Mtu adaiwa kufufuka-Nipashe

Kitia

JF-Expert Member
Dec 2, 2006
418
73
Mtu adaiwa kufufuka

2008-07-28 09:22:01
Na Patrick Chambo, PST Hai

Mamia ya wananchi katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameshikwa na butwaa baada ya kumuona msichana aliyedaiwa kufariki dunia takriban miaka mitatu iliyopita akiranda randa mitaani.

Tukio hilo la aina yake, lilitokea katika kijiji cha Machame Mkuu, mkoani Kilimanjaro na msichana huyo anayedaiwa kufa na baadaye kukutwa akitembea mitaani ametajwa kuwa ni Neema Mushi, mkazi wa kijiji hicho.

Aidha, habari zilizopatikana kijijini hapo zilisema kuwa, binti huyo alisema kuwa alikuwa akiishi Tanga.

Mchungaji Elimfoo Mushi wa Usharika wa Machame Mkuu, alisema ndiye aliyeendesha ibada ya kumuombea Neema ambaye mwili wake ulifikishwa kanisani hapo.

Akizungumza na PST, Neema alisema kuwa kweli hilo ni jina lake, lakini alikanusha kuwa alikufa na kuzikwa na badala yake alikuwa akiishi Tanga.

Alisema eneo alilokuwa akiishi ni siri yake na kwamba akiwa huko alisikia kuwa alikufa na kuzikwa mwaka 2005.

``Mimi sijui kitu, najua nilikuwa naishi Tanga �na wala siwaambii nilikokuwa naishi. Nimeshangaa narudi watu wanakimbia hadi nilipopelekwa polisi, wakaja ndugu zangu wakanitambua kuwa eti mimi nilikuwa marehemu,`` alisema.

Shangazi wa Neema, Bi. Liliani Mushi, alisema ndiye aliyemuuguza Neema hadi umauti unamfika na kusafirisha mwili wake hadi kijijini hapo na kuzikwa kwenye makaburi ya kanisa.

``Kweli mimi nimeokoka na sali Kanisa la Ephata, huyo mtoto alinifia mikononi huko Namanga nilikokuwa naishi naye nimeshangaa kuambiwa eti njoo umuone Neema, amekuja Machame kutoka Tanga, nilichoka, hakika huu ni muujiza wa Mungu watu wanasema kuwa eti ni msukule, mimi siamini, ninachojua alinifia tukamzika. Huyu hapa muulizeni wenyewe katoka wapi,`` alisema shangazi huyo.

Naye Mchungaji Mushi alisema, ``nasema nijuacho mimi ni kuwa huyu ndiye Neema ambaye mwili wake uliletwa hapa kanisani na tukauzika makaburini, kwamba ni muujiza wa Mungu au msukule, mimi sijui,`` alisema.

Polisi wilayani Hai, wamekiri kuchukua maelezo ya Neema, wazazi, Mchungaji na ndugu wengine walioshiriki katika mazishi.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa mkoa Bw. Lucas Ng\'ohoko, hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo.

Aidha, ndugu na jamaa wa Neema wako kwenye harakati za kupata kibali cha polisi ili waweze kufukua kaburi hilo.

* SOURCE: Nipashe
 
Naomba wana jf waliojirani na huko Hai wafuatilie hili swala mpaka tujue ukweli wake
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom