Mtu aliyebadili jinsia azua kizaazaa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtu aliyebadili jinsia azua kizaazaa Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JosM, May 18, 2009.

 1. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa ni mkazi mwa Mbezi Beach eneo la Makonde Juu /Kipongoso anajulikana kwa jina la ALLuh

  na Exuper Kachenje

  WAKAZI wa maeneo ya Mwananyamala wilayani Kinondoni jana walimiminika katika hospitali ya Mwananyamala, kutaka kumuona mgonjwa aliyelazwa ambaye anadaiwa kuwa alibadili jinsia yake na kuwa mwanamke.

  Imeelezwa kuwa mgonjwa huyo aliokotwa na polisi kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi jijini Dar es Salaam. Alikuwa hajitambui na habari zaidi zinasema kuwa alikuwa amebakwa.

  Habari za kuwepo katika hospitali hiyo mtu wa aina hiyo aliyewekewa viungo vya kike, zilianza kusambaa katika maeneo ya Mwananyamala na vitongoji vingine vya Jiji la Dar es salaam majira ya saa 4:00 asubuhi jana.

  Mwananchi ilifika hospitalini hapo saa 6:05 na kukuta watu wakisimuliana kuhusu mtu huyo huku wakionyesha kustaajabishwa na kushtushwa na habari hizo.

  ”Loh, dunia kweli imekwisha, wanasema ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni, tumesikia yupo mgonjwa wa aina hiyo amelazwa hapo wodi namba tatu, lakini tunazuiwa kumuona kazungushiwa pazia, ” alisema mmoja wa wakazi hao akimsimulia mwenzake.

  Ndani ya wodi namba tatu ambayo inashughulikia upasuaji na matatizo ya jinsia (Ward III Gyne and Surgical), kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakionekana kuwa na hamasa ya kumuona mtu huyo, ambaye Mwananchi ilidokezwa kuwa anaitwa Victoria.

  Alikuwa amelala kwenye kitanda ambacho kilizungushiwa pazia na kubandikwa tangazo linalozuia mtu kuingia ndani na kumwona.

  "Si ruhusa mtu yoyote kuinga katika chumba hiki,” lilisomeka tangazo lililobandikwa katika pazia.

  Mwananchi ilifanikiwa kumuona Victoria ambaye utaifa wake haukutambulika mara moja, lakini ni mtu mweupe na ambaye ametoboa masikio na nywele zikiwa za asili ya Kiasia.

  Habari za ndani kutoka hospitali hiyo zinasema kifuani Victoria ana matiti makubwa ambayo muuguzi mmoja alidokeza kuwa yanaonekana kuwa ya kutengeneza kwa sindano.

  Alisema nia ya kuzungushia pazia kitanda chake ni kuzuia watu wasiendelee kumshangaa na pia kuwaondolea hofu wagonjwa wengine ambao ni wanawake waliolazwa wodi hiyo.

  Habari zaidi zinasema kuwa ingawa Victoria hajaweza kuzungumza, hali yake imeanza kuwa nzuri na ameanza kupata fahamu kwa kufumbua macho na awaonapo wanaume huwafurahia zaidi kuliko wanawake.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa Victoria alifikishwa hospitalini hapo saa 11:00 alfajiri jana na polisi baada ya kuokotwa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi akiwa hajitambui na inahisiwa alibakwa na watu wasiojulikana.

  “Hii ni Police case (suala la kipolisi), aliletwa na polisi sikumbuki wa kituo gani” kilisema chanzo cha habari hospitalini hapo.

  “Inavyoonekana Victoria alifanyiwa uhuni, watu walimbaka na kumtelekeza ufukweni. Nadhani maeneo ya Mbezi Beach kuna matatizo... waandishi fuatilieni, hii ni mara ya pili. Kuna wakati aliokotwa mtu katika kali hiyo maeneo hayo akaletwa hapa na alikufa hakuwa na ndugu.”

