Mtoto wa Rais Kikwete mlinzi wa mali za UVCCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Rais Kikwete mlinzi wa mali za UVCCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Sep 6, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  LAITI NYERERE ANGEFUFUKA SASA HIVI SIJUI.....

  Mtoto wa Rais Kikwete mlinzi wa mali za UVCCM

  Na Mwandishi Wetu

  MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amepewa wadhifa nyeti ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), mali na miradi yote ya umoja huo zitakuwa chini yake.

  Ridhiwan amepewa nafasi hiyo wakati baba yake akiwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, huku UVCCM yenyewe, ikiwa katika msuguano wa chini chini wa kuhusu ubadhirifu wa mali za jumuia hiyo.

  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, ingawa mali za UVCCM ziko chini ya Baraza la Udhamini ambalo kwa sasa linaongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Ridhiwan ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi inayoangalia mali na kutoa ushauri namna ya kuzitumia.

  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Hamad Yusuf Masauni, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alithibitisha, lakini akasema si Ridhiwan pekee bali kwa mamlaka yake, aliunda kamati ndogo tano za utekelezaji.

  Kwa mujibu wa Masauni, Ridhiwan kama walivyo wenyeviti wa kamati nyingine ndogo, hana mamlaka zaidi ya kuishauri Sekretarieti na Kamati Kuu namna bora ya kuendeleza au kubuni miradi mipya ambayo itakuwa na tija kwa UVCