Mtu aliyekuwa mbunge na Waziri kwa miaka zaidi ya 20 ukimwambia mishahara ya watumishi wa umma ni midogo, hawezi kukuelewa isipokuwa tu...

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kama mtu huyo ni mtu considarate,ana utu,hajasahau alikotoka na zaidi ni mtu mwenye kusikiliza ushauri anaopewa na wasaidizi wake.

Mtu wa aina hiyo na ambae yeye kwa miaka mingi karibu kila kitu anagharamiwa na serikali kuanzia nyumba ya kuishi,chakula,mavazi,walinzi,wafanyakazi wa nyumbani,n.k anaweza kuwaona hamjitumi,mnadeka,wavivu,walalamishi,n.k lakini anasahau hata yeye aliacha kazi na kuingia kwenye siasa kutafuta masilahi bora ila kwakuwa ameshapata,basi nyinyi wengine shauri yenu.Ubinafsi!

Kuna mambo yanayohusu maisha ya watu ambayo yanapaswa kuwekwa wazi kisheria na kikatiba ambayo yatamfunga kila mwenye mamlaka kuyatekeleza na katiba au sheria inapaswa kutoa adhabu kali iwapo muhisika atayapuuza bila kujali nafasi yake maana sisi binadamu ni wabinafsi sana na zaidi tunasahau tulikotoka.

Nakumbuka tulisoma katika historia kuwa tulimkataa na kumlaani mkoloni kwa mambo mengi mojawapo likiwa ni kuwalipa wafanyakazi(watu weusi) ujira mdogo na kutowapa stahiki zao zingine kumbe na sisi tumerithi yale yale!!
 
JK 2006 nikiwa napata mshahara wa 98000 na posho kiasi Cha 31000 kwa mwezi. Lkn posho nilikuwa napikiwa chakula kwa lazima hata nisipokuwepo posho inakatwa.

Aliipandisha mpaka 157,000 kwa mwezi na posho ikawa 60,000/-

Kumbuka JK alikuwa mwanajeshi so alilelewa monduli vizuri hakuibuka tu.

Big up JK tunakutakutakia uzee mwema.

Ulijadili na wapinzani wako wa kisiasa mkatoka na soln.
 
Daah

Hakuna pesa hata wakulima wa Pamba wanakopwa na kile kiherehere cha TRA kutangaza makusanyo ya kodi kila mwezi hakipo tena maana ni AIBU TUPU!

Mtapandishiwa mwezi wa saba budget ijayo Miezi mitatu kabla ya uchaguzi ili mkasimamie na kupiga kura mnasikia eeee
 
Mzee baba ni adui wa wafanyakazi. Kila siku anahamisha magoli. Alianza kwa kusema hapandishi mshahara mpaka ahakiki wafanyakazi na kuwaondoa wafanyakazi hewa. Zoezi likaisha bila nyongeza. Akapeleka mbele magoli ili wafanyakazi tusifunge, akasema hawezi kuongeza mishahara wakat kuna stickers na sgr.. Eti tusubiri mpaka atakapokuwa anaondoka madarakan. Huku ni kukomoana tu. JK aliweza VP kuajiri kila mwaka, kulipa watumishi hewa na kuongeza mishahara kila mwaka na madaraja yakapanda?
 
tuweni nasubira watumishi wenzangu Raisi wetu anatupenda ataongeza mda ukifika miradi ni mingi, tumuunge mkono na kumpongeza
 
Huyu anakwapua hazina kujenga chato na matumizi mengine ya kipuuzi ambayo hayana vipaumbele vyovyote kwa Watanzania ikiwemo ulinzi wake utadhani yuko Uwanja wa vita.

Mzee baba ni adui wa wafanyakazi. Kila siku anahamisha magoli. Alianza kwa kusema hapandishi mshahara mpaka ahakiki wafanyakazi na kuwaondoa wafanyakazi hewa. Zoezi likaisha bila nyongeza. Akapeleka mbele magoli ili wafanyakazi tusifunge, akasema hawezi kuongeza mishahara wakat kuna stickers na sgr.. Eti tusubiri mpaka atakapokuwa anaondoka madarakan. Huku ni kukomoana tu. JK aliweza VP kuajiri kila mwaka, kulipa watumishi hewa na kuongeza mishahara kila mwaka na madaraja yakapanda?
 
JK 2006 nikiwa napata mshahara wa 98000 na posho kiasi Cha 31000 kwa mwezi. Lkn posho nilikuwa napikiwa chakula kwa lazima hata nisipokuwepo posho inakatwa.

Aliipandisha mpaka 157,000 kwa mwezi na posho ikawa 60,000/-

Kumbuka JK alikuwa mwanajeshi so alilelewa monduli vizuri hakuibuka tu.

Big up JK tunakutakutakia uzee mwema.

Ulijadili na wapinzani wako wa kisiasa mkatoka na soln.

ina maana kama aangeendelea kuongeza hata 50 kil mwaka,kwa sasa ungekuwa unapokea 375000/15000 posho.

bado ni mshahara duni sana,unajua wanasiasa wanatumia udhaifu wenu vibaya sana.

sasa hivi kila mtumishi akiongezwa 150k katika mshahara wake,ameshasahau msoto wote.
 
sisi tumerithi yale yale!!
Yaani tena sisi ndo wabaya kabisaaa! wana siasa walitutumia tu, kwa masrahi yao! Eti wanananilipa mshahara laki 4, jamani? nilikotoka 1000000/= hee! mbaya zaidi wamenikatia mshahara wenyewe! sababu nimenunua kigari
 
Back
Top Bottom