Mtoto wangu kazaliwa na kilo 6 na tatizo la mdomo sungura

Shy land

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
6,024
1,958
Habari za siku nyingi wakuu na members wore wa JF.

Ndugu wana JF wezangu tarehe 25 mwezi wa sita mwaka huu, wife alijifungua mtoto wa kilo 6 na mtoto akawa na tatizo la ugonjwa wa mdomo sungura.

Nashukuru Mungu hadi sasa mtoto anaendelea vizuri, nimeazisha thread hii kwa lengo la kuweza moja, kufahamishwa kama kuna tatizo mtoto atakalolipata badaye kutokana na kuzaliwa na kilo nyingi hivyo jambo ambalo siyo yakawida kwa elimu yangu na uzoefu wangu kwa watoto.

Pili niliambiwa zahanati kuwa mtoto akifikisha kilo kumi nimpeleke hospital kubwa ili kufanyiwa operation ya tatizo la mdomo sungura, kwa watu wanaofahamu hosptali nzuri na muda gani sahihi wakupeleka mwanagu wanijuze Tafadhali sana.

Na kama yupo mdau ambaye ashawahi kuwa na tatizo kama hili naomba, naomba sana sana tuwasiliane ili anijuze kuhusu utaratibu mzima na ngarama za zoezi nzima la operation.

Wakuu asanteni sana na poleni kwa mwandiko na kiswahili kibaya. Yote hii inasababiahwa na Mimi kuishia darasa la Saba.

Mwisho nisaidien mawazo yenu ni muhimu sana kwangu
 
Mshukuru Mwenyezi Mungu kwa kukupatia mtoto mwenye afya njema. Tatizo la mdomo wa sungura linatibika na hali itakuwa sawa. Kuhusu uzito usihofu, inaonekana mama alikua anapata lishe bora. Nimeona wamama wengi wanaokula samaki sana wakiwa wajawazito wanapata watoto wenye uzito mkubwa wengine husema pia watoto wanakua na akili sana, hili sina uhakika nalo.
 
Kwa mdomo sungura nenda CCBRT na linatibiwa bure kabisa na kama upo mkoani utatumiwa gharama za usafiri mpaka kufika dsm.
Ukiona ina fit nichek DM nikupe namba yao uwapigie kujua arrangements
 
Kwa mdomo sungura nenda CCBRT na linatibiwa bure kabisa na kama upo mkoani utatumiwa gharama za usafiri mpaka kufika dsm.
Ukiona ina fit nichek DM nikupe namba yao uwapigie kujua arm
Kwa mdomo sungura nenda CCBRT na linatibiwa bure kabisa na kama upo mkoani utatumiwa gharama za usafiri mpaka kufika dsm.
Ukiona ina fit nichek DM nikupe namba yao uwapigie kujua arrangements
Asante sana nakufata mkuu
 
Naona ushapewa muongozo sahihi wa mdomo sungura, nini cha kufanya...

Kuhusu uzito wa mwanao, hakuna madhara yoyote ihakikisha tu mama anampa mtoto maziwa ya kutosha
 
Mdomo wa sungura Kwa Sasa sio inshu , mtoto atarekebishwa na atakaa Vizuri.

Watoto Hawa changamoto yao kubwa Huwa ni katika lishe , na hivo basi ili Kumlinda na kumsaidia ,hakikisha Mama anajitajidi sana kumlisha Kwa angalau Mara 10 Kwa siku .

Mdomo wa sungura wenyewe kama wenyewe haihitajiki haraka kuurekebisha ila Hawa watoto wakati Fulani wanakua na Matatizo mengine Ivo ni vema umpeleke Hospital Kwa ajili ya uchunguzi zaidi .

Habari njema, Huduma za Hawa watoto ni Bure Bure Kabisa Tena Kwa TAASISI nyingine zinazotoa huduma zao ,Hadi Nauli wanakutumia.

Kuhusu Uzito mkubwa 6Kg, nadhan Kwa Tanzania ,mtoto wako amejivunjia rekodi yake,. Ni jambo la Heri mtoto kua na uzito ila wakati Fulani ni kiashiria Cha Matatizo ya ki genetic au Matatizo Kwa Mama au baadhi ya Medical conditions zinazopelekea uzito kua mkubwa ...na hivo Unawajibika Kumpelekea Mtoto Hospital Kwa uchunguzi zaidi .

Kuhusu Hosp , inategemea ni Wapi ulipo, kama upo Kanda ya Ziwa, Njoo Bugando chap !!.

Mwisho, Zingatia sana sana Lishe Kwa mtoto , Zingatia kwenda Hosp Kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa mtoto

Watoto Hawa wanakuaga na Akili Sanaa☺️☺️
 
Hongera kwa kupata mtoto mkuu. Hilo tatizo ni dogo sana. Waone CCBRT popote ulipo watakupa muongozo wote...gharama ni nafuu sana. Nenda pia NHIF mkatie bima ya watoto sh 50,400
 
Hongereni kwa kuzawadiwa big baby


Uzito hauna shida, hakikisheni mbali na huo mdomo viungo vingine vipo mahali pake sababu naomba nikupe case yangu

Nilijifungua mtoto wa kg nne, kumbe kwenye harakati za kujifungua walimvuta vibaya mkono wake uko loose halaf mbaya zaidi wakat wanampeleka kitandani walimlaza upande wa huo huo mkono mie nimekuta tu katoto kamelala alipokuja kuamka nikamueka sawa mkono mmoja umekaa tu tena na kiganja cha mkono kikawa kimepinda kuita dokta ananiambia nikae wiki kisha nimpeleke tena aangaliwe kama tatizo lipo au linaendelea,

