!!there is nothing like that..!!
Labda kama ulipewa kqa kubakwa...!!a virus can stay undetected and dormant for years...
 
Bondemania

Senior Member
Jan 12, 2012
102
195
Guys iko hivi,IMANI NDIO INAYOFUNGUA EVERYTHING,UKIAMINI KATIKA DAWA FULANI UTAPONA,UKIAMINI KATIKA MAOMBI UTAPONA,YOU KNOW WHY?WHAATERVER UTAKACHOILISHA NAFSI YAKO NDICHO KITAKACHOKUPA MATOKEO IWE NI NEGATIVE OR POSITIVE RESULTS,THATS IT
 
Mwanasheka

Member
Feb 26, 2013
16
0
Kama TASA na WAGUMBA wanapata watoto kwa jina la Yesu Kristo sembuse kupona UKIMWI. Kwa Yesu kila jambo linawezekana. Yeremia 32:27..Tazama mimi ni BWANA,MUNGU wa wote wenye MWILI: Je! kuna neno GUMU lolote NISILOLIWEZA?..Barikiwa
 
BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,875
1,250
Miujiza ya uponyaji ipo kwa 100%;amesema askofu Kakobe kuwa itakuwa dhahiri katika ziara yake nje ya Tanzania,na kuwa shuhuda hizo zitatangazwa hadharani na kuitikisa dunia kuanzia juni 20/2013 katika mkutano wa Injili,Toronto kama wanavyoelezea waumini wake.
 
Kwelitupu

Senior Member
Aug 22, 2012
111
195
Bibie Nasema ikiwa hao Wachungaji Kennedy au Kakobe, wanaweza kuwaombea Watu wenye Virusi vya HIV na wakapona basi itakuwa ni jambo la maana itabidi wagonjwa wote wenye hivyo Virusi vya HIV waende kwa Wachungaji hao wawili Kennedy au Kakobe, mimi hicho kitu hakiwezi kuniingia akili hata kama Wanaofanya hayo wachungaji itakuwa ni kweli mimi siwezi kuamini kabisa basi kutakuwa hakuna haja ya kwenda mtu hospitali ukiumwa tu nenda kwa Mchungaji Kakobe au Mchungaji Kennedy akuombee ili upone ninafikiri na uongo wa hali ya juu na huenda kwa hao Wachungaji ikwa hadithi ya kama ya Babu wa lolindo .

Ndugu yangu MziziMKavu, hapo kwenye Red; hili ndio tatizo kubwa la sisi wanadamu: IMANI HABA, sasa kama unakua na mtazamo hasi na imani haba kiasi hicho unawezaje kupona ukienda kanisani kuombewa? Nimeona hata kwa comments humu wengi wanaonyesha kutoamini miujiza kwa jina la Yesu, and that is EXACTLY WHY THEY HAVE NEVER EXPERIENCED ANY OR WILL NEVER SEE ANY MIRACLE in their lives!!!.
Kumbuka hata wakati wa Bwana Yesu alipokuwepo duniani pamoja na upako na uweza mkuu uliokuwa juu yake si wote waliponywa, ilitegemea na imani na mtazamo wa muhusika. Kuna siku alikwenda kwenye mji wa Nazareti na wakawa wanam-despise, ikawaje?: "57 And they took offense at Him...58 And He did not do miracles there because of their unbelief." Matthew 13:57-58

Tafakari.....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom