Mtoto wangu hataki kuniita Baba nifanyaje?

Nuoxian

Member
Mar 15, 2020
68
125
Habari ndugu, jamaa, na marafiki kama mada inavyojieleza hapo juu mimi naishi na mke wangu pamoja na watoto wawili wa dada zangu ambao wametangulia mbele za haki.

Shida kubwa inayokuja ni huyu mtoto wangu na yeye amejikuta ameingia kwenye mkumbo wa kuita uncle kama wenzake wawili wanavyoniita, saivi ana miaka 3 msaada nifanye nini ili aniite baba? Maana najaribu kumuambia mimi sio uncle ni baba lkn anataniita baba kwa mda huo huo baada ya apo ataendelea kuita Uncle.

1621318049161.png

 

Brian Spilner

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
662
1,000
Kawaida sana wala huna huja ya kumaind, with age atakuita baba tu don't push him/her. Otherwise kuwe kuna kitu unapungukiwa usipoitwa baba.

Mimi kuna mtu nilizoea kumuita mamdogo ajili ya watoto nilikua naishi nao ambaoo kiuhalisia ilitakiwa nimwite mamkubwa.
Kwetu Bibi yetu wazazi wetu wanamuita bibi ajili yetu
Mtaani kwetu kuna mamdogo wa mtaa mzima kwasababu anapoishi, yeye ni mama mdogo wa watoto. Miaka zaidi ya 28 sasa.

Wababa huita wake zao mama kwasababu ya watoto kumuita mama (wakati mwingine huwa na sababu nyingine)

Dada wa kazi huitwa dada na familia nzima kwasababu watoto wa familia humuita dada, hadi baba wa familia nae anamuita dada.

Mimi nilikua nikimuita dada yangu mamdogo kwasababu tuliishi na mtoto wa dada mkubwa aliyemuita dada mamdogo.

Inatokea sana. Sikutegemea aanzishie uzi.
 

Mzimu wa Kolelo

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
1,458
2,000
Kawaida tu MM alikuwa ananiita BABA AISHA tangu anaanza kuongea mpk alipokalibia miaka 4 ndo akaanza kuniita baba

Na hii ilitokana kusikia kila mtu ananiita BABA AISHA BABA AISHA naye akaliunga humo humo

Sawa na mimi nilikuwa na mjombaangu namuita babu kutokana kucheza na wajukuu zake LIKIZO tukienda kumtembelea wao wanaita BABU BABU basi na mimi nikazoea hvyohvyo mpk nimekuwa mtu mzima 7bu tunaelewana sana bado namuita hivyohvyo BABU kwa kumtania

Hvyo ataacha tu kutokana wenzake kazoea hvyo na yeye ila ataacha tu
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,024
2,000
Mtoto wangu wa pili alikuwa anamwita babake Baby

Ahahhahahhahahaah 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nimecheka sana.
Dah!

Wa tatu mpk kesho ananiita Mama ....
Anaweka jina lake(yani kama huyo ...... sio yeye)
Anasikia nyumba nzima wananiita kwa jina lake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom