Mtoto wangu tangu amezaliwa hafumbui macho wala hatikisiki

Kuna daktari wa watoto hapo kwani au??

Jamani mm ni mwanachama mpya humu jamii forum nilikuwa naulizia pump kwa ajili ya kilimo zinapatikana wapi na zinauzwa kiasi gani pump ndogo za kumwagilia at least ekali 1 mpaka 5

Sawa. Ila changamoto IPO hapa hospitali tulipo hawataki mtoto apewe referal. Wanataka habaki hapa hapa
 
Maombi ni sahihi, lakini fanya means mtoto afike Dar,option mbili 1.muhimbili 2.kuna hospital inaitwa tumaini hospital upanga opposite na jeshi karibu na diamond jubilee.huyo daktari aliekuambia mtoto hapewi rufaa sio kweli jishushe wakuandikie rufaa Kwenye referral letter wataandika findings zao na treatment zako hivyo zitampa nafasi kwa atakae mpokea Dar kupata picha ya tatizo.
 
Sawa. Ila changamoto IPO hapa hospitali tulipo hawataki mtoto apewe referal. Wanataka habaki hapa hapa
Daah .. Vigezo vikiwa ni Mtoto Mchanga haruhusiwi kupata Referal ama ? .. Jaribu pia kua na Moyo wa Uvumilivu na usikivubkwa kipindi Hiki , Kama kuna taratibu za Kidaktari Pia Zisikilize kwa Matokeo Mazuri ya Afya ya Mtoto .. Jitahidi kua mvumilivu kuliko shauku , huku ukiendelea Kusolve na Kupata solution kutoka Sehemu nyingine .
Isitomee Ukapata Ushawish wa kidharau Ushauri wa mAdaktri wa hapo .

Sent from my SM-N7502 using JamiiForums mobile app
 
Je hospitali walimpatia Carbon DiOxide? ili aamke? wakati anajifungua mtoto alilia? yawezekana bado mwili kutambua kama yupo nje, kama kitovu kimekatika mshtue na maji ya baridi...
 
Je hospitali walimpatia Carbon DiOxide? ili aamke? wakati anajifungua mtoto alilia? yawezekana bado mwili kutambua kama yupo nje, kama kitovu kimekatika mshtue na maji ya baridi...
Sijajua kama alipatiwa maana daktari kila kitu wanfanya siri hawaweki wazi tatizo nini na matibabu yakoje
 
Sijajua kama alipatiwa maana daktari kila kitu wanfanya siri hawaweki wazi tatizo nini na matibabu yakoje
Mkuu usizembee, utapoteza , kuwa 100% responsible. Huyo ni mtoto wako na wewe ndie unayelipa bili. Ni muhimu ujue kila kitu kutoka kwa daktari. Na sometime penyeza penyeza rupia apate extra "attenntion".
 
Sawa. Ila changamoto IPO hapa hospitali tulipo hawataki mtoto apewe referal. Wanataka habaki hapa hapa

Pole ndugu, mmefikia wapi? Na sababu zao za kutokupa ilikuwa nini haswa? Au umejaribu kwingine?
 
Pole sana Mkuu Mungu ni mwema atakuwa ok maombi muhimu
Pia kama walivosema jitahidi kwa haraka mumpeleke hospital kubwa
 
Pole ndugu, mmefikia wapi? Na sababu zao za kutokupa ilikuwa nini haswa? Au umejaribu kwingine?
Wanasema mtoto mchanga ambaye ana matatizo kama haya haruhusiwi kupewa referal kwa sababu anaweza akapata matatizo akiwa kwenye gari kwa sababu gari inaweza kutikisika hivyo mtoto akapata matatizo zaidi halafu lawama ikaenda kwao.
 
Pole sana

Kwa hiyo upo bado hapo hospitali? Au umeondoka kwenda ingine? Ila why now waone hivyo na wewe ulimpeleka mwenyewe? Wana madaktari wa watoto hapo?

Hao wanaokuficha tatizo ni nini labda hawalijui, sababu ni muhimu kama wamejua kuwataarifu wazazi na kuwapa options za matibabu etc
 
Kaa chini na uyo daktari muulize tatizo ni nini hasa na hatua sahihi za kuchukua kwa hali ya mtoto maana mwisho wa siku wewe ndio una jukumu la afya ya mtoto ukiwa unawaangali tu haiwezi kusaidia.
Mungu awafanyie wepesi najua jinsi inavyoumiza kuona mtoto anaumwa alafu haujui tatizo ni nini nimepitia hii hali na hainitoki akilini mwangu.
 
Duh!!pole Sana. I just try kujiweka katika viatu vyako lakini nashindwa hata kuvivaa. Mungu amfanyie wepesi kachanga kenu,pia nadhani kuna madaktari humu wakiuona huu Uzi wanaweza kutoa majibu. Tafuta daktari mmoja msogeze karibu ataweza kukupa ushawishi
 
Brother.
Usikurupuke kwenye hii ishu. M nakushauri nenda ukutane na hao watalaam wa afya wakwambie nn tatizo la mtoto wako coz naona had ss umepanic na hufaham kiundan mtoto ana shida gan. So, kabla ya yote ya kuomba rufaa jaribu kuuliza kwa daktar na wauguzi hapo wakupe abc's,zitakusaidia kuliko kwenda kuanza kudai rufaa kama unajua shida ya mtoto kiundan.
#n hayo tu!
 
Daaah.... Hawatoi rufaa inauma sana. Unajua mtoto hawaumi eeh wanachukulia simple simple tu..... Hapo specialist lazima aisee
 
Habari wakuu! Mke wangu amejifungua mtoto Wa kiume tangu tarehe 2 mwezi huu Wa Tatu. Ila mtoto tangu amezaliwa hafumbui macho, hawezi kunyonya, hatikisiki yaani viungo vya mkono na miguu havitikisiki. Maziwa anapewa kupitia mabomba. Ila anapumua na kupata choo . Naomba msaada wenu. Kama kuna hospitali au daktari ambaye ni specialist Wa watoto naomba nielekezwe.
Pole sana kwa matatizo yanayomsumbua mtoto wako. Mimi ningeomba kuuliza...je kabla hajazaliwa mama alikuwa anapata/kusikia mtoto akicheza tumboni kama kawaida? Na je amezaliwa kwa njia yakwaida au upasuaji? Mwisho ujauzito ulikuwa umekamilika? Nikimaanisha amezaliwa kipindi chake Na sio kawahi au kachelewa kuzaliwa?
 
Back
Top Bottom