Mtoto wangu tangu amezaliwa hafumbui macho wala hatikisiki

Daktari hajaweka bayana tatizo la mtoto. Japo kuna Nesi kaniambia mtoto ameathirika kichwani kutokana na complication during deliver. Ila daktari hajatuambia chochote
Pole sana, daktari inamlazimu akwambie tatizo la mtoto wako kwa kina na namna ambavyo amepanga matibabu yake. Kama hawezi kukwambia hayo nenda kwa Daktari mkuu. Ikishindikana chukua mwanao mpeleke Private Hospital au Muhimbili kama ambavyo umeshauriwa humu. Ukiendelea kukaa hapo tatizo linaweza kuwa kubwa.
 
Referral Mara nyingi inatolewa kama hospitali aliolazwa hawana uwezo Wa kumtibu; ila kama mtoto hukulia Mara baada ya kuzaliwa, au alivutwa kwa kutumia vifaa maalum au mama alipata uchumngu Wa muda mrefu ambao ulisababishwa atolewe kwa kuvutwa; inawezekana aliumia ubongo (damage of immature brain) kitaalam amepata Cerebral Palsy; na ukubwa Wa tatizo utategemea alichukua muda gani kulia, na inaathiri uwezo Wa misuli kufanya kazi
 
Kwa hiyo unatushauri tufanyeje?
 
Muhimbili mtoto anapokelewa kwa rufaa. Bila barua ya rufaa huwezi kupata msaada muhimbili. Hapa hospitali nilipo hawataki kutoa rufaa

Si kweli kitu hicho , basi itakuwa hospital ya kinyama sana kama watamkataa mtoto mchanga .
 
Poleni Sana,tunazidi kuwaombea. Mungu mfanyie wepesi,litapita hili. Muaminini Mungu tu
 
Kama upo dar Nenda tabata chang'ombe kwa dokta kundy (Kundy dispensary)ni specialist mzuri sana wa watoto.
 
Mi nashauri aendelee kupatiwa huduma hapo hospital, ataendelea kurecover Slowly ingawa sijui hio hospital uwezo wake Wa kimatibabu ukoje, kuna specialist wa Watoto/Daktari wa watoto? ingekuwa vizuri akamuona Huyo mtoto;
Na wakati mwingine pia wanashindwa kutoa referral kama chanzo cha tatizo ni wao wenyewe;
 
Pole sana, InshaAllah M/Mungu atawafanyia wepesi tunakuombea na kumuombea mtoto wetu na mama wa mtoto M/Mungu awajaalie moyo wa subira
 
Ukisali omba sana mungu atamtia nguvu ,Japo hukutaja una ishi wapi ila kama una uwezo nenda mtwara masasi kuna hospitali imefunguliwa na wachina ni madaktar wazur sana huenda akapata matibabu ..
Kweli kabisa pale karibu na stand nawajua wale jamaa wapo vzur sana
 
Back
Top Bottom