Mtozi Alloyce Nyanda: Kuna watu wanamtumia Swai kumchafua Sabaya?

Sabaya ni kiboko ya Mbowe plus BAVICHA! Na huyo ni mtoto wenu, sipati picha angekuwa msukuma tungesikia kila aina ya matusi. Kampeni yenu haitafanikiwa mama Samia naye anaakili, sana mnachofanya ni kumpiga teke chura!
Atakuwa anakutifua mtaro si bure.
 
Mama amesema hataki wafanyabiashara wabugudhiwe. Huyu Sabaya ana madudu mengi ya hovyo, aliwahi kusema wafanyabiashara wa mabasi Arusha/Moshi-Dar wameunda genge la uhalifu kuharibu miundombinu ya reli ili biashara zao zisiathirike, kuna CCTV kamera footage zinamwonyesha akivamia biashara za watu na kuwaumiza watu, kuna ile ishu ya kulala hoteli moja ya kitalii Arusha akagoma kulipa na kuwatisha kuwa yeye ni usalama wa taifa.
In short huyu ni muhuni na anaendesha genge la wahuni kupora na kuwaumiza watu. Hafai hata kuwa mwenyekiti wa mtaa.
 
Haya ni swala la muda tu, jiwe kwa jiwe, moto kwa moto
Mzee walikua wanavamia hatari siku moja walivamia duka la Mama mmoja tena katoka msibani wanataka kuondoka nae sijui risiti sijui report mimi nikaingilia kati kidogo na kuwaomba wamuache yule Mama nikawauliza swali la kizushi asipotoa report kuna madhara gani yaani walikariri maswali na majibu hapo kuna wateja washaondoka weengi tuu daah baadae wakaamua kuondoka wakidai watarudi nikapata taarifa walikua wanamchukua mwenye duka wanazunguka nae hata siku nzima ili atoe hela akitishiwa asipewe kesi ya uhujumu uchumi majambazi kweli wale jamaa nimeshuhudia kwa macho yangu na niliwaambia mimi siogopi kitu chochote lakini hamuwezi kumuonea huyu mama tukiona...
 
Anaandika Mtozi Alloyce Nyanda

Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson

Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.

1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?

2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?

3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!

4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?

6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?

Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?

Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
Tangu lini sabaya alikuwa msafi?
 
Cartbert nakufahamu muda sasa toka ukiwa Usukumani ulipo kuwa unahangaikia maisha ndugu na kwa hakika kwa upambanaji wako hatimaye ulipata pesa na leo ni mtu mwenye biashara zako nzuri na zinazo kuingizia riziki ikiwamo hotel yako ya Weruweru.

Pamoja na yote lipo jambo ambalo naanza kuhisi kama si linaenda kukufilisi basi litaenda kukufanya uwe mtu wa kujuta sana hapo baade nalo ni kutaka upambane na wanasiasa.

Kaka siasa na wafanya siasa zao huwa si watu wa kutabirika na mara nyingi huwa wote ni watu wa visasi na kinyongo.Mpambano wako na yule bwana mdogo Sabaya binafsi nahisi utakayeumia ni wewe na hii ni kwa sababu dogo ana watu nyumba wanaomtumia kukuumiza kisa ni USWAHIBA WAKO na MBOWE.

Kwa muktadha huo ustarajie kabisa Sabaya utamkalisha kwenye hilo zaidi ndiwe unayeenda kuumia!

CCM haikupendezwa na namna ulivyokuwa ukiisariti wakati ule mlipokaa chama na wafanyabiashara na kupanga mikakati ya kulichukua jimbo la Hai nawe kwa uswahiba wako na Mbowe ulikuwa ukivujisha MIKAKATI ile na mara moja walipo kugundua walikoma mara moja kukupa mwariko wa kujumuika nao na ndipo nawe uliamua pasi na siri kuonyesha uswahiba wako bila woga na Mbowe.

Sabaya ni kirusi mahsusi kilicholetwa Hai kwa ajili 'yenu' na usipokuwa makini utaishia kufirisika.

Nimekushauri japokuwa hatua ni uamuzi wako kupiga.

Achana na wanasiasa Cart..
 
Eeeh this way Sabaya that way Sabaya!

Whats so special with him?!
 
Iwe ni Sabaya au mwingine, kama huo ni ukweli, biashara imemshinda. Hotel kufungwa haina hata impact kwa uchumi wa mkoa.
 
Naona Sabaya anahangaika mno,Video zako zimetapakaa mitandaoni sasa na mama hapendi wapandisha mabega na ww unakuja kutupandishia mabaga humu.Soma alama za nyakati kaka,Enzi za vitisho zimezikwa CHATTLE.
 
Sukuma Gang, mnahangaika kama kuku anayetaka kutaga,haya umehamia kwa kibaka wa kimasai
Wasukuma hata usipotupenda unapoteza muda bure tu ndugu Sisi tupo leo,kesho na hata keshokutwa.

Ziada,sisi ndiyo wenye funguo zote za siraha zenye ncha kali ndani ya Nchi hii-jiongeze!
 
Mbona Sabaya ulikuwa unamtisha Swai kwani yeye ni mwanasiasa,? Kama wanasiasa wanacheza ngoma zao sasa si wacheze wanasiasa kwa wanasiasa?

Mbona sasa wanaingilia watu wengine wasiowahusu wao wakiguswa wanaishia kulia🤣🤣🤣🤣
 
Anaandika Mtozi Alloyce Nyanda

Nimeona Video ya Mfanyabiasha Cathbert imepostiwa na @kumbushodawson

Kumbuso ni rafiki yangu sana na kwa kuwa sisi sote huwa ni waumini wa ujenzi wa hoja basi kabla ya kuingia katika mjadala wa msingi napenda maswali haya yajibiwe kisha tuje sasa kwenye Hoja hiyo hapo juu.

1. Huyu Bwana Cathbert mwaka 2019 aliwahi kusema kuwa Mkuu wa wilaya Sabaya aliwahi kuvamia hotelini kwake na makundi ya watu na kupora hela na kulazimisha kuchukua mwanamke kwa nguvu na kwamba Bwana Cathebert alisema atatoa Video ya CCTV ikionyesha huo unyama wa Sabaya lakini tangu mwaka 2019 hadi leo ni miaka 2 hakuna hiyo Video; je Video ipo wapi?

2. Anadai Sabaya alimzuia mwekezaji wa maonyesho ya nyoka kufanya hivyo Hai! unajua nyoka ni maliasili na nyara muhimu za serikali? umewahi kumuuliza kama alikidhi vigezo na taratibu za kisheria kumruhusu kufanya hivyo?

3. Huyu bwana katika Video hapo
Juu anasema amekimbia na kujificha kutokana na vitisho vya Sabaya na anamuomba mama Samia amsaidie! Swali mtu anasema amejificha wakati anasema yupo pahala flani kwenye shamba tena mchana kweupe na yupo Tanzania je Kumbuso kujificha ndo huku ambapo Mimi na wewe hatupo Kilimanajaro ila tumeshajua huyu bwana yupo wapi!

4. Asante Tours Ooshi si Arusha na kwamba kuna video ikionyesha kwamba mwezi wa pili mwaka huu kampuni na ofisi iliuzwa kwa mnada na bank ya CRDB mil 600 kutokana na madeni ya bwana huyu anayodaiwa toka mwaka 2009 huko nako Sabaya alikuwa Hai?

6. Zimekuwepo tuhuma za huyu bwana kupora maeneo na kuyabadilisha hati kisha anaenda kukopa bank na kuyatumia kwa
Manufaa yake na DC alishwahi kuyarudisha mashamba kwa wenyewe, je Kumbuso unafahamu Hilo? Je, alishawahi hata kujirekodi kusema kuwa ni uwongo?

Baada ya uteuzi wa mawaziri,makatibu wakuu mhe Rais alisema sasa anakuja kwa ma Rc na kina sabaya,Haya nayo yakazuka,common sense inasemaje?

Naomba Tuanze na haya kisha twende kwenye hoja ya Msingi ya bwana Mfanyabiashara ambae yupo shambani alipojirekodi kutupa habari amejificha.
Huyu Nyanda naye asaidie upelelezi,amekuwa mnufaika wa ujambazi wa Sabaya, gharama za arusi yake kwa asilimia tisini ziligharamiwa na huyu jambazi
 
Back
Top Bottom