Kama mzazi nilibadili hospital nikaunganishwa na dokta wamifupa tukaanza tiba tangu ana siku mpaka sasa ni miezi sita kila kitu kimekaa sawa

Alichoniambia dokta wangu ni kua mtoto akizaliwa akalia bila shida na ikatokea amepata tatizo kama hivo bas hayo matatizo yanatibika isipokua kama atachelewa kulia hio haitibiki mana shida imeanzia kwenye ubongo

Kukutoa hofu inatibika hio mdomo sungura bana kwa hio onana na madaktar mapema ujue nn unatakiwa kufanya
 
Asanteni sana Sky Eclat Nafaka FUTURE HUNTER ndg yangu was Siku nyingi sana Watu8, maoni na hongera zenu na kuniondelea wasiwasi juu ya mtoto wangu, Madame S asante sana kwa kunikumbusha hayo yore, MarkHilary na Carlos The Jackal nawashukuru sana kwa kutumia Mb na mda wenu kunitia faraja na utaratibu wa kufaata ili kutatua tatizo la mtoto huyu. Moyo wangu sitautendea haki nikiacha kuwashukuru Moderator kwa kazi yao kupangilia vizuri habari na maelezo yangu ili yaeleweke kwa kila msomaji. Mungu awabariki sana
 
Hongera kwa kupata mtoto mwenye afya njema. Suala la mdomo sungura limeongelewa vyema na wachangiaji wengine. Binafsi nitajikita kwenye uzito wa mtoto.

Watoto wa uzito wa kiasi hiki hujulikana kama MACROSOMIA.
Watoto hawa wanaweza kukua vyema kama watoto wengine.

CHANZO
Hii inaweza kuwa ni kutokana na:

1: Maumbile ya wazazi/kijenetiki.

2: Mzazi ambaye hakuwa na control nzuri ya sukari kwenye damu wakati wa ujauzito. Kutokana na hili, ni vyema kuwa waanglifu sana kwa wale ambao wanapata watoto wenye uzito kuanzia kilo nne na kuendelea mara tu baada ya kuzaliwa. Kwani huwa wana nafasi ya sukari yao kushuka, kutokana na mazoea ya kupata sukari nyingi inayopatikana toka kwa mama wakati akiwa tumboni.

USHAURI
1: Upande wa mama wa mtoto, kufatiliwa vyema sukari yake kwa sasa na pindi awapo mjamzito.

2: Kwa upande wa mtoto:
A: Mwanzishe mtoto kunyonya mara tu baada ya kuzaliwa, cheki sukari ya mtoto hasa anapoonyesha kutokuwa mtulivu au anapoonyesha hali ya kuchoka bila sababu.

B: Kutokana na ukubwa wa mwili na shingo kuwa fupi, wengi huwa na upumuaji ambao wazazi hupata wasiwasi kuwa hauko vyema. Ingawa huwa uko sawa, ila ni vyema kuwahusisha wataalamu wa afya ili kuelekeza jinsi ya kumlaza mtoto ili kutoleta shida wakati akiwa mchanga.

C: Watoto wa aina hii huwa ni rahisi kupata kitu kinaitwa metabolic syndrome hii inahusisha presha, sukari, mafuta/cholesterol nyingi na uzito uliopitiliza.

Hivyo, ni vyema kuwa na ufuatiliaji wa karibu pia na watoa huduma ya afya kwa kadri ya makuzi yake.
 
Habari zenu jamani,naomba kuuliza kuna mtoto alizaliwa na kilo3 point 2,kliniki yake kwanza uzito wake ukawa kilo 5 na point 3,kliniki yake ya pili akawa na kilo8 point 3,Je ukuaji huo wa uzito wa mtoto upo sahihi kabisa ama nyie mnaonaje
 
Habari zenu jamani,naomba kuuliza kuna mtoto alizaliwa na kilo3 point 2,kliniki yake kwanza uzito wake ukawa kilo 5 na point 3,kliniki yake ya pili akawa na kilo8 point 3,Je ukuaji huo wa uzito wa mtoto upo sahihi kabisa ama nyie mnaonaje
Wastani wa kuongezeka mtoto uzito ni wastani wa gram 800-1500 kwa mwezi.

Suala la msingi:
1: Kliniki ya kwanza ilikuwa baada ya muda gani tangu kuzaliwa?

2: Kliniki ya pili ilikuwa muda gani baada ya ile ya kwanza?

3: Mizani iliyotumika ni ileile?

4: Umejaribu kutumia mzani tofauti?

5: Mwili wa mtoto kuongezeka unaendana na unachokiona kwenye mzani?
 
hongereni kwa kuzawadiwa big baby

uzito hauna shida, hakikisheni mbali na huo mdomo viungo vingine vipo mahali pake sababu naomba nikupe case yangu

nilijifungua mtoto wa kg nne...
Mkuu naomba msaada wa kupata contact za huyo daktari wa mifupa nimsaidie mwanangu jamani, amezaliwa na kesi kama hiyo ya mkono kutokucheza na kupinda kiganja Ila vidole vinacheza vizuri na nikimuwekea kudole changu kwenye kiganja chalet anakamata vizuri tuu.
 
Je mama yake ana kisukari?uzito mkubwa kwa mtoto wakat mwingine sio afya ila ni tatizo kwa mama katk kipind cha ujauzito kama kisukar au pressure na kupelekea mtoto kukua na kupata uzito mkubwa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom