Mtoto wangu wa miaka 8 anaogopa somo la hisabati kama ukoma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wangu wa miaka 8 anaogopa somo la hisabati kama ukoma!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark City, Apr 18, 2010.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wadau naombeni msaada wenu,

  Mwanangu wa miaka 8 (yuko darasa la 3) anataka kunipa kichaa. Nimejaribu sana kumsaidia aweze kufanya vizuri kwenye masomo yote na amejitahidi ila siyo hisabati.

  Nimekuwa nikimfundisha lakini naona siku zinavyoenda ninakuwa kama natangaza uadui naye au vita. Anaonekana kukata tamaa na hisabati hadi napata wasi wasi.

  Hata ukimwomba kuona madaftari yake, wakati mwingine anaficha daftari la hisabati (na kudai kuwa liko kwa mwalimu) au analiweka chini kabisa ya madaftari mengine. Nadhani angependa nisilione kamwe.

  Kwenye mitahani anafanya vizuri masomo yote isipokuwa hisabati. Anaweza kupata A kidogo, B+ na B lakini hesabu ni kuanzia 40-50%. Mbaya zaidi hata ukimfundisha kitu akaelewa na kufanya mazoezi vizuri, kesho yake hakumbuki zaidi ya nusu ya vitu. Ndugu zangu nifanyeje?

  Nasikitika sana kwani sikuwahi kuona kama hisabati ni somo la kusumbua kiasi hicho na hasa hasa katika hatua za awali. Lakini kubwa kabisa ni kwamba ninsingependa kumwona mwanangu anakata tamaa na somo lolote mapema namna hii.

  Naombeni maoni au ushauri.
   
 2. P

  PELE JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hesabu ni somo muhimu sana katika dunia ya leo. Mwanao bado ni mdogo na hongera sana kwa kuanza kumsaidia mapema katika somo hilo. Usiwe mkali wala kupata frustration endelea na juhudi zako. lakini usichukue kipindi kirefu kukaa naye huku ukimfundisha, saa moja au dakika 90 kila siku zinatosha kabisa na tena ujitahidi kutumia lugha ya upole na siyo ukali na baada ya muda utaanza kuona matokeo ya juhudi zako.

  Kwanza mpe table kuanzia moja mpaka 12 awe anazipitia kila siku na wakati mwingine kufanya kama wimbo ili aweze kuzishika kichwani. Narudia tena mwanao bado mdogo kwa wewe kuanza kuwa na wasiwasi lakini mpe wasaa wake kama mtoto afanye vitu vya kitoto na pia unapokuwa unamfundisha achana na lugha ya ukali na uwe mvumilivu sana ili asizichukie hesabu vinginevyo itakuwa vigumu sana kuzifahamu.
   
 3. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Sikubaliani nawe hata kidogo, yaani miaka 8 darasa la 3 alianza na miaka 5? huoni umri ni kigezo # 1 cha uelewa wa mtu?
  Masomo ya darasa la tatu ni magumu sana kwa mtoto wa umri huo hasa kama anasoma english medium, so pata ushauri kwa walimu wake na usimfosi.
  Ushauri wa PELE pia ni muhimu, ukiona bado mrudishe nyuma 1 year

  ...................................

  Amani yetu inatumiwa vibaya.
   
 4. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Badilisha methodology yako, make it simple and use child friendly examples na hakikisha mtoto hakuogopi.
  Kamuzu sio kweli umri ni shida hapo, mtoto anatakiwa kuanza darasa la kwanza akiwa na miaka 5
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wala usihangaike na kutishika. Wala usipate hofu kuwa anaogopa hisabati. Dunia si hisabati peke yake. Kuna mengi mengine ambayo yanaweza kumtoa katika maisha. Inafurahisha kuwa ameshaonyesha kuwa hicho kitu ni kigumu wkake tangu mwanzoni. Ni wakati wako sasa kama mzazi kumsaidia kubaini kile anachokimudu na kukipenda ili ajielekeze huko tangu wakati huu. Usimlazimishe kwenye hisabati kwani utamuharibia maisha yake ambayo anaweza kuyajenga hata bila hiiyo hisabati
   
 6. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Dark City kama wewe si mwalimu basi kumfunza mtoto inataka techniques zake na hasa yule ambae somo fulani linampiga chenga mfano kama hilo hisabati.

  Mimi mtoto wangu nilikuwa napata shida naye sana kwenye hisabati kama wa kwako lakini kumbe sikuwa na techniques. Alipofika darasa la pili kwenye shuleni fulani walipata mwalimu mzuri na aliendelea vizuri sana.

  Kwa hivyo kama unae mwalimu anaefundisha grade one mpaka three ndie ataeweza kumfunza vizuri kuliko mwalimu wa madarasa ya juu.
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hakika yawezekana mtoto anapambana na hesabu zilizo juu ya umri wake. Si ajabu anasoma hesabu za darasa la IV au la V maana mitaala yetu kwa kweli inatisha wakati mwingine. Nazungumza hivi nikikumbuka siku moja nilikuwa naongea mambo ya mitaala na mwalimu mmoja mzungu anayefundisha katika moja ya High Schools zetu hapa nchini. Yule mwalimu mzungu aliniambia kwa mshangao kidogo kuwa mitaala ya High School ya Tz si sawa na ile ya kwao. Akasema kule kwao yale ambayo vijana wetu wa High school wanayasoma kule kwao mambo hayo wanayasoma wakiwa Chuo kikuu. Akasema mitaala yetu iko juu mno ukilinganisha na umri wa mtu na level yake ya kufikiri. Kumbe si ajabu huyo mtoto - nikifuata mawazo ya yule mwalimu - akawa anafundishwa shuleni mambo ya darasa la nne au la tano ambayo yako mbali kabisa na umri wake wa kufikiri.
   
 8. d

  diana98 Member

  #8
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [
  Du!! mhhh
   
 9. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  huyo mtoto bado mdogo, mwendee taratibu
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Si kweli kwamba mtoto kuanza shule na miaka 5 ni tatizo. Hizo ni fikra zako tu. Najua hii ndio sababu hata serikalini wanang'ang'aniza watoto waanze shule na miaka 7. Matokeo angalia vibinti vinavyozaa huko mashuleni hata kabla ya kumaliza shule ya msingi.
  Ukweli miaka 5 ni kwamba huo ndio umri mzuri hasa wa kuanzia shule darasa la kwanza.

  Jambo ninaloliona ni kijana mwenyewe tu anahitaji kupata msaada zaidi na hasa kupata mwalimu mzuri wa hesabu na aliyebobea katika taaluma.

  Mimi nina kijana wangu yuko form 2 sasa na ndio kafikisha miaka 13 yuko safi katika masomo.
  Binafsi nilipokuwa shule ya msingi sikuipenda hesabu. Nakili kwamba niliichukia sana na kuona ni somo gumu sana. Nilipenda masomo yote kasoro hesabu tu maana niliona ni gumu.

  Baba yangu alikuwa mwalimu na alinikabidhi kwa mwalimu mwenzake mmoja nikiwa darasa la 5 anisaidie. Nakiri kuwa alikuwa a born teacher kwa sababu alinifundisha hesabu na nilielewa kila alichonifundisha na nilitokea kuwa mzuri katika hesabu na ni msingi wake ndio ninaotumia hadi leo hii.

  @Dark city usikate tamaa. Mtie moyo kijana. Usiwe mkali sana kwake. Mtafutie mwalimu mzuri, mpole mwenye kipaji cha hesabu utashangaa matokeo.
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu usipate taabu sana mimi nilikuwa na hali hiyo na mtoto wa miaka 7 na alikuwa std 3 kama huyo na tatizo ni hasira zako anapokosea unamchapa kumbe hilo ni kosa. Mimi nilichofanya ni kumtafutia mwalimu ambaye ana uzoefu na hadi leo mtoto napenda sana hesabu na anaziweza sana siku hizi. Kwa hiyo ukiwa mkali mtoto unamchanganya anakuwa anaogopa badala ya kujifunza.

  Nakushauri mtafutie mwalimu ambaye anauzoefu wa kufundisha watoto.
   
 12. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #12
  Apr 18, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wazazi huwa hatupendi kuona watoto wetu wakifanya vibaya shule. na sometimes tunatumia nguvu kutaka mtoto afanye vizuri kumbe ndo tunaharibu. Mimi pia nina mtoto ambaye mwanzo alikuwa anafaulu sana hesabu, baadae akahama shule akaanza kufanya vibaya sana hesabu. alikuwa anafanya vizuri sana masomo yote kasoro hesabu. Nilipofwatilia nikagundua kuwa rafiki zake wote wa shule mpya hawapendi hesabu, kwa hiyo wanaambiana kuwa hesabu ngumu.
  Nilimwommba mtoto wa dada yangu ambaye ni mkubwa kwake na anapenda sana hesabu, akaanza kumshawishi tena kuwa hesabu ni somo rahisi sana, na ikawa kila weekend anakuja nyumbani kumfundisha. sasa angalau anafanya vizuri tena.
  Jitahidi kutafuta mwalimu au mtoto ambaye anapenda hesabu wawe wanafundishana, wewe mwenyewe utapata kichaa bure
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Inawezekana kuwa umri ni tatizo lakini nina wasi wasi na hilo. Mtoto alianza shule akiwa na miaka sita kamili na anafanya vizuri kwenye masomo megine kama nilivyosema. Angekuwa anafeli masomo yote, ushauri wako wa kumkaririsha darasa ungefaa. Ila hapa nadhani kuna tatizo zaidi ya umri.

  Kwa hiyo una maana kwamba mtoto afanye specialisation akiwa darasa la 3? Sidhani kama ni busara. Kama angekuwa amefikia hata darasa la saba ningekubaliana na wewe. Pia mimi siyo muumini wa mambo ya mzaha kama hizo kauli zinazosema kuwa maisha siyo hisabati n.k. Kuna jamaa tulisoma naye O'level akawa hasomi kwa madai ya kwamaba maisha siyo shule. Baada ya kumaliza shule alipata Division Zero (0) na kuambulia kibarua cha ulinzi karibu na njia inayoendea kituo cha treni. Kwa hiyo wakati washikaji wanakwenda A'level wakawa wanapatia karibu na ofisini kwake!

  Kwa hiyo simlazimishi ila lazima nijiridhishe kuwa kweli ameshindwa hilo somo badala ya kuchukua hatua nyepesi nyepesi eti kwa vile dunia siyo hesabu tu.


  Labda kama una maana kuwa syllabus nzima ya Tanzania ni mbovu (yaani inashindwa kuoanisha vitu vya kufundisha na umri wa watoto). Hata hivyo vitu vinavyofundishwa darasa la 3 Tz ni karibia sawa na vile wanavyofundisha Kenya. Mtoto anatumia vitabu vyote, vya Tz na Kenya.

  Inawezekana bado ni mdogo lakini mbona anamudu masomo mengine? Hilo la kumwendea taratibu nitalifanyia kazi.

  Kweli mkuu, inawezekana nashindwa kupatia mbinu za kumfundisha. Ila nimejaribu kumwachia mama yake kwa muda naona bado habadili mwelekeo ili alipende somo la hisabati. Nimejaribu kufuatilai shuleni kwao, nikaamibiwa hili tatizo la hisabati wanalo watoto wengi darasani kwao. Nitaangalia uwezakono wa kutafuta mwalimu ambaye anaweza kumrudishia hamu ya kulipenda hili somo.
   
 14. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Jitahidi mkuu, taratibu tu ataelewa maana naona hatari ya mwanao kuwa kama yule mwalimu wa kwenye tangazo la haki elimu anayefundisha square root.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu nikiangalia hilo tangazo halafu nikamwangalia boy wanagu natamani ardhi inimeze. Kama kweli wapo walimu wa namna hiyo basi duniani kuna vituko!
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kabla sijatoa ushauri wangu niambie mwanao anajua kuhesabu hadi ngapi?

  nikutahadharishe kuwa watoto ni saikolojia tupu......... hata unapoongea naye kuna vitu huwa anakuambia unashindwa kusikia kwa sababu ya kushindwa kumsoma saikolojia yake...........

  naanza kwa kukupa kitu kimoja unachoweza kuona cha kipuuzi lakini kizingatie, halafu ukinielewa, uende kumwelekeza na mwanao, kama umeanza kumkaririsha tebo tafadhari sitisha kwanza hadi tutakapokuwa tumeelewana namna ya kumuelekeza kujifunza hesabu..........

  step 1:
  nakushauru usome avatar ya fixed points, halafu ujaribu kufumba macho na ujaribu kuweka namba mbalimbali kufuatana na mtiririko wa kuhesabu kwenye mistari ya mchoro wa ile avata bila kuitazama............. kisha fungua macho uone jinsi ulivyoweka namba zako na umbile linalojitokeza ukiziunganisha hizo namba kwa mstari............. hesabu idadi ya pembe/kona zinazotokea, angalia kama umbo liko katika sura inayoeleweka ama la.......... usijaribu kulazimisha umbo lako lifanane na lile la avatar ya fixed point na wala usisahihishe ukigundua halifanani na wala usichungulie avatar wakati ukiandika namba zako hadi umemaliza kuziandka......... na ukimaliza, kazi a avatar inakuwa imekwisha............. tuanaingia hatua nyingine...........

  ukimaliza hilo zoezi, kabla hujaongea na mtoto niPM nitakupa hatua inayofuata yaani step 2..............
   
 17. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #17
  Apr 18, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapo kwenye Red, mama yake na wewe wote ni wazazi tu, kama wewe ulishindwa kama mzazi basi hata mama kama sio mwalimu wa primary hataweza, labda kama angekuwa mwalimu. Mimi mwenyewe mama na siwezi kufundisha wanangu, huwa tunaishiana kufinyana na kumwambia akalale hata kama katoka kuamka. maana sometimes nahisi kama hataki kusoma ili akacheze, kwa hiyo adhabu huwa kama hutaki kusoma basi na kucheza hakuna. kwa kweli inaumiza sana mtoto asipofanya vizuri, na hasa kama unaamini angeweza kufanya vizuri akiongeza juhudi.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hii inategemea ww baba ulikuwaje enzi hizo kwenye Hisabati!
  Kama ulikuwa unakuna kona vipindi vya hesabu basi umemwambukiza hata mke wako nae jaribu kuulizia kama alikuwa fit kwenye hisabati labda kachukua kipaji cha mama yake.
   
 19. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Mwambie "troublesome, crack headed halfcast from Harare" will come get him if he doesn't do his homework...lol!!
   
 20. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  inategemea na wewe mzazi ulizipenda? watoto wanafuata.....
   
Loading...