Mtu ambaye hadi sasa hajaelewa somo la Makinikia, Ndege na Korosho lazima atakuwa na kichwa kizito.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mwezi wa pili alipokuja mwakilishi wa Barrick Afrika alituambia na waziri wa sheria wakati huo prof. Kalamaganda akatuhakikishia kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa tatu Barrick watakuwa wameshatulipa $300m.

Walio karibu na bandari watuambie kama yale makontena yapo.

Wakati huo huo serikali iliahidi hadi kufikia tarehe 31/3 mwaka huu wakulima wote wanaodai pesa za korosho watakuwa wamelipwa pesa zao.

Halafu nasikia mafundi wa chini ya mwembe wa Magomeni kota walichokonoa injini ya ndege pendwa ika noki, dah! mambo ni mengi muda ni mchache sana.

Kwa leo ngoja niishie hapa, kesho nitakumbushia maendeleo ya barabara ya njia 10 ambayo itakuwa ya kwanza barani Afrika.

Rais alituambia maendeleo hayana chama na watanzania sio wajinga wanaona nani mbabaishaji.
 
Back
Top Bottom