  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, mganga mkuu wa hospitali ya Mwananyamala, Dk Suleiman Mtani alisema anachojua yeye aliyepokelewa ni mgonjwa kama wengine na wajibu wao ni kumpatia huduma inayostahili.

  “Ni kweli kuna mgonjwa amepokelewa leo alfajiri, akiwa hajitambui, mpaka muda huu hajaweza kuzungumza. Lakini ninachoweza kuwaambia ni kuwa amepokelewa kama wagonjwa wengine na jukumu letu ni kumsaidia kwa kumpatia matibabu si kutoa taarifa zake,” alisema Dk. Mtani.

  “Maadili ya kazi yetu, ni kulinda utu na heshima ya mgonjwa, madaktari hawatoi taarifa za mgonjwa kwa mtu asiyehusika. Tafadhali naomba tuzingatie hilo, ni kiapo cha kazi yetu.”

  Hata hivyo alisema kama ni kupata taarifa kamili za mgonjwa huyo polisi ndiyo inaweza kuwa nazo kwani ndiyo iliyomfikisha hospitalini hapo na kuwa hakuna taarifa zake zaidi kwa sababu hawezi kuongea pia hadi jana mchana ndugu zake hawajajitokeza.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye alisema: “Nipo nje ya Dar es Salaam, mtafute kaimu wangu afande Damas Masinde.”

  Alipotafutwa, Masinde alithibitisha kuokotwa kwa mtu huyo, lakini akasema uchunguzi unaendelea kujua nini kilimpata.

  “Askari wetu wa kituo cha Kawe walimwokota mtu huyo na kumpeleka Hospitali ya Mwanayamala. Ngoja nikwambie ukweli ndugu yangu, mchana nimemtuma mkuu wa upelelezi kwenda pale kujua zaidi habari za mtu huyo, lakini kwa kuwa bado hajapata fahamu madaktari na manesi hawakumruhusu kumuona,” alisema Masinde.

  Alifafanua kwamba askari wake wanaendelea kufuatilia na atakapopata nafuu atafanyiwa uchunguzi na taarifa itatolewa.

  “Hatuna uhakika amepatwa na nini. Tunaendelea kufuatilia tukipata ukweli tutatoa taarifa. Kwa sasa siwezi kusema lolote,” alisema afande Masinde.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sa sijui tumwite he/she? Inanikanganya!

  To me -no wonder, he/she is simply paying for the actions of his/her own decision, and he/she has got none to blame.!

  Ni mpumbavu flani tu, ambaye hajapata kujipenda maishani mwake, then how would he/she expect the 3rd parties to love or feel pitty on him/her?

  He/she has chosen a way of life, acha ailipie.
  Tchao!
   
 3. Y

  YesSir Senior Member

  #3
  May 18, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duhhhhhhhh
   
 4. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pia huyu jamaa ana kaka yake kwa sasa yupo nje ya nchi nae ni shoga, zamani alikuwa anafanya kazi NEW AFRICA HOTEL,wana asili ya kiasia.ukifanikiwa kumwona unaweza dhania kuwa ni mwanamke kumbe ni dume lililo jigeuza jike.
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mmmmh!!!....Makubwa!!!
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  ahha, kinyaaa sana.
  mijitu mingine bwana,
  basi tu, ''akiona wanaume anafurahi kuliko wanawake'' MAKUBWA!!!!
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Nakwambia mishoga yote itaabika tuu. Sijui kwa nini mbwa naye hakwenda kummaliza kama yule wa shoga wa Mbezi beach aliyezikwa wiki iliyopita!!! Halafu wanatumia beach zetu vibaya. Kama ni uchafu wao wa kupakuana si waende guest house!??? Shame.
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Jamani, huyu siyo yule Aloo aliyewahi kuandikwa sana na gazeti moja katika miaka ya 90 -- nadhani Family Mirror -- shoga ambaye aliwahi kuoa Mjapani, akazaa naye na baadaye mkewe alimkimbia alipogundua kumbe ni 'mwanamke' mwenzake? Alikuwa anaishi maeneo hayo hayo ya Mbezi Beach.

  Ni mwembamba mwenye asili ya kisomali au Kiburushi au Kishihiri. lakini kama ni huyo, miaka hii ya sasa atakuwa umri wake umekuwa mkubwa.

  Sikumbuki vizuri, lakini mwenye kumbukumbu tunaomba atumwagie habari za huyu.
   
 9. k

  kapuchi Senior Member

  #9
  May 19, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  wadau

  nimepata habari kupitia magazeti mbali mbali ya leo kuwa yule jamaa aliyebadili jinsia zake, na kukutwa ametupwa na polisi kwenye fukwe zabahari ya hindi huku akiwa amebakwa na watu wasiojulikana,hali yake bado ni tete.

  sasa mimi nashindwa kuelewa hiyo hali inatokana na kufanyiwa vibaya na hao wabakaji au inawezekana alinywesha kitu kibaya.
   
 10. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Katika magazeti ya leo wanasema amehanishiwa Muhimbili ICU na wanasema jinalake sombody Abdallah alikuwa na nyumba mbezi beach akaiuza na pesa yake ndio aliokwenda kufanyiwa hiyo operation ya kujibadilisha jinsia zake.
   
 11. k

  kapuchi Senior Member

  #11
  May 19, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  unajua mimi bado nashindwa kuelewa ni namna gani mtu anabadilisha jinsia kutoka ya kiume kuwa ya kike?ile jinsia ya awali inakatwa na nyingine inatengezwa kwa plastic na kubandikwa au inakuwaje jamani

  hebu mwenye uelewa wa ziada atusaidie.
   
 12. dmaujanja1

  dmaujanja1 JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  KAPUCHI naomba kuongezea hapo kwako je utamtambuaje kuwa kabadili Jinsia?
  nA Je anazo bidhaa ngapi? na ile bidhaa ya kiume kama inabaki wanaIdisable au zote zina perform duty at per.
  Please mwenye uelewa anisaidie hapa.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Ndiye yeye Aloo Abdalah, alikuwa benet sana na Asia Idarus. Alikuwa akishinda Zanzibar Hotel na Amina Msomali.
  Jamaa aliwin maisha, akanunuliwa nyumba Mbezi beach, akaiuza akaenda ulaya na kurudi Mwanamke. Kwa sasa
  Amepanga Mbezi Beach na yuko kwenye hatua za mwisho kufungua bonge la night club hapo hapo anapoishi.

  Ukweli wa kilichomsibu inadaiwa amekunywa dawa ambazo zimereact na hormone change yake. Kisa chote kimetokea akiwa home alipopanga kwa sasa.

  Hii habari ya kuokotwa beach ni deal ya mwenye nyumba akiamini jamaa atavuta, hivyo kumdhulumu kila kitu.
  Baada ya kuzidiwa Baba mwenye nyumba alipiga simu polisi na ni defender ya polisi ndio iliyomfuata na kumchukulia toka home kwake mpaka hospitali.
  Hii story ya kukutwa beach ni deal ya polisi na mwenyenyumba huku wakiombea mchezo uishe wamkombe kila kitu kwa sababu ndugu zake walishamsusa.
   
 14. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Huyo mgonjwa bwana vijana walitaka kutest...aliliwa timing kitambo maana kulikuwa na redio za mbao kuwa bibi she-male na amekewa cha chini. Basi wakamtia mikono akashughulikiwa hadi wachana ile kitu iliyowekwa na nyuzi zake, Ngoma ikawa nyeupe watu wakala kona.

