Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,375
- 14,870
Shida ipo ndiyo maana haujawahi kusikia mwanajeshi katangaza kuutaka urais huku bado anashikilia madaraka ya jeshi.
Yaani Kanali akiwa bado jeshini aruhusiwe kugombea urais, kisha akaukosa urais, akishaukosa anarudi tena kua Kanali na anatakiwa amtii aliyekua mpinzani wake.
Chief unakomalia hayo mawazo yako kwa kutumia doctrine ipi ya demokrasia?
Si ndio maana nikakuambia wewe unafikiri "negative", yaani Kanali au generali akigombea uraisi na akishindwa na akirudi jeshini eti anaweza kupitia jeshi akahamasisha Mapinduzi dhidi ya aliyeshinda ambaye atakuwa labda ni Amiri jeshi wake !!!---- hiyo ndiyo fallacy potofu na uoga, kwani yeye hajui kwamba Amiri jeshi ndiye top kuliko yeye?? kwani ni lazima afanye mapinduzi au uasi kupitia jeshi??, kwani Amiri jeshi hawezi kumuondoa madarakani anapoona inafaa?? ni mapinduzi mangapi yamefanywa au yameongozwa na wasiokuwa wanajeshi??--- kama Generali anayo dhamira ya kutangaza nia na anazuiwa na sheria kutotangaza je atashindwaje kuhamasisha mapinduzi kupitia jeshi ili atimize nia yake ya kuwa raisi??!! maana hiyo ndio hofu yenu lakini mnashindwa kuitafakari kwa mapana na marefu.
Mkuu msingi mkubwa unaoweza kuepusha mapinduzi mnayoyaogopa ni NIDHAMU NA HESHIMA kutoka kwa hao wanajeshi na sio kitu kingine kwani jeshi (viongozi wa jeshi) lisilokuwa na nidhamu linaweza kufanya mapinduzi, na imeshatokea, wakati wowote na sio lazima kupitia kutangaza nia, nidhamu jeshini ndio moyo wa jeshi na sio the otherwise.