Mtu aliyewasumbua majasusi wa Mossad kwa miaka zaidi ya 20 kufanikiwa kumuua

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Ni Imad Mughniyeh. Mzaliwa wa Lebanon Disemba 7 mwaka 1962 katika kijiji chenye kukaliwa na washia wengi cha Tayr Dibba. familia yake ya kishia ilikuwa ya hali ya chini sana. Akiwa katika umri mdogo alionekana kuwa na ujasiri mkubwa kulinganisha na umri wake. Mengi hayajulikani ila elimu ya chuo alisomea uinjinia katika chuo cha American University of Beirut. Inasemakana alikuwa kijana mrefu, mwembamba, mtanashati na mcheshi sana. Baadae alikuja kuwa kiongozi mkubwa katika masuala ya kijeshi, intelijensia na usalama ndani ya kikundi cha Hezbollah nchini Lebanon

Kujihusisha na siasa

Akiwa katika umri mdogo alianza kujihusisha na chama cha siasa cha nchini Palestina cha Fatah. Mughniyeh alikuwa sehemu ya waanzilishi wa kikundi maalum cha makomandoo na operesheni maalum
FORCE 17 kilichokuwa chini ya kiongozi wa zamani wa Palestina bwana Yassir arafat miaka ya 70. Akiwa na miaka 22 alihamia kikundi cha Hezbollah cha nchini Lebanon baada ya kutofautiana na wenzake katika chama cha Fatah japo ushurikiano wa baina ya makundi hayo mawili ulikuwa uko pale pale katika mapambano dhidi ya Israel.

Akiwa na miaka 30 alihusika katika kuisuka upya Hezbollah na kukifanya kiwe kikundi cha kimapambano na kivita zaidi

Mughniyeh alikuwa mtu aliyekemea na asiyependa vurugu na ukatili.Aliamua kujihusisha na matukio ya kigaidi baada ya kaka yake kuuawa katika jaribio la CIA kumuua muasisi wa Hezbollah Sheikh Fadlallah mwaka 1985 na hiyo ndio ikawa ‘turning point’ ya kuamua kupambana na wamarekani na washirika wake

Uhusiano wake na Iran

Inasemekna Mughniyeh aliweza kuwa karibu sana watu wakubwa nchini Iran pamoja na vyombo vya usalama, na inasemekana ndiye aliyekuwa kiungo muhimu kati ya Hezbollah na Iran katika misaada ya kivita, kiintelijensia na kiulinzi. Hakuna maelezo ya wapi alipitia mafunzo ya kivita na inteligensia

Matukio aliyohusishwa nayo dhidi ya Marekani

Amekuwa akihusishwa katika upangaji na utekaji nyara na mauaji ya raia wengi na maofisa wa kigeni hasa wamarekani, waingereza na raia wa mataifa mengine ya ulaya nchini lebanoni akiwemo mkuu wa CIA kituo cha Beirut nchini Lebaon.

Mwaka 1985 aliweza kuteka ndege ya kimarekani na kuipeleka mji wa Beirut nchini Lebanon

Ulipuaji wa kambi ya jeshi ya Marekani nchini Lebanon mwaka 1983 na kupelekea vifo vya wanajeshi wengi wa Marekani

Akiwa na miaka tu 22 akawa ndio mtu anayetafutwa kuliko yeyote na vyombo ya ulinzi na usalama vya nchini marekani(kabla ya September 11), na CIA wakaanza mchakato wa kulipiza kisasi. fedha taslimu dola za kimarekani milioni 5 ziltengwa kama zawadi kwa atakaesaidia kupatikana kwake.

Baadhi ya matukio aliyohusishwa nayo dhidi ya Israel

Mwaka 1983 alihusishwa na bomu la kujitoa mhanga ndani ya gari lililoharibu jengo lililokuwa linatumiwa na makachero wa usalama wa ndani wa Israel shin bet kama makao makuu yake nchini Lebanon katika mji wa Port of tyre na kuua waisrael 28 wakiwemo wafungwa 32 wa kilebanoni waliokuwa wakishikiliwa katika jengo hilo.

Mwaka mmoja baadae jengo lingine karibu na hilo pia likitumiwa na makachero wa Shin bet lilipuliwa na kupelekea kuuawa kwa waisreal 78

Alihusika katika ulipuaji wa ubalozi wa Israel nchini Argentina na kuua watu 29 wakiwemo wanadiplomasia wa Israel mwaka 1994

Ulipuaji wa jengo la jumiuiya ya kiyahudi nchini Argentina mwaka huo huo na kuua waisrael 85 na kujeruhi zaidi ya 300. Matukio haya mawili nchini Argentina bado mpaka leo yanayanatoa changamoto kubwa Rais wa sasa wa Argentina mama Fernandez.

Kwa matukio haya na mengine mengi, vyombo vya usalama Mossad na cha intelijensia ya jeshi cha Amaan waliafikiana kuwa kumuua bwana Mughniyeh itakuwa moja suluhisho kwani yeye ndiye aliyegundulika kuwa mpangaji mkuu wa wa mipango yote ya mashambulizi dhidi ya Israel. Pia waliafikiana kuwauwa viongozi waandamizi wa kikundi cha Hezbollah kulipa kisasi.

Mafichoni

Baada ya Mughniyeh kuona viongozi waandamizi wa Hezbollah wanauawa na Israel katika kilichoonekana kulipiza kisasi akaamua kufanya upasuaji wa uso (plastic surgery) kujibadilisha muonekano wake ili asiweze kutambulika na inasemekena mpaka mda huo vyombo vya usalama vya Israel vilikuwa na picha yake moja tu.

Baada ya muda Mossad wakapoteza surveillance juu ya Mughniyeh, wakawa hawajui alipo na inasemekana alikuwa nje ya Lebabon, wakaamua wafanye kitu chochote kitakachoweza kumfanya arudi nchini Lebanon ili wamtie kwenye himaya yao.

Mwaka 1994 Mossad wakaamua kumfuata mdogo wake Mughniyeh aliyejulikana kwa jina la Fuad ambaye pia alikuwa akijihusisha na harakati za Hezbollah ili wamtumie kumpata Mughniyeh. Baada ya Fuad kukataa kufanya nao kazi wakaamua mpango wa pili ni kumuua Fuad ili Mughniyeh atakapokuja kwenye mazishi watekeleze azma yao kwani kwa taratibu za kishia ni muhimu sana kuhudhuria mazishi ya ndugu yako wa damu. Na mpango huo ulitekelezwa na jasusi wa Israel nchini Lebanon bwana Ahmed halek ambaye alikuwa ni mlebanoni.

Baada ya kumuua Fuad, Mughniyeh hakuonekana katika mazishi, inasemekana hakuudhuria au alihudhuria katika namna ambayo hawakuweza kufahamu.

Baada ya kifo cha mdogo wake Bwana Imad akaagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya kifo cha mdogo wake, na kupelekea walebanoni wengi waliokuwa wakijasusi kwa ajili ya Israel kukamatwa kwa wingi. Lakini kiongozi wa tukio hilo bwana Ahmed Halek na mkewe walikuwa wameshakimbizwa na Mossad kusini mwa Lebanon kulikokuwa kukidhibitiwa na majeshi ya Israel. Baadae wakashauriwa wapelekwe nje ya nchi kwa usalama wao zaidi na wakakubali kuelekea nchi moja ulaya ambayo haikutajwa. Lakini baada miezi michache waliamua kurudi kusini mwa Lebanon baada ya kuona tabu kuendana na mazingira ya nchi waliyopelekwa kufichwa. Baada ya kurudi wakakabidhiwa ulinzi wa masaa 24 na Israel na wakaonywa kuwa wakimya sana na ku ‘keep low profile’

Mughniyeh na timu yake wakafahamu ujio wa bwana Halek na baada ya kumchunguza kwa mda wakagundua udhaifu wake wa kupenda pombe na wanawake na wakamtengenezea mtego. Wakaamua kumtumia agent wao aliyejulikana kwa jina la Ramzi Nahara. Huyu alikuwa drug dealer na informer wa Mossad kwa miaka mingi, aliwahi kukamatwa na Hezbollah ambao baada ya mda chache walimuacha huru(tofauti na waliokuwa wakiuawa), hivyo alijihisi ana deni la kuwalipa Hezbollah kwa kumuacha hai ambao baada ya makubaliano ya kumuacha wakamgeuza kuwa ‘Double agent’ wao na wakamuweka katika listi ya wafungwa wa kubalishana na wafungwa wa Hezbollah waliokuwa wakishikiliwa na Israel, hivyo mpaka mda huu waisrael hawakugundua kuwa ameshabadili upande na wakamgomboa kama ‘asset’ wao na akaendelea na maisha kama kawaida ya kuwa informer wa Israel kusini mwa Lebanon.

Ramzi akaagizwa amualike bwana Nahara kwenye sherehe ndogo na marafiki wengine na kumuahidi kuwepo kwa pombe na wanawake wa kumwaga, bwana Nahara bila ajizi akakubali na akaamua kuwatoroka walinzi wake ili apate uhuru zaidi wa kujiachia katika sherehe hiyo. kwenye sherehe Ramzi akamewekea madawa ya kulevya kwenye kinywaji akalewa, wakambeba na kumtia kwenye buti la gari na kumpeleka Beirut kwa ajili ya interrogation ambapo inasemekana Mughniyeh alikuwepo na alimkata baadhi ya vidole katika 'interrogation' hiyo na mwisho bwana Ahmed Halek akakiri kufanya kazi na Israel kwa miaka mingi na kuhusika katika kifo cha mdogo wake. Akatoa siri nyingi za taarifa za mafunzo ya kijasusi aliyopitia nchini Israel na Cyprus chini ya vyombo ya usalama ya Israel. Kisha akashtakiwa na kuuawa mwaka 1996.
Bwana Nahara nae akagundilika na vyombo vya usalama ya Israel kuwa ni double agent wa Hezbollah na kuuawa.

Baada ya matukio haya, bwana Mughniyeh akawa target namba moja wa Mossad. Waliendelea kumtafuta kwa miaka yote hiyo na hatimae mwaka 2000, wakati viongozi wakuu watano Hezbollah wakitembelea kambi ya kishia karibu na mpaka wa Israel, afisa wa jeshi wa Israel IDF akagundua tukio hilo na kugundua wale ni viongozi wa Hezbollah, akapiga picha na kuzituma makao ya vyombo vya ulinzi kwa ajili ya uchambuzi na ikagundulika bwana Mughniyeh mbali na kujibadili sura alikuwa miongoni mwa wale viongozi watano. Haraka haraka maandalizi yakafanyika nchini Israel kuandaa ‘sniper’ kwa ajili ya kumtungua bwana Mughniyeh. Lakini ilitakiwa wapate ruhusa ya waziri mkuu bwana Ehud Barak kuikamilisha mission hiyo, ambaye alikataa ku ‘take risk’ kwani ulikuwa umepita muda mchache tangu suluhu ya kusimamisha mapigano kufikiwa kati ya Israel na kikundi cha Hezbollah, suluhu ambayo jamii ya kimataifa ilipata tabu sana kuhahikikisha inafikiwa. Waziri mkuu alikuwa na wasiwasi kuwa kumuua Mughniyeh ndani ya ardhi ya Lebaon ingekuwa kama kutangaza kuvunja suluhu hiyo ya makubaliano na hivyo kuogopa lawama kubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa. Maamuzi hayo hayakuwafurahisha wanausalama nchini isreal na kuyaona ni maamuzi laini.

Kufikia wakati huu akawa ndio most wanted kwa vyombo vya usalama vya nchi za Ulaya, Isreal na Marekani

Jaribio la Marekani kumkamata

Miaka ya 2000 wamarekani kupitia NSA walinasa mawasiliano na kugundua ndege Mughniyeh aliyokuwa ameipanda kutokea Iran kwenda Syria kupitia Kuwait. CIA wakaviomba vyombo vya mamlaka vya Kuwait kuichelewesha ndege hiyo kuondoka itakapotua ili makomandoo wa jeshi la Marekani wa NAVY SEAL wafike na kumkamata bwana Mughniyeh. Mamlaka za Kuwait ziliweza kuizuia ndege hiyo kwa lisaa limoja tu na wakaamua kuiachia kuondoka baada ya kuingiwa na woga wakihofia kisasi cha Hezbollah. Hivyo jaribio hilo likashindikana

Kwa mujibu wa afisa wa zamani wa CIA bwana Rober Baer anasema Mughniyeh inawezekana kabisa akawa ndio mtu mwenye akili nyingi sana waliyewahi kupambana nae, wakiwemo KGB au mtu yeyote.

Kuuawa Mughniyeh

Baada ya miaka mingi bila mafanikio Mossad na CIA wakaafikiana kufanyana operation ya pamoja kumuua Mughniyeh, Mossad wakachukua jukumu la kufanya surveillance na CIA wakachukua jukumu la kushambulia

Mughniyeh inasemekana alikuwa makini sana mwenye tabia ya kubadilika sana, akiingia mlango mmoja anatoka na mwengine,haweki appointments kwenye simu, hatabiriki, kutwa kubadilisha magari na 'safe houses' na nadra sana kusafiri. Mossad na CIA waliendelea kusubiri mpaka nafasi na hatimae mwaka 2008 Damascus nchini Syria waliona mwanya wa kumuua Mughniyeh baada ya yeye kujisahau na kuanza kuona yuko salama na kufikia kuacha kutembea na walinzi wake, kuzurura na kuanza kuchukua wanawake hovyo. Baada ya kuchunguza mienendo yake hatimae walifanikiwa kuweka bomu katika gari lake Februari 12 2008 na alivyoingia bomu lililipuka na ndio ukawa mwisho bwana Mughniyeh. Na furaha iliyopatikana nchini Israel kwa kuuawa bwana Mughniyeh ni sawa na furaha iliyopatiakana nchini marekani baada ya kuuawa kwa Osama bin laden, wana report bwana DAN RAVIV na YOSSI MELMAN katika kitabu chao SPIES AGAINST ARMAGEDDON; Inside Israel’'s Secret Wars

January 2015 israel ikitumia ndege mbili zisizokuwa na rubani 'drones' ilishambulia msafara wa viongozi wa Hezbollah nchini Syria karibu na mpaka wa Israel na kumuua mtoto mkubwa wa Mughniyeh Jihad Mughniyeh, miaka 25 aliyekuwa pia mpiganaji wa Hezbollah

wenye ujuzi zaidi karibuni
 
Nimewai kuona documentary ya huyu mtu ila siwezi kusimulia vizuri namna hii!
 
Hapo kwenye matukio ya argentine ni kweli hadi leo yanamtesa huyu mama kuhusu bombing of israel diplomatics.
 
Ni Imad Mughniyeh. Mzaliwa wa Lebanon Disemba 7 mwaka 1962 katika kijiji chenye kukaliwa na washia wengi cha Tayr Dibba. familia yake ya kishia ilikuwa ya hali ya chini sana. Akiwa katika umri mdogo alionekana kuwa na ujasiri mkubwa kulinganisha na umri wake. Mengi hayajulikani ila elimu ya chuo alisomea uinjinia katika chuo cha American University of Beirut. Inasemakana alikuwa kijana mrefu, mwembamba, mtanashati na mcheshi sana. Baadae alikuja kuwa kiongozi mkubwa katika masuala ya kijeshi, intelijensia na usalama ndani ya kikundi cha Hezbollah nchini Lebanon

kujihusisha na siasa

Akiwa katika umri mdogo alianza kujihusisha na chama cha siasa cha nchini Palestina cha Fatah. Mughniyeh alikuwa sehemu sehemu ya waanzilishi wa kikundi maalum cha makomandoo na operesheni maalum FORCE 17 kilichokuwa chini ya kiongozi wa zamani wa Palestina bwana Yassir arafat miaka ya 70. Akiwa na miaka 22 alihamia kikundi cha Hezbollah cha nchini Lenaon baada ya kutofautiana na wenzake katika chama cha Fatah japo ushurikiano wa baina ya makundi hayo mawili ulikuwa uko pale pale katika mapambano dhidi ya Israel.

Akiwa na miaka 30 alihusika katika kuisuka upya Hezbollah na kukifanya kiwe kikundi cha kimapambano na kivita zaidi

Mughniyeh alikuwa mtu aliyekemea na asiyependa vurugu na ukatili.Aliamua kujihusisha na matukio ya kigaidi baada ya kaka yake kuuawa katika jaribio la CIA kumuua muaisi wa Hezbollah Sheikh Fadlallah mwaka 1985 na hiyo ndio ikawa ‘turning point’ ya kuamua kupambana na wamarekani na washirika wake

Uhusiano wake na Iran

Inasemekna Mughniyeh aliweza kuwa karibu sana watu wakubwa nchini Iran pamoja na vyombo vya usalama, na inasemekana ndiye aliyekuwa kiungo muhimu kati ya Hezbollah na iran katika misaada ya kivita, kiintelijensia na kiulinzi. Hakuna maelezo ya wapi alipitia mafunzo ya kivita na inteligensia

Matukio aliyohusishwa nayo dhidi ya Marekani

Amekuwa akihusishwa katika upangaji na utekaji nyara na mauaji ya raia wengi na maofisa wa kigeni hasa wamarekani, waingereza na raia wa mataifa mengine ya ulaya nchini lebanoni akiwemo mkuu wa CIA kituo cha Beirut nchini lebaon.

Mwaka 1985 aliweza kuteka ndege ya kimarekani na kuipeleka mji wa Beirut nchini lebanoni

Ulipuaji wa kambi ya jeshi ya marekani nchini Lebanon mwaka 1983 na kupelekea vifo vya wanajeshi wengi wa marekani

Akiwa na miaka tu 22 akawa ndio mtu anayetafutwa kuliko yeyote na vyombo ya ulinzi na usalama vya nchini marekani(kabla ya September 11), na CIA wakaanza mchakato wa kulipiza kisasi. fedha taslimu dola za kimarekani milioni 5 ilittengwa kama zawadi kwa atakaesaidia kupatikana kwake.

Baadhi ya matukio aliyohusishwa nayo dhidi ya Israel

Mwaka 1983 alihusishwa na bomu la kujitoa mhanga ndani ya gari liliharibu jengo lililokuwa linatumiwa na makachero wa usalama wa ndani wa Israel shin bet kama makao makuu yake nchini Lebanon katika mji wa Port of tyre na kuua waisrael 28 wakiwemo wafungwa 32 wa kilebanoni waliokuwa wakishikiliwa katika jengo hilo.

Mwaka mmoja baadae jengo lingine karibu na hilo pia likitumiwa na makachero wa Shin bet lilipuliwa na kupelekea kuuawa kwa waisreal 78

Alihusika katika ulipuaji wa ubalozi wa Israel nchini Argentina na kuua watu 29 wakiwemo wanadiplomasia wa Israel mwaka 1994

Ulipuaji wa jingo la jumiuiya ya kiyahudi nchini Argentina mwaka huo huo na kuua waisrael 85 na kujeruhi zaidi ya 300. Matukio haya mawili nchini Argentina bado mpaka leo yanayanatoa changamoto kubwa Rais wa sasa wa Argentina mama Fernandez.

Kwa matukio haya na mengine mengi, vyombo vya usalama Mossad na cha intelijensia ya jeshi cha Amaan waliafikiana kuwa kumuua bwana Mughniyeh itakuwa moja suluhisho kwani yeye ndiye aliyegundulika kuwa mpangaji mkuu wa wa mipango yote ya mashambulizi dhidi ya Israel. Pia waliafikiana kuwauwa viongozi waandamizi wa kikundi cha Hezbollah kulipa kisasi.

Mafichoni

Baada ya mughniyeh kuona viongozi waandamizi wa Hezbollah wanauawa na Israel katika kilichoonekana kulipa kisasi akaamua kufanya upasuaji wa uso (plastic surgery) kujibadilisha muonekano wake ili asiweze kutambulika na inasemekena mpaka mda huo vyombo vya usalama vya Israel vilikuwa na picha yake moja tu.

Baada ya muda Mossad wakapoteza surveillance juu ya Mughniyeh, wakawa hawajui alipo na inasemekana alikuwa nje ya Lebabon, wakaamua wafanye kitu chochote kitakachoweza kumfanya arudi nchini Lebanon ili wamtie kwenye himaya yao.

Mwaka 1994 Mossad wakaamua kumfuata mdogo wake Mughniyeh aliyejulikana kwa jina la Fuad ambaye pia alikuwa akijihusisha na harakati za Hezbollah ili wamtumie kumpata Mughniyeh. Baada ya Fuad kukataa kufanya nao kazi wakaamua mpango wa pili ni kumuua Fuad ili Mughniyeh atakapokuja kwenye mazishi watekeleze azma yao kwani kwa taratibu za kishia ni muhimu sana kuhudhuria mazishi ya ndugu yako wa damu. Na mpango huo ulitekelezwa na jasusi wa Israel nchini Lebanon bwana Ahmed halek ambaye alikuwa ni mlebanon.

Baada ya kumuua Fuad, Mughniyeh hakuonekana katika mazishi, inasemekana hakuudhuria au alihudhuria katika namna ambayo hawakuweza kufahamu.

