Mtozi Alloyce Nyanda: Kuna watu wanamtumia Swai kumchafua Sabaya?

Angalia alichokuwa anawafanyia wafanyabiashara,
 
Kwa hiyo DC aligeuka Afisa TRA akawa naye anakusanya mapato ya serikali?

Task Force!
 
Ndugu yangu ukitaka kumtetea sabaya utaishia kuchafuka mwenyewe. Hata umtoe swai katika masuala aliyowahi kufanya sabaya ni mengi. Muulize nandy alichofanyiwa pale weruweru mountain lodge usiku sabaya akiwa na genge lake.
Nandy yupi mkuu
 
Anaandika Mtozi Alloyce Nyanda

Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson

Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.

1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?

2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?

3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!

4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?

6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?

Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?

Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
Nyanda mjinga sana najua kapewa hela na sabaya kumtetea mjinga mwenzake sabaya,mwizi,tapele mporaji nk siku zake zinahesabika mungu atajibu maombi ya wanyonge.
 
Tukitawala na kutoa maamuzi kwa mitandao hatutafika. Nadhani taifa letun haliwezi chukua mambo ya mitandaoni kutolea maamuzi. Tuache kazi zisonge mbele.
 
Aisee mpaka nimesisimka ...ajabu huyu mtu atatumbuliwa tu na hakuna atakachofanya CCM wanalindana sana yani Mbwa hao.
Hivi Sabaya ana chafuliwa au Sabaya ni mchafu?? /kuna gani la uongo Swai kasema kuhusu Sabaya?
Kama Sabays kakutuma umekosea kuandika hapa. Huu ujumbe unge mpelekea mkewe kama anae. Sisi tunao mjua Sabaya hatuhitaji kuelezwa kwa ana chafuliwa. Maana Sabaya si mchafu tuu bali ni jambazi na muuaji.
VIDEO YA CCTV CAMERA IKIMUONYESHA MKUU WA WILAYA YA HAI AKITESA MTU NA WATU WAKE.

Diwani Msangi wa Sombetini afunguka juu ya kipigo alichopewa na Sabaya
Philip Kana
4th April 2021

DIWANI wa Kata ya Sombetini, Jiji la Arusha, Bakari Msangi, amefunguka namna alivyoshambuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akiwa na walinzi binafsi.

Anadai kwamba Sabaya wakati akimshamblia, alikuwa na walinzi wake binafsi sita waliobeba silaha ikiwamo bastola mbili.

Diwani huyo ameiambia SAUTI KUBWA kwamba ameamua kuyasema hayo baada ya Sabaya na wapambe wake kusambaza taarifa kuwa Februari 9, mwaka huu, alipigwa na baaadhi ya watu baada ya kumfumania “akiwa na mke wa mtu.”

Msangi akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa anasema, Februari 9, mwaka huu majira ya saa 11 jioni alipokea simu kutoka kwa Mohamed Asaad, akimweleza kuwa mkuu huyo wa wilaya amevamia dukani kwake, hivyo kama anafahamiana naye anaomba akamsikilize na kumsaidia. Assad ni mmiliki wa duka la mapazia la Shaahidi Storea lililopo Barabara ya Nyamwezi karibu na Soko Kuu jijini Arusha.

Msangi anasema: “Mimi nikaenda pale dukani nikakuta mlango wa chuma umefungwa nikagonga hawakufungua, nikaamua kuuvuta juu nikaingia. Kweli nikamkuta Sabaya na vijana wake sita wamewaweka chini ya ulinzi wafanyakazi na wateja waliokuwa kwenye hilo duka, wanawapiga,” anasema Msangi na kuongeza.

“Nikamuuliza Sabaya kuna shida gani? Akaniambia hawa Waarabu ni wahujumu uchumi, wanafanya biashara haramu wanauza dola feki, wanauza bidhaa hawatoi risiti, akaniorodhesha makosa kibao…

“Nikamwambia mimi kama diwani wajibu wangu ni kuwatetea wananchi wa Arusha, lakini wewe hapo ulipo siyo TRA, (Mamlaka ya Mapato Tanzania), siyo Takukuru wala Usalama wa Taifam na siyo polisi, iweje uwanyanyase hawa badala ya kutumia vyombo husika vikaja kuwakamata hawa watu?”

Msangi anasema kuwa kauli hiyo ilionekana kumuudhi Sabaya ambaye bila simile alimgeukia na kuanza kumshushia kipigo.

“Aliwaamuru vijana wake waninyang’anye simu zangu, wakachukua na fedha walizonikuta nazo kama laki tatu na elfu tisini, wakanipiga vibao wakanikalisha chini,” anasema Msangi na kuongeza.

“Walipokuwa wananikalisha, niligoma, wakaamua kunifunga pingu mikononi. Wakaanza kunipiga, nikamwambia Sabaya haki ya Mungu mtaniua, lakini sitaondoka hapa mpaka nisimamie haki ya hawa watu.

“Wakati haya yakiendelea, Sabaya alimchukua mdogo wa mwenye duka na kuingia naye chumba kingine ambako walikuwa wakizungumza. Baadaye nikagundua kuwa alikuwa akimuamuru ampigie simu kaka yake, Asaad ili aje dukani kwake…”

Diwani huyo anasema kuwa iIlipofika saa tatu usiku alimwambia Sabaya awaache, lakini aligoma na baadaye kuwapiga vibao wateja waliokuwamo ndani ya duka na wadogo wa Asaad, kisha aliwaambia waondoke.

“Sabaya akapiga simu kwa OC CID akamwambia kuna watu nimewakamata ni wahujumu uchumi nataka kuwaleta hapo polisi. Wale ndugu zake Assad wawili wakaingizwa kwenye gari la walinzi aliokuwa nao – mabaunsa, mimi nikaingizwa kwenye gari alilokuwa amepanda Sabaya…

(Sabaya)
“Msafara ukaanza kuelekea Central, tulipofika tukamkuta OC CID, Gwakisa kasimama nje anatusubiri na mimi nikataka kushuka, lakini Sabaya akanizuia.”

Diwani Msangi anasema Sabaya alimwambia hajamshusha polisi kwa sababu hajamaliza kazi naye, anataka akamuonyeshe nyumbani kwa Ally Assad Ajirin na kwa kaka yake Mohamed Assad Ajirin. Anazidi kusimulia:

“Tukaenda kwa Ally Assad Ajirin, tukafika tukagonga mlango hawakufungua. Kidogo wakati tunatoka, tukakutana na mzee mmoja anaongea na simu akajua labda ni mzee wa familia hiyo akamkamata baadaye akamuacha” anasema Msangi na kuongeza.

“Tukaondoka tukaenda kwa Mohamed Assad tulipofika akavunja mlango akaingia ndani akawaluta mke wa Mohamed na watoto. Hawakumkuta Mohamed, hivyo tukaondoka.

“Tukatoka tukazunguka mjini mimi nikiwa nimefungwa pingu. Baadaye wakaenda supermarket ya Panone pale Ngarenaro wakanunua vinywaji wakawa wanakunywa, kisha tukaondoka mpaka pale Hoteli ya Tulia, iko pale WhiteRose,”.

“Tulipofika hapo wakaingia ndani wakaniacha mimi kwenye gari wakawa kama wamenisahau. Palepale nikaona mfuko waliokuwa wameweka simu, nikavivuta nikafanikiwa kuchukua simu.

“Simu kubwa nikaiicha ndani ya chupi nyingine ndogo nikaitumia kumpigia mke wangu. Nikamwambia yote yaliyonikuta, nikamwambia anifuate ila aje na jirani yetu hapo nyumbani.

“Baadaye kidogo, Sabaya akatoka akiwa kabadili nguo, mwanzo alikuwa kavaa kaunda suti sasa ametoka kavaa koti, akaja kwenye gari akaniambia nasikia kuwa watu wanakutafuta ni nani, nikamwambia sijui…

“Sabaya akasema itakuwa ana simu huyu embu mpigeni ‘teru’ (mkagueni). Walinikagua, lakini walishindwa kuziona kwa sababu zilikuwa ndani ya suruali.

“Sabaya alimuona mke wangu eneo lile, jirani na gari lake, akahoji akisema ‘huyu malaya anayekufuatilia ni nani?’

“Akawa anawaagiza mabaunsa wake waende wakamchukue, nikawaambia mtamchukuaje mke wangu, baadaye nikaamuriwa kwenda kuzungumza naye nikiwa chini ya ulinzi…

“Sabaya akaja akamtolea mke wangu bastola akamwambia leo naenda kumuua Bakari. Mke wangu akapiga ukunga, Sabaya akaona kuna shida, lakini mimi nikamwambia mke wangu asiwe na wasiwasi kwani hapo walipofika hawezi kufanya chochote nikamwambia akanisubiri Arusha Technical …

“Mabaunsa wakaniingiza kwenye gari tukaondoka tulipofika pale Petrol Station ya Mount Meru, kabla ya taa za barabarani, wakasimamisha gari wakaniambia nishuke nikimbie. Nikagoma, wao wako na bunduki na bastola nakimbia vipi? Wangeweza kunipiga risasi nikawaambia wanipeleke mahali mke wangu yupo…

“Wakaenda wakanishusha pale Arusha Technical ambapo mke wangu alikuwa wakanipiga mkwara. Nikaondoka kufika nyumbani ndiyo nikaanza kusikia maumivu, nikawapigia viongozi wenzangu sikuwapata ….

“Nikaamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa, Iddi Kimanta nikamweleza kila kitu, yule mzee alilia kabisa wakati naongea naye. Akawapigia RPC na OCD akawaeleza kisha akaniambia tukutane Polisi, nilipofika nikawakuta viongozi wamejaa …

“Ilikuwa saa sita usiku, wakaniandikia PF3 nikaenda hospitali kutibiwa, hivi napokwambia naendelea na matibabu na polisi wako kwenye uchunguzi.”

Diwani huyo alisema kuwa hakuweza kutambua namba za gari alilokuwa akitumia Sabaya kwani wakati wakitoka dukani kwa Assad alikuwa ameweka namna za DFP na walipokuwa wakitoka hoteli ya tulia alikuwa amebandika namna za UN.

Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, James Ruge alisema endapo tukio hilo lilitokea, halina uhusiano na taasisi anayoiongoza, na kubainisha kuwa “hiyo ni jinai.”

Sabaya hakujibu simu za mwandishi wetu wala ujumbe mfupi wa simu uliomtaka azungumzir sakata hili na tuhuma hizi.
 
Huyo anayemtete Sabaya itakua ni Sabaya mwenyewe au itakua sabaya anamnanihii
Sasa mimi kwa macho yangu nimemuona Sabaya anakuja Arusha na msafara wa wapambe na mademu wa chuo na walinzi wamebeba bunduki SMG huku wamevaa maspy koti, na chimbo lake alilokuwa anapenda Ni Hotel ya Point Zone pale mianzini,swali anakuja na mabunduki kila siku arusha kufanya nini na sio eneo lake la kazi? Pili Sabaya ana rekodi anaingia Bar anakula,anakunywa na wapambe wake zaidi ya 10 na walinzi wake, ikifika muda wa kulipa bill anajifanya "amepigiwa simu na muheshimiwa", anaingia kwenye gari anaondoka. Amesababisha wahudumu wengi sana kukatwa mishahara yao ili kulipia bill za Sabaya na wapambe wake. Tatu, uliza maduka ya Arusha hasa ya electronics yaliyopo stand ndogo, Sabaya anaenda anachukua Tv hadi za million 3 anasema atakuja kulipa,akipigiwa simu kukumbushwa deni hapokei simu. Jambo linanishangaza unapata wapi ujasiri wa kumtetea mtu muovu kama huyo? Sisi tunamjua personal, sio mambo ya kuhadithiwa na mtu. Amerusha pesa watu wengi sana, ametesa watu wengi sana.Mama Samia asipomshugulikia, MUNGU atamshugulikia.
 
Sabaya akitoka madarakani lazima akimbie Hai vinginevyo atafanywa kitu mbaya sana.
Mambo ya Sabaya husituletee hapa,huyo siku zake zishafika mwisho tangu siku ya kwanza tu alivyoapisha SSH.
Kwahiyo hakuna namna ya kumuepusha kikombe hiko.
 
SIASA ZA HAI HUWA HAZIISHI.

Kuna clip za jamaa mmoja zinasambaa anaitwa Cathberth yeye kaamua kufa na Ole Sabaya. Ukimsikiliza jamaa utaona Siasa Professional inayofanyikaga hai. Na inavyoonekana jamaa Kuna watu wamemuweka tu front. Hii issue yake na Sabaya imekaa kisiasa sana na lengo kubwa hapa ni kumu- influence Mama Samia afanye maamuzi wanayotaka yaani Kama wanampangia mama kazi

Kwa Hai bado Siasa za uchaguzi wa 2020 haujaisha. Nakumbuka hili eneo ambalo huyu jamaa analilalamikia liliwahi kuwa na mgogoro mkubwa tu Kati yake na Bibi mmoja ambaye anadai eneo Hilo ni lake. Ngoja nikuwekee link ujikumbushe kidogo.-

Huyu Bibi ali- Trend Sana na baadhi ya watu wakadai amehongwa yule Bibi anayeitwa Chalii ya Arusha baadaye kwa juhudi za Milard Ayo wakakutanishwa Bibi anayedai kudhulumiwa shamba na Bibi anayeitwa Chalii ya Arusha. Link ifuatayo inakupa ukweli wote walipokutwanishwa:-

Ni kweli kuwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kumekuwa na mbanano katika ukusanyaji wa Kodi na wengi aidha wameumia. Lakini mbanano huo umeifanya Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwenye makusanyo ya Kodi na ya Sita Kitaifa.

