Mtu akiandika hivi huwa najisikia hasira

kibangubangu

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
212
285
Kiswahili ni lugha tamu sana, ila pale mtu anapoanza kuiharibu inatia hasira sana. Kwa mfano, pale watu wanaposema maneno yafuatayo:

"Abali yako we kaka"
"Wewe hujui dhamani ya moyo wangu ndo maana unanitesa"
"Nikiwa laisi nitaenda kukaa Ikuru"
"Hajila hazijatoka bado"

Hebu weka na wewe baadhi ya maneno yanayokukera na kukuongezea msongo wa mawazo.

Maoni yaliyotolewa na wadau:
kibangubangu, Yaani mimi nikishaona tu uandishi kama huu tu ghafla akili yangu huwa inam-undermine na kumchukulia kama mtu ambaye hakwenda shule au ambaye hajaelimika!! Hata kama umeandika content nzito kiasi gani.

Mfano unakuta mpaka maneno ya kingereza tu mtu anachanganya L & R

Mfano.:
Flash :utasikia frash (kweli kabisa )
Fresh :eti flesh
Ready: ledi. etc

Yaani hili ni janga la taifa

Mimi nahisi east africa nzima sisi wabongo ndo tunaongoza kwa kiswahili kibovu.

Bahati mbaya fani yangu sio ya ualimu tena yale masomo ya kuandika essay maana hata kama umeandika vizuri kiasi gani ila kuna makosa ya aina hiyo ni kukosesha tu maana hii ni kuuwa elimu
Huwezi kucompete kwenye somo la kiswahili kwa nchi ambazo wanahitaji kujifunza kwa mtindo huu, majirani zetu wataendelea kupata hiyo contract tu.
 
Wapo wengi sana

Ukiona hivi ujue hawasomagi magazeti kwa asilimia kubwa, waandishi wa magazeti ni msaada mkubwa sana kuweka Kiswahili vizuri

Na Waalimu wa zamani walikuwa wapenzi wakubwa wa kusoma magazeti

Sasa mtu atakuaje maneno sahihi wakati yuko busy kuchat na Mshikaji na Msela pamoja na youtube?
 
yani sipendi mtu anayetumia maneno "208", "lewo", "7babu" "ni mhimu xana". Yani uozo mtupu.
 
ndalibanza,
"208"

Inatamkwa kama namba yenyewe kamili? Au wahusika uliyowakusudia wana maanisha nini?

Nitoe ushamba kidogo.
 
Ukute ni mpenzi wako anakuandikia meseji ya mahaba kisha anakosea kosea hivyo, tena ni Kiswahili, hata kama unampenda, dah
Wengine wanaandika herufi kubwa tupu halafu hawajui kuweka nafasi kati ya neno na neno

Anakuandikia RAAZIZ.AILINI..URIPATA.SARAM.NIRIZOMTUMA.MELI

Akaanisha Laaziz Irene ulipata salamu nilizimtuma Mary?
 
Baada ya watoto kuanza kutumia mitandao ya kijamii pamoja na simu imekuwa vurugu mechi
Hawataki mambo mengi wanataka shortcut kwenye kuandika ujumbe kwa muandikiwa
 
Back
Top Bottom