Baada ya kifo cha mdogo wake Bwana Imad akaagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya kifo cha mdogo wake, na kupelekea walebanoni wengi waliokuwa wakijasusi kwa ajili ya Israel kukamatwa kwa wingi. Lakini kiongozi wa tukio hilo bwana Ahmed Halek na mkewe walikuwa wameshakimbizwa na Mossad kusini mwa Lebanon kulikokuwa kukidhibitiwa na majeshi ya Israel. Baadae wakashauriwa wapelekwe nje ya nchi kwa usalama wao zaidi na wakakubali kuelekea nchi moja ulaya ambayo haikutajwa. Lakini baada miezi michache waliamua kurudi kusini mwa Lebanon baada ya kuona tabu kuendana na mazingira ya nchi waliyopelekwa kufichwa. Baada ya kurudi wakakabidhiwa ulinzi wa masaa 24 na Israel na wakaonywa kuwa wakimya sana na ku ‘keep low profile’

Mughniyeh na timu yake wakafahamu ujio wa bwana Halek na baada ya kumchunguza kwa mda wakagundua udhaifu wake wa kupenda pombe na wanawake na wakamtengenezea mtego. Wakaamua kumtumia agent wao aliyejulikana kwa jina la Ramzi Nahara. Huyu alikuwa drug dealer na informer wa Mossad kwa miaka mingi, aliwahi kukamatwa na Hezbollah ambao baada ya mda chache walimuacha huru(tofauti na walikuo kuwa wakiuawa), hivyo alijihisi ana deni la kuwalipa Hezbollah kwa kumuacha hai ambao baada ya makubaliano ya kumuacha wakamgeuza kuwa ‘Double agent’ wao na wakamuweka katika listi ya wafungwa wa kubalishana na wafungwa wa Hezbollah waliokuwa wakishikiliwa na Israel, hivyo mpaka mda huu waisrael hawakugundua kuwa ameshabadili upande na wakamgomboa kama ‘asset’ wao na akaendelea na maisha kama kawaida ya kuwa informer wa Israel kusini mwa Lebanon.

Ramzi akaagizwa amualike bwana Nahara kwenye sherehe ndogo na marafiki wengine na kumuahidi kuwepo kwa pombe na wanawake wa kumwaga, bwana Nahara bila ajzii akakubali na akaamua kuwatoroka walinzi wake ili apate uhuru zaidi wa kujiachia katika sherehe hiyo. kwenye sherehe Ramzi akamewekea madawa ya kulevya kwenye kinywaji akalewa, wakambeba na kumtia kwenye buti na kupelekwa Beirut kwa ajili ya interrogation ambapo inasemekana Mughniyeh alikuwepo na alimkata baadhi ya vidole katika 'interrogation' hiyo na mwisho bwana Ahmed Halek akakiri kufanya kazi na Israel kwa miaka mingi na kuhusika katika kifo cha mdogo wake. Akatoa siri nyingi za taarifa za mafunzo ya kijasusi aliyopitia nchini Israel na Cyprus chini ya vyombo ya usalama ya Israel. Kasha akashtakiwa na kuuawa mwaka 1996.
bwana Nahara nae akagundilika na vyombo vya usalama ya Israel kuwa ni double agent wa Hezbollah na kuuawa.

Baada ya matukio haya, bwana Mughniyeh akawa target namba moja wa Mossad. Waliendelea kumtafuta kwa miaka yote hiyo na hatimae mwaka 2000, wakati viongozi wakuu watano Hezbollah wakitembelea kambi ya kishia karibu na mpaka wa Israel, afisa wa jeshi wa Israel IDF akagundua tukio hilo na kugundua wale ni viongozi wa Hezbollah, akapIga picha kuzituma makao ya vyombo vya ulinzi kwa ajili ya uchambuzi na ikagundulika bwana Mughniyeh mbali na kujibadili sura alikuwa miongoni mwa wale viongozi watano. Haraka haraka maandalizi yakafanyika nchini Israel kuandaa ‘sniper’ kwa ajili ya kumtungua bwana Mughniyeh. Lakini ilitakiwa wapate ruhusa ya waziri mkuu bwana Ehud Barak kuikamilisha mission hiyo, ambaye alikataa ku ‘take risk’ kwani ulikuwa umepita muda mchache tangu suluhu ya kusimamisha mapigano kufikiwa kati ya Israel na kikundi cha Hezbollah, suluhu ambayo jamii ya kimataifa ilipata tabu sana kuhahikikisha inafikiwa. Waziri mkuu alikuwa na wasiwasi kuwa kumuua Mughniyeh ndani ya ardhi ya Lebaon ingekuwa kama kutangaza kuvunja suluhu hiyo ya makubaliano na hivyo kuogopa lawama kubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa. Maamuzi hayo hayakuwafurahisha wanausalma nchini isreal na kuyaona ni maamuzi ya laini.

Kufikia wakati huu akawa ndio most wanted kwa vyombo vya usalama vya nchi za ulaya, Isreal na Marekani

Jaribio la Marekani kumkamata

Miaka ya 2000 wamarekani kupitia NSA walinasa mawasiliano na kugundua ndege Mughniyeh aliyokuwa ameipanda kutokea Iran kwenda Syria kupitia Kuwait. CIA wakaviomba vyombo vya mamlaka vya Kuwait kuichelewesha ndege hiyo kuondoka itakapotua ili makomandoo wa jeshi la Marekani wa NAVY SEAL wafike na kumkamata bwana Mughniyeh. Mamlaka za Kuwait ziliweza kuizuia ndege hiyo kwa lisaa limoja tu na wakaamua kuiachia kuondoka baaa ya kuingiwa woga wakihofia kisasi cha Hezbollah. Hivyo jaribio hilo likashindikana

Kwa mujibu wa afisa wa zamani wa CIA bwana Rober Baer anasema Mughniyeh inawezekana kabisa akawa ndio mtu mwenye akili nyingi sana waliyewahi kupambana nae, wakiwemo KGB au mtu yeyote.

Kuuawa Mughniyeh

Baada ya miaka mingi bila mafanikio Mossad na CIA wakaafikiana kufanyana operation ya pamoja kumuua Mughniyeh, Mossad wakachukua jukumu la kufanya surveillance na CIA wakachukua jukumu la kushambulia

Mughniyeh inasemekana alikuwa makini sana mwenye tabia ya kubadilika sana, akiingia mlango mmoja anatoka na mwengine,haweki appointments kwenye simu, hatabiriki, kutwa kubadilisha magari na 'safe houses' na nadra sana kusafiri. Mossad na CIA waliendelea kusubiri mpaka nafasi na hatimae mwaka 2008 Damascus nchini Syria waliona mwanya wa kumuua Mughniyeh baada ya yeye kujisahau na kuanza kuona yuko salama na kufikia kuacha kutembea na walinzi wake, kuzurura na kuanza kuchukua wanawake hovyo. Baada ya kuchunguza mienendo yake hatimae walifanikiwa kuweka bomu katika gari la Mughniyeh Februari 12 2008 na alivyoingia bomu lililipuka na ndio ukawa mwisho bwana Mughniyeh. Na furaha iliyopatikana nchini Israel kwa kuuawa bwana Mughniyeh ni sawa na furaha iliyopatiakana nchini marekani baada ya kuuawa kwa Osama bin laden, wana report bwana DAN RAVIV na YOSSI MELMAN katika kitabu chao SPIES AGAINST ARMAGEDDON; Inside Israel’s Secret Wars

January 2015 israel ikitumia ndege mbili zisizokuwa na rubani 'drones' ilishambulia msafara wa viongozi wa Hezbolla nchini Syria karibu na mpaka wa Israel na kumuua mtoto mkubwa wa Mughniyeh anaitwa Jihad Mughniyeh, miaka 25 aliyekuwa pia mpiganaji wa Hezbollah

wenye ujuzi zaidi karibuni

Japo hii sio tetesi lakini umenikumbusha riwaya za James bond na James Hadley Chase R.I.P sana mabingwa huko mlipo naamini mnakula bata
 
Pumbav unajivunia ugaid

Anajivunia nani??!!!
Neno ugaidi inategemea uko upande gani na tafsiri yako inaegemea paradigm gani juu ya matumizi yake. . . . .ingawa sikubaliani na (ugaidi??!!!)
Hebu msome (Machiaveli???!!) juu ya retaliation. . . . .

Habari hiyo inataka jicho la tatu kuielewa maana ina maswali na.mafundisho mengi sana haswa kwa wewe "uneyuogopa" ugaid kiasi hutaki kufikiri. . . .
1. Wanapata wapi mafunzo??!!
2. Wanachaguliwa lini, wapi na kwa vigezo gani maana wanaovuma ni "watu" haswa. . .!!!
3. Link zilizopo kati ya makundi hayo ya "kigaid" na backbone yao. .
4. Je ni kweli wana uhusiano na vikosi fulani fulani vya ulinzi katika nchi fulani fulani mathalani umesoma hapo drug dealer nchini X ni informer wa force Z nchini G . . . . wakati nchini G unga hauruhusiwi. . . ."sabotage" hiyo ni accidental au planned and sustained project?!!

Mi nadhani badala ya kuwa na chuki zinazo "curb" akili anza kutazama ugaid kama mfumo mpana sana
 
Pumbav unajivunia ugaid

Hapana mkuu mimi siwezi kupenda ugaidi mkuu nauchukia sana, kwanza nikujulishe hiyo habari au story nimecopy na kupaste kwenye vitabu vyao wenyewe vinahusu intelligensia yao, na hayo ni maelezo kutoka kwa wakuu intelligensia hizo. Nia kwanza ni kushare nini kilikuwa kinaendelea behind the scenes na kupata elimu kuhusu haya mambo. Lakini pia wao waliweka kwa lengo pia la kujivunia waliyoweza kufanikisha na pia kuwajulisha raia wao kwamba wasione tu kimya ni vyombo vyao vya usalama vinahangaika kucha kuhakikisha taifa liko salama Na wamesucrife maisha ya watu wengi tu na haikuwa kazi rahisi wao kupata ushindi. Mimi nimeshaandika kuhusu KIDON ambayo ni Assasination unit ya KIDON lakini si kweli kwamba eti nakubaliana na kila wanalofanya. stineriga
 
Anajivunia nani??!!!
Neno ugaidi inategemea uko upande gani na tafsiri yako inaegemea paradigm gani juu ya matumizi yake. . . . .ingawa sikubaliani na (ugaidi??!!!)
Hebu msome (Machiaveli???!!) juu ya retaliation. . . . .

Habari hiyo inataka jicho la tatu kuielewa maana ina maswali na.mafundisho mengi sana haswa kwa wewe "uneyuogopa" ugaid kiasi hutaki kufikiri. . . .
1. Wanapata wapi mafunzo??!!
2. Wanachaguliwa lini, wapi na kwa vigezo gani maana wanaovuma ni "watu" haswa. . .!!!
3. Link zilizopo kati ya makundi hayo ya "kigaid" na backbone yao. .
4. Je ni kweli wana uhusiano na vikosi fulani fulani vya ulinzi katika nchi fulani fulani mathalani umesoma hapo drug dealer nchini X ni informer wa force Z nchini G . . . . wakati nchini G unga hauruhusiwi. . . ."sabotage" hiyo ni accidental au planned and sustained project?!!

Mi nadhani badala ya kuwa na chuki zinazo "curb" akili anza kutazama ugaid kama mfumo mpana sana

Ni kweli kabisa mkuu kuna mengi ya kujifunza, ukiangalia huyu jamaa hakuwa kabisa anapenda mambo ya violence, lakini motives yake ilikuwa ni kisasi. Kwa hiyo mtu anaweza leo akawa safi kesho unashangaa amekuwa gaidi, muuaji, jambazi n.k
 
Anajivunia nani??!!!
Neno ugaidi inategemea uko upande gani na tafsiri yako inaegemea paradigm gani juu ya matumizi yake. . . . .ingawa sikubaliani na (ugaidi??!!!)
Hebu msome (Machiaveli???!!) juu ya retaliation. . . . .

Habari hiyo inataka jicho la tatu kuielewa maana ina maswali na.mafundisho mengi sana haswa kwa wewe "uneyuogopa" ugaid kiasi hutaki kufikiri. . . .
1. Wanapata wapi mafunzo??!!
2. Wanachaguliwa lini, wapi na kwa vigezo gani maana wanaovuma ni "watu" haswa. . .!!!
3. Link zilizopo kati ya makundi hayo ya "kigaid" na backbone yao. .
4. Je ni kweli wana uhusiano na vikosi fulani fulani vya ulinzi katika nchi fulani fulani mathalani umesoma hapo drug dealer nchini X ni informer wa force Z nchini G . . . . wakati nchini G unga hauruhusiwi. . . ."sabotage" hiyo ni accidental au planned and sustained project?!!

Mi nadhani badala ya kuwa na chuki zinazo "curb" akili anza kutazama ugaid kama mfumo mpana sana

Mkuu hapa unaangaika kumuelewesha mtu wa kufuata mkumbo.
Hawa ni aina ya watu wa kukariri.

Ni vigumu sana kwa kuyaelewa mambo ya dunia hii kwa upana.
ndio maana wanaishia kuwa kasuku
 
Japo story imesheheni mauaji, lakini najifunza kuwa kuna watu wanajua sana kutumia brains zao effectively ktk given tasks
 
Back
Top Bottom