#COVID19 Mtu akisema tahadhari dhidi ya Uviko-19 ni kukosa Imani

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,726
5,442
Ameandika Pastor Dr.Zakayo Nzogere (PhD), Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la MICC Mwanza.

Pamekuwa na matamko mengi yanayokinzana kutoka kwa watumishi wa Mungu kuhusu UVIKO19.
Wapo wanaosema ni maandalizi ya “Mpinga Kristo” na alama ya Mnyama 666; na wengine wakisema ni mlipuko wa kawaida usio na uhusiano wowote wa kiimani.

USHAURI WANGU KWA WATUMISHI WENZANGU;
1. Kuwa Mtumishi wa Mungu haimaanishi tuna majibu ya kila jambo kila wakati.

2. Kuwa Mtumishi wa Mungu haimaanishi kila unachokiamini, unachokisema, au kukifiria basi kimetoka kwa Mungu. Mambo mengine ni utashi binafsi unaotokana na taarifa ulizonazo.

3. Kuwa Mtumishi wa Mungu haikupi mamlaka ya kuwafanyia wafuasi wako maamuzi binafsi. Hata Mungu mwenyewe anatutaka tuchague kati ya uzima na mauti; hatulazimishi (Kumbukumbu 30:19).

4. Kuchukua tahadhari siyo kukosa Imani. Kuna wakati Yesu alichukua tahadhari ya kutoingia Yerusalemu waziwazi kwa sababu kuna watu walitaka kumuua; hivyo akaingia kwa siri (Yohana 7:1-10). Si kwamba aliogopa kufa; bali hakutaka kufa kabla ya kutimiza kazi iliyomleta.

Wayahudi walipotaka kumuua Mtume Paulo alitoroshwa mjini kwa kushushwa na KAPU (Matendo 9:25); hebu fikiria Mtumishi wa Mungu kujificha kwenye kapu.

5. Ni sahihi Mtumishi wa Mungu kuwa na msimamo binafsi kuhusu mambo tofauti, lakini si sahihi KUMUINGIZA MUNGU kwenye misimamo binafsi.

Mtume Paulo anatusaidia kwenye kutoa matamko ambayo sio maagizo ya Mungu moja kwa moja, kwa kuweka wazi mara zote anapotoa mtazamo binafsi juu ya jambo fulani:

1Korintho 7:6 (NEN) “Nasema haya kama ushauri na si amri”

1Korintho 7:12 (NEN) “Lakini kwa wengine nasema (si Bwana ila mimi)..”

MIMI NAAMINI YAFUATAYO:

1. Covid19 ni janga la
kawaida na litapita.

2. Chanjo ya Covid haina athari zozote za kiroho kwa Mkristo.

3. Hakuna kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu wala kugeuza imani yetu.

4. Ni sahihi Wakristo kuchukua tahadhari zote za kiafya kama tunavyoelekezwa na wataalamu.

NB: Mtu akisema tahadhari dhidi ya UVIKO ni kukosa Imani; muulize kwanini anafunga mkanda kwenye gari? Kwanini anavaa kofia ngumu kwenye pikipiki? Au kwanini ameweka chandarua chumbani? Zote hizo ni tahadhari, sio ukosefu wa imani.!
 
Waacheni wananchi wachague maana ni suala la HIARI sio LAZIMA! mbona simple tu

Wakuchanjwa kachanjwe, usiyetaka kuchanjwa usichanjwe... Case closed!
 
Back
Top Bottom