sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,032
Nyumbani kwangu ikifika wakati wa chakula cha usiku (dinner) ni lazima tule pamoja kwenye chumba kimoja,
Sasa kuna mtoto wa shangazi ni kama miaka 20 hivi hapendi kufata sheria ya mda wa dinner. Sheria ya muda wa mlo wa usiku ni kwamba simu hazitakiwi kutumika, simu inabidi ziachww vyumbani.
Lengo ni kupata chakula cha usiku kama familia, ni muda ambao watu wote ndani ya nyumba tunajumuika, kila mtu anaelezea siku yake imeendaje, maendeleo ama changamoto kwenye shughuli zake, ushauri, kukumbushana umoja ni nguvu, n.k.
Sasa huyu dogo ni kama haheshimu huu utaratibu, yeye akija bado yupo busy na simu kwa kuibia ibia. Shangazi yangu ni mtu ambae tumezoeana sana tangu nikiwa mtoto, naogopa nikimminya sana dogo ataenda kulalamika halafu ikala kwangu.
Nimemwambia kama mara 3 anaacha ila anarudia.
Suluhisho ni nini??