Mtoto wa Spika Sitta hatarini kubuzwa mahakamani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Spika Sitta hatarini kubuzwa mahakamani.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pengo, Nov 21, 2009.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Taarifa zilizotufikia na ambazo zimethibitishwa na wahusika zinasema kuwa mtoto wa kiume wa mh.Samwel Sita ambaye ni spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania,aitwae Edward Sitta yupo mbioni kuburuzwa mahakamani na mdhamini wake aitwae mzee Richard kwa kutaka kumsababishia hasara ya kuuzwa nyumba yake iliyopo Sinza Makaburini nyuma ya baa maarufu iitwayo Ukanda wa Gaza.

  Mnamo mwanzoni mwa mwezi mei,bwana Edward Sitta pamoja na Partner wake wa biashara aitwae Godwin,wote kwa pamoja wanamiliki kampuni iitwayo Business Care inayojishighulisha na mambo ya biashara walimwendea mzee Richard na kumshawishi awape hati yake ya nyumba ili wakapate mkopo benki na baadae wangeikomboa ile hati na kumpa faida kiasi mzee Richard ambaye ni rafiki mkubwa wa mzee Sitta.Kwa kutumia kampuni yao ya Business Care,Godwin na Edward walipeleka hati ya nyumba ya mzee Richard benki ya NMB Azikiwe na kufanikiwa kupata mkopo wa milioni kumi Tshs.10,000,000/=.Business Care ilimwakikishia mzee Richard kuwa ndani ya miezi mitatu wangeweza kumrudishia hati yake baada ya kuikomboa benki lakini hadi mwezi huu wa November bado hawajarejesha pesa za mkopo benki na sasa inakadiliwa kufikia milioni kumi na tano Tshs.15,000,000/= kutokana na riba.

  Baada ya kuona mafanikio ya kurejeshewa hati yake yanafifia,jumatano 18/11/2009 mzee Richard akaamua kumfuata mh.Sitta ambaye ndio kwanza alikuwa anarudi nchini akitokea Marekani na kumpa kisanga chote kilivyotokea na pia kumwambia hatosita kuifikisha mahakani kampuni ya Business Care inayomilikiwa na Edward Sitta na mwenzie Godwin.Kuona hivyo mzee Sitta kwa kuchelea hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini kwa muda huu,amemwagiza mtoto wake Edward kutafuta pesa za haraka kulipa benki ili hati ya mzee Richard irudishwe na pia isije kuwa ni mwanzo wa kumchafua yeye mh.Sitta kwa wapinzani wake.

  Anayetaka maelezo zaidi awasiliane na mzee Richard (Sinza nyuma ya baa Ukanda wa Gaza-nyumba yake inatazamana na kiwanja cha wazi cha watoto),Meneja wa NMB tawi la Azikiwe au amtafute Edward Sitta mwenyewe.
   
Loading...