Mtoto wa siku 19 (Kama wiki mbili na nusu hivi) analia sana

PAND PIERI

Senior Member
Jul 30, 2020
183
270
Poleni na majukum ya kujenga Taifa ndg zg , mtoto mwenye umri niliyotaja hapo juu analia Sana ( Sana Sana wakati was usiku) Kama tumbo inamsokota vile, Kuna muda anajikunja sana, huku akiwa analia.

Anajamba na haja kubwa anaenda, nilimpereka hospital wakaniambia ni hali ya kawaida akiwa anajamba na kwenda haja kubwa hamna shida . Mtoto anajikakamua/ tumbo ina msokota na analia tumbo ikianza kumsokota hata kunyonya hanyonyi.

Shida yangu ni kuomba msaada /dawa nikamnunulie angalau ajisikie vizuri najisikia vibaya anaposokotwa na tumbo na hata abemberezwe hatuli mpaka tumbo itulie kidogo.
 
Hii wanaita chango inawasumbua saana watoto wachanga, ila akifika miezi 3 inakoma, dawa za hospital hazisaidii!

wakati wa kunyonyesha mama amwekee chuchu vzr mdomoni na kuhakikisha mtoto haiingizi gesi tumboni!

Mama akishamnyonyesha mtoto amwegemeze tumbo la mtoto usawa wa bega lake huku akimpiga piga taratibu mgongoni walau kwa nusu Saa ili kumcheulisha!

Pia Mama anaweza akampaka mtoto mafuta tumboni kisha akaipasha mikoni yake (mama) kwenye moto, ikiishapata moto amfanyie massage ya tumbo mtoto mpaka atakapocheua ili kutoa gesi tumboni!

Kuna mtu alinambia kuwa maduka ya wahindi wana dawa nzuri.

Pia nasikia mvumbaze (kashwagalaa kwa kiyaha) husaidia hii kitu! Pole saana mkuu.
 
Amepata bacteria infection kwenye tumbo, hakikisha mama mtoto kabla ya kumnyonyesha asafishe vizuri chuchu zake/ kuoga Mara kwa Mara maana zikichanganyikana na jasho na uchafu zinampa madhara mtoto anayenyonya
 
Amepata bacteria infection kwenye tumbo, hakikisha mama mtoto kabla ya kumnyonyesha asafishe vizuri chuchu zake/ kuoga Mara kwa Mara maana zikichanganyikana na jasho na uchafu zinampa madhara mtoto anayenyonya
Mkuu usafi Sina wasiwasi, anajitahidi kwa usafi.
 
Back
Top Bottom