  Jamani, watoto wa uswahili bwana wanaweza kufa hivi hivi kwa kuonja visivyolika. Haya ngoja tuendelee kupata zaidi kwa wambeya. Afu bongo kweli noma yaani pale kuna watu hawataki kutoka kabisa pale Mwananyamala eti hadi wamuone huyo dume jike. Asa sijui wapate nini?
   
 15. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  hueleweki......
   
 16. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #16
  May 20, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33


  ,,,Yaani kama nayaona majitu yalivyo toa mimacho hapo nje ya hio ward,kiumbe kimehamia MUHIMBILI sasa,hali bado tete.
   
 17. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ni kweli atakuwa huyu jamaa. Huyu jamaa asili yake ni Kilimanjaro na Arusha. Yeye anavyodai ni chotara wa kihindi na Kiarabu. Aloo ama Anti Alu alianza mambo haya akiwa baharia miaka ya 80. Na inasemekana baada ya hapo alipata kuishi na Giriki moja lililomfanya mkewe. Baada ya Giriki hilo kuondoka akamwacha jamaa na kumwachia na nyumba maeneo ya Mbezi Beach. Jamaa amekubuhu na masuala ya ushoga. Na alikkwishawahi kukamatwa na Polisi kwa tuhuma ya kuwashawishi wanafunzi wa Makongo Sekondari kufanya vitendo vya kishoga. Mpaka tunavyoongea amekwishatengwa na familia yake. Alikuwa akipendelea sana kufuatana na aliyekuwa mke wa Salmin Amour aliyepata kuwa Rais wa Zanzibar lakini akaachika Salma Amour. Haieleweki mahusiano yao lakini mama huyo alikuwa akidai ni dereva wake. Jamaa anafahamiana na watu wengi sana serikalini na ni ushahidi tosha hata baadhi yao wanafanya mambo ya kishoga. Huyu Aloo kwa mfano anafahamiana sana na Jamaa mmoja ambaye anaitwa Abuu Cisco Mtiro ambaye ni balozi wa Tanzania mahali fulani nadhani. Natarajia wako wengi wanaomfahamu jamaa huyu. Ila ubaharia na pia alikuwa na sura nzuri kweli ya kike wenzake labda walimtamani. Shoga mwingine ambaye wanamtaja taja sana anaitwa KIBO MAREALLE naye ni wa huko huko Mbezi Beach. Samahani Moderators lakini huo ndio ukweli wenyewe. Ni lazima tuupige vita ushoga na tuulaani kwa nguvu zote.
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hakuwa baharia bali mfanyakazi wa kwenye ndege ( steward) ATC.
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  Hii inasikitisha sana. Hata hao ndugu zake kama wamemsuta nayo si nzuri sana. Undugu huchagui ila unazaliwa. Inabidi waje wamsaidie ndugu yao na akipona, wanaweza kumuacha aendeleee mwenyewe na biashara yake.

  Huyu Polisi na baba mwenye nyumba inabidi washitakiwe kwa kosa la kumuacha mtu bila msaada na au hata kumpeleka Beach ili afie huko na wao wakombe hela zake. Baniani mbaya...... washenzi hawa.

  Hata kama ni SHOGA, mwisho wa siku jamaa ni Binadamu. Mie nashindwa kuelewa watu wanaopiga kelele hapa. Jamaa na mwili wake, wee inakusumbua nini? Kama alikuwa akirubuni watoto wa Makongo, ilitakiwa ashtakiwe na aadhibiwe kwa hilo. Ila kama ni watu wazima, hiyo si biashara yetu.

  Mwisho najiuliza hapa kitu kimoja. Hivi jamaa akifungua hiyo club yake, na mtu akupatie tenda ya kuwa una suply kwake nyama, mayai, mboga, nk na kwa mwezi unatengeneza kama Tsh 3M, utakataa eti kwa sbabu jamaa ni shoga au utachangamkia tenda??
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  ...alitaka kujiua kwa sababu ya mapenzi - kufuatana na ujumbe aliouandika kabla hajanywa sumu!
   
Loading...