Mtoto wa Waziri wa Elimu asome Buguruni S/Msingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Waziri wa Elimu asome Buguruni S/Msingi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by urassa, Apr 21, 2009.

 1. u

  urassa Member

  #1
  Apr 21, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Elimu au Afya hatakuwa na uchungu wa kubadili hali ya shule au hospitali wakati hana mtoto wake anayesoma au kupata matibabu sehemu hizo, viongozi tuache unafiki
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Apr 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  aika mmeku
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hahahaha imekaa vizuri hiyo.
  siku hizi hata hausiboi anawaza kumpeleka mwanaye shule za kimataifa.
  kuna mahala pameoza ktk nchi hii, tunasikia harufu tu wala hatujihangaishi kutafuta uozo huu na kuufagilia nje.
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hapa kuna Ukweli,

  hata mahospitali viongozi wakiugua watibiwa Tz ndo huduma ziboreshwe!
   
 5. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Swadakta, ila sasa na sisi ndio tushajizoelea masikini ya Mungu. Tunashukuru Mkuu kwa kuanzisha hii
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Wakuu,
  Nadhani wananchi hawajui nguvu waliyo nayo katika kukomesha baadhi ya mambo au kuboresha mambo pale inapotakikana, kwa kupitia sanduku la kura.Sijui kwa mfano kama mwananchi wa kawaida anajua kuwa wakati wa kipindi cha uchaguzi ndicho kipindi cha kuwakaanga hao viongozi.Mfano mdogo tu -Nchi nyingine wananchi kupitia caucuses zao ( wanawake, vijana etc) wameweza kutengeza manifesto mbadala na kuwasulubu wagombea kwa maswali makali ya ni vipi watahakikisha wananchi wanapata huduma bora na hata kuwataka wafanye mrejesho wa kile walichowafanyia wananchi kwa miaka 5 inayoisha ili kujijengea uhalali wa kuchaguliwa tena.Najua nchini Canada kwa mfano wanawake waliweza kutumia " shocking pink Paper" kuwatetemesha wagombea wa nafasi nafasi za uongozi kwa mtindo huo.BAWATA walijaribu kidogo ila wakaonekana wanaunga mkono chama cha upinzani NCCR maana wakati ule 1995 kiliitingisha CCM kwelikweli.No wonder baada ya uchaguzi, BAWATA ikapigwa rungu la kichwa na wale waliohusishwa nayo wakaonekana ni wapinzani.

  Nadhani hili la tiba na shule nje ya nchi ni moja ya ajenda muhimu ambayo wangeivalia njuga na hata ikiwezekana kuwataka hao viongozi waji commit kuwa hawataenda kujitibia nje ( kwa kodi za wananchi)au hata kupeleka watoto wao nje kupata elimu muda wote watakaokuwa madarakani! Najua kabisa mtacheka na kuona hili haliwezekani lakini bila kutafuta dawa chungu sana, hii nchi itakuwa maziwa na asali kwa wachache, na shubiri kwa walio wengi hasa walala na waamkahoi!
   
 7. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Jamani mwenzenu mbona nilikwisha jiandaa kuvumilia tu!
  Kwasasa mtoto wangu ansome Shule ya Msingi Mburahati, anakaa kwa shangazi yake Kigogo. Akimaliza shule ya msingi atakwenda soma shule moja ya sekondari za kata Kule Ntwara inayofundishwa na walimu" Voda-fasta".
  Kuhusu chuo sina uhakika kama atasoma,labda kama kama nafasi za ualimu zitakuwa bado hazijaisha aende angalau ule wa shule za msingi.
  nachoomba ni kwamba asiumwe kipindi chote hicho.
  Akiwa shuleni nimemwambia mi sina hela ya kumpa kila siku eti anunulie chipsi na maji ya chupa. Nimemwambia yeye hata shangazi yake kuwa mihogo mitano ya sh 50 na maji ya kiroba(cha kupuliza) yanatosha.
   
 8. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Hahahahaaaaaaaa! kama utani vile kumbe ndiyo hali ya mtz wa kawaida. Watoto wetu ndivyo tunavyowa - handle, hatuna namna. It pains, we know most of ward secondary schools have no facilities, since we don't have alternatives, we're forced to send our children in such substandard schools.
   
 9. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Jamani swala la elimu ya tanzania si la kufanyia mchezo, tusiongee kwa utani hapa kwani tunatengeneza matabaka ya watawala na watawaliwa bila kujijua, hii aina tofauti na mkoloni alivyokuwa anasomesha watoto wa machifu wamsaidie kutawala ndio kinafanyika sasa.

  Wenye pesa nyingi na viongozi wanaandaa watoto wao kuwa viongozi wa taifa letu kwa kuwapa elimu ya nje ya nchi inayothaminiwa na kila sector ndani ya nchi yetu wakati watoto wa wenye kipato cha kati wanasomeshwa kwenye shule za FM wawasaidie watoto wa wenye pesa kuendesha nchi baadae vilvile kwa kuwapatia nafasi kidogo kwenye vyuo vya serikali vyenye idadi kubwa ya wanafunzi wakati huduma ziko chache.

  Watoto wa watanzania walio wengi wanaishia kuajiliwa kwenye nafasi za chini kwa kuwa track yao ya elimu haithaminiwi na sector tulizonazo na kufanya hawa kuwa watawaliwa wakati wote.

  Hii inatengeza viscious cycle kwani mtoto wa mwalimu anayelipwa Sh. 150,000 hataweza kumsomesha mtoto wake shule ya Sh. 2,000,000 kwa mwaka hacha kuchangia gharama kwa 60% ya chuo.
   
 10. s

  sikukuu Member

  #10
  Apr 21, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaumiza sana kwakweli,hii habari inagusa karibu kila mtu,hivi hii nchi inakuwaje lakini!!!!!! kwa sababu nyakati za mwalimu watu walikuwa hawachangii matibabu Hosp wala karo sec school kama leo lakini tulisoma na tukamailza vizuri pia warrant za kusafiri likizo tulikuwatunapewa, lakini leo tunalipia karibu kila kitu lakini huduma ndiyo hakuna kabisa !! ama kweli nchi hii iko mikononi mwa mafisadi wachache
   
 11. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kwa kuwa na wewe ni mmoja wao,naomba utuambie watoto wako wanasoma wapi?
   
Loading...