FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,018
- 40,686
Tuchukulie kwa mfano mtu anakuja kukushawishi akukopeshe pesa kiasi cha milioni 100 ili ujenge nyumba ya kuishi; ila sasa masharti ya huo mkopo ni kwamba lazima ramani za jemgo, vifaa vya kujengea, BOQ, na mafundi wote watoke kwake huyo anaekukopesha.
Halafu huyo anaekukopesha anakuletea ramani ya nyumba ya thamani ya milioni 10, ila kwakuwa QS aliyeandaa BOQ ni wake, anaweka thamani ya jengo ni milioni 100, hivyo pesa yote inaishia kwake katika material na mafundi, hivyo kujihakikishia soko la bidhaa zake na ajira kwa mafundi wake.
Na kwakuwa mkopo huu hauna riba , basi unapachikwa jina la ‘Mkopo wenye masharti nafuu’.
Sasa nauliza tu, huyu mtu anaechukua mkopo wa aina hii, ana akili timamu kweli?