Haya anayoyalalamikia Cathberth ni mfumo sio Mtu. Haya anayoyalalamikia kila mfanyabiashara analalamikia. Task force za kudai Kodi zipo nchi nzima na wengi wamedaiwa hivyo na wengine ni kweli wamefilisika.

Ndio maana naona Siasa nyuma ya hili Jambo.

Tuchukulie Mfano Akhsante Tours ipo Manispaa ya Moshi lakini Juzi Juzi imepigwa mnada na CRDB kwa nini asilalamikie Hilo?

Kwenye video nyingine anadai amejificha Jipe kweli Jipe ni mahali pa Kujificha? Kwamba hao maadui zake wanashindwa kufika Jipe?

Kinachofanyika Sasa ni Sabaya aondolewe Hai. Hii ndio agenda not otherwise na huenda akafanikiwa.

Siasa za Hai huwa haziishi Kirahisi...... hii ndio Siasa Professional na kwa jicho la kawaida huwezi kuona.

Kwa kuwa kuna ahueni Kidogo kwa wafanyabiashara kutokana na kauli ya Mama Samia Cathberth aache kubeba watu mgongoni arudi kwenye game ya biashara afanye biashara mambo yasonge. Huu ugomvi wake na Sabaya ni wa kisiasa zaidi na haumnufaishi yeye wala Sabaya. Anayenufaika ni wanasiasa ambao hawaonekani kabisa.

Ole Mushi
0712702602.

Tuseme sabaya anaonewa sasa anavyovamia na kupata watu tuseme anasungiziwa hadi alivyoonesha dharau kwa Mkuu wa Mkoa tuseme tunamsingizia ppale hakuwa yeye
 
Anaandika Mtozi Alloyce Nyanda

Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson

Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.

1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?

2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?

3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!

4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?

6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?

Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?

Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
SWALI LA 1: SIONI MANTIKI KWA NYANDA KUMUULIZA SWALI HILI KUMBUSHO. KWANZA SIO KUMBUSHO ALIYEDAI KUWA NA HIYO VIDEO. PILI, ILE VIDEO YA CCTV IWEPO AU ISIWEPO HAIONDOI TUHUMA ZILIZOPO DHIDI YA SABAYA, KWA KUWA UTENDAJI KAZI WAKE UMEJAA VITENDO VYA KIHUNI NA USIOZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI. TATU, KIMBUSHO HATOI TUHUMA, TUHUMA ZINATOLEWA NA SWAI.

SWALI LA 2. SWAI HASEMI KAMA HUO MRADI WA NYOKA ULIZUIWA NA WATU WA MALIASILI, KUMBUSHO HANA SABABU YA KUWAULIZA WATU WA MALIASILI KWA KUWA ANAMNUKUU TU MLALAMIKAJI ANAYEDAI SABAYA NDIYE KAMZUIA. SWALI AMBALO YEYE MWENYEWE MTOZI ANAPASWA KUJIULIZA NANI AMBAYE ANGEZUIA MRADI HUO KIUTARATIBU, KAMA HOJA NI VIGEZO-NI SABAYA KAMA DC AU WATU WA MALIASILI?

SWALI LA 3. KWANINI NYANDA ASILICHULIE TU KWAMBA SUALA LA SWAI KUWA JIPE KAMA KUJIFICHA KWA MAANA YA KWAMBA ENEO LILE HALIKO KATIKA MAMLAKA YA SABAYA KAMA DC?

SWALI LA 4. NANI AMEMWAMBIA ALOYCE NYANDA KUWA KAMA MALI ZA SWAI ZIMEUZWA ARUSHA KWA MNADA NA CRDB BASI ANAKOSA HAKI YA KULALAMIKA DHIDI YA SABABYA KAMA ANAONA KUNA MAMBO MABAYA AMEFANYIWA? HII NDIO CRITICAL THINKING YA WATANGAZAJI WA STARTV?

SWALI LA 5. JIBU LAKE NI SAWA NA JIBU LA SWALI NAMBA 4.

* HUYU NYANDA ACHUNGUZWE, INAWEZEKANA AMEPEWA MSHIKO KUMTETEA SABAYA!
 
Ongea na hii ..wanaziba hadi kamera ili wafanye uporaji
 
Sabaya ni kiboko ya Mbowe plus BAVICHA! Na huyo ni mtoto wenu, sipati picha angekuwa msukuma tungesikia kila aina ya matusi. Kampeni yenu haitafanikiwa mama Samia naye anaakili, sana mnachofanya ni kumpiga teke chura!
 
Tuhuma zimeelekezwa kwa Sabaya zinakuwasha nini? Mwache aje jamvini ajitetee mwenyewe au aendee mahakamani kushtaki kwa kuchafuliwa jina.
 
Back
Top Bottom