Mtoto wangu wa mwisho sio wa mume wangu. Je, nimwambie ukweli?

Kama kweli umeokoka nenda kawaambie hao Jamaa ukweli, huyo mume wako na aliyekuwa mchepuko wako....waambie tu ukweli kuhusu huyo mtotp
 
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 33, naishi hapa Tanzania, mkoa naogopa kutaja. Nimeolewa na nimebahatika kuzaa watoto wawili katika ndoa yangu. Ila hapa siku za karibuni niliamua kuokoka na tumefundishwa kusema ukweli huko kanisani..

Sasa ukweli nilionao mimi ni kuhusu huyu mtoto wangu wa mwisho, sio wa mume wangu wa ndoa. Nilichepuka tu huko nje kwa ushawishi wa huyu jamaa maana nilijikuta nimevutiwa naye ghafla. Ila mimi kama mama najua ukweli huyu mtoto sio wa mume wangu, ila mume wangu anajua ni wake na pia hata yule baba wa mtoto naye hajui kama ni wake hii ni siri ambayo nimekuwa nayo toka muda sana..

Sasa kila nikienda kanisani nafsi inanisuta hata amani ya kusali inakosa najiuliza nimwambie ukweli mume wangu au niendelee kunyamaza. Kuhusu kunipenda mume wangu ananipenda na anipa kila kitu hadi gari alininunulia ni shetani tu alinipitia na kujikuta nafanya tukio hilo..

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kuhusu hili

View attachment 861310

Kwa niaba.
Shetani ana kazi sana. Watu wanakwepa lawama kwa kumsingizia yeye. Sema ukweli uishi kwa amani, kubeba mzigo muda wote huo ni torture ila pia ukimwambia mmeo ujue ndoa ndio imeisha hapo.
 
Write your reply...wewe mwenyewe almashauri ya kichwa chako inasemaje!??tuanzie hapo
 
Piga kimya,ukimwambia utaharibu sana...kwenye familia nyingi wanaume wanalea watoto wasiokuwa wao!
 
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 33, naishi hapa Tanzania, mkoa naogopa kutaja. Nimeolewa na nimebahatika kuzaa watoto wawili katika ndoa yangu. Ila hapa siku za karibuni niliamua kuokoka na tumefundishwa kusema ukweli huko kanisani..

Sasa ukweli nilionao mimi ni kuhusu huyu mtoto wangu wa mwisho, sio wa mume wangu wa ndoa. Nilichepuka tu huko nje kwa ushawishi wa huyu jamaa maana nilijikuta nimevutiwa naye ghafla. Ila mimi kama mama najua ukweli huyu mtoto sio wa mume wangu, ila mume wangu anajua ni wake na pia hata yule baba wa mtoto naye hajui kama ni wake hii ni siri ambayo nimekuwa nayo toka muda sana..

Sasa kila nikienda kanisani nafsi inanisuta hata amani ya kusali inakosa najiuliza nimwambie ukweli mume wangu au niendelee kunyamaza. Kuhusu kunipenda mume wangu ananipenda na anipa kila kitu hadi gari alininunulia ni shetani tu alinipitia na kujikuta nafanya tukio hilo..

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kuhusu hili

View attachment 861310

Kwa niaba.
Nakushauri uwaeleze wote ukweli,mumeo,huyo uliyechepuka nae,ndugu zako Na viongozi wako wa kabisa,hapo ndipo utakuwa huru
 
Wanaume wenye watoto wawili humu jf kakagueni watoto wenu. Suala la gari laweza kuwa changa la macho, wewe kama una watoto wawili ma mkeo bila kujali ulimnunulia gari au laa kakague wanao haraka.
 
Kitanda hakizai haramu, kuna kazi kubwa mbele yako:-
1. huyo mtoto ana haki ya kumjua baba yake halisi.
2. Mumeo ana haki ya kutambua huyo sio mwanae ili maamuzi mengine yafanyike.
3. Baba wa huyo mtoto (biological father) ana haki ya kujua ukweli kuhusu mwanae, madhara ya kuusema huo ukweli siwezi kutabiri lakini lazima mambo yako(ya familia yako) hayatabaki vilevile)........................
 
Unakuta siku moja watoto wa mchepuko wanakuja kupishana au kukutana na mwanao afu wanaonana wanafanana afu mwishowe ''duuh Jessica yaani nimeamini duniani wawili wawili cheki yule jamaa anavyofanana na wewe" kakake Jessica, mmoja wa mtoto wa mchepuko atavyosikika akimwambia dadake

Mwambie tu ukweli, ukweli humuweka mtu huru..Bora afahamu mapema kwani atakapojua ukweli itakua balaa zaidi.

Inawezekana jamaa keshajua ila anasubiri muda ufike.

Hivi unachepukaje na kupata ujauzito kizembe hivyo, kila siku wanasema kuhusu njia za uzazi, uh...
 
Form four ulipita kweli? Soma habari mpaka mwisho...nilishasema kwa niaba...au mpka niweke na sauti? Uwe na adabu kijana
Dah miaka 33 nae anaita kuwa na adabu kijana as if yeye ndo monitor humu ndani. Binti wewe humu ndo teenager. Wote tumekubuhu hata ndefu tunanyolea chupa
 
Dah miaka 33 nae anaita kuwa na adabu kijana as if yeye ndo monitor humu ndani. Binti wewe humu ndo teenager. Wote tumekubuhu hata ndefu tunanyolea chupa
Do u smoke?
Do you drink?
Do you like sex?.....
 
wewe acha kufanya reasearch na sisi waa JF, sisi wengine humo ni wasomi wakubwa, waliotebea dunia nzima, kukutana na watu aina mingi na wenye akiri tofauti, uchumi tifauti na pia elimu tofauti na mila tofauti, hii umeandika hapa ni kitu unafanya reasearch kwetu au ni upuzi tu wako, tafuta njia ingine ya kufanya mambo, barikiwa sana
 
Back
Top Bottom