Mtu aliyekufa miaka 3 iliyopita ajitokeza na kukamatwa na Police | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu aliyekufa miaka 3 iliyopita ajitokeza na kukamatwa na Police

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shine, Feb 6, 2012.

 1. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mtu mmoja aliyekufa miaka 3 iliyopita huko Africa kusini ajitokeza na kudai amerudi rasmi. Ndugu na jamaa wanadai ni huyo ndugu yao aliyefariki lakini police wamechukua finga print na kudai niya jambazi waliyekuwa wakimtafuta na kuendelea kumshikilia kwaajili ya kumfanyia vipimo vya DNA na pia baada ya kujitokeza alikuwa akilala na mke wake na sasa ni mjamzito.
  Sourcd BBC
   
 2. twatwatwa

  twatwatwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 2,036
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hakufa huyo
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  nashawishka kukataa,.......
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  nani alihakikisha alikufa huko nyyuma?walimzika au alipotea tu
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  jambazi hilo limekimbiiia weeeee limechoka sasa na kurudi kuforge kifo
   
 6. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Eti alikufa, duhu!
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  amekua yesu mnazareti
   
 8. GIUSEPPE

  GIUSEPPE JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 4,489
  Likes Received: 4,503
  Trophy Points: 280
  Masuala ya "uchawi" na "ushirikina" yazua kizaa zaa Afrika Kusini!

  Mtu mmoja nchini humo anayedai kuwa ni mwanamuziki mashuhuri aliyekufa, anashikiliwa na mamlaka za nchi hiyo hadi watakapothibitisha utambulisho wake kwa vipimo vya DNA, wamesema polisi.

  Mtu huyo anasema yeye ni Khulekani "Mgqumeni" Khumalo - mwanamuziki wa nyimbo za kiasili za Kizulu ambaye alifariki mwaka 2009.

  Hata hivyo alizuka katika nyumba ya familia yake wiki iliyopita akidai kuwa alikuwa ametekwa na mizuka.

  Familia yake wakiwemo wake zake wawili, wanasema anaonekana kuwa ndio mwenyewe - lakini polisi wamesema atashtakiwa kwa udanganyifu iwapo vipimo vya DNA vitaonesha anadanganya.

  Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg, Nomsa Maseko amesema polisi wanatarajia kupata majibu ya vipimo vya DNA baadaye wiki hii - na mpaka wakati huo mtu huyo atasalia kizuizini.

  Mwandishi wa BBC anasema iwapo vipimo vya DNA vitaonesha kweli ni Bw Khumalo, polisi watalazimika kwenda mahakamani kupata kibali cha kufukua maiti, ili kujua nani hasa alizikwa, katika mazishi yaliyokuwa ya hali ya juu ya Bw Khumalo ambayo yalihudhuriwa na wanasiasa, vyombo vya habari na mashabiki wake.

  Kesi hiyo imezua kizazaa nchini Afrika Kusini - na siku ya Jumapili iliyopita, maelfu ya mashabiki walikwenda Kwazulu-Natal kushuhudia "kutolewa" rasmi kwa mtu huyo.

  Polisi walitumia maji yenye nguvu kutawanya watu baada ya msongamano kutokea kutokana na kila mtu kutaka kumuona mtu anayejiita Bw Khumalo.

  Aliwaambia mashabiki wake kuwa hakuwa amekufa - lakini alipotea baada ya kuchukuliwa na wachawi.

  Amesema alifungiwa katika pango na mizimu kwa miaka miwili, na alilazimishwa kuimba na kulazimika kula matope ili asife kwa njaa.

  "Nimekuwa hai muda wote," amekaririwa akisema na gazeti la The Times la Afrika Kusini.

  "Nimepoteza uzito mwingi lakini ni mimi," alisema.

  Mtu huyo, ambaye hakuwa na mtindo wa nywele wa rasta ambao Bw Khumalo alikuwa nao, alipuuza ombi la mashabiki la kumtaka aimbe, badala yake alitaja majina ya ukoo wake, kwa mujibu wa gazeti la The Times.

  Polisi wa Afrika Kusini wamesema wanashughulikia mkasa huo kwa kufanya upelelezi wa kesi ya uhalifu

  Source: wavuti.comĀ  - Blogu
   
 9. G

  G. Activist JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nashawishika alikufa, mbona Lazaro alifufuka....
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu unaambiwa alizikwa na majibu ya Dna ndo yanasubiriwa kutoa jibu kamili
   
 11. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ngugu zake pamoja na mkewe ambae sasa ni mjamzito aliyopeewa mume wake aliyefufuka
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndo maana hata mimi mwenyewe nimeshindwa ata kushangaa
   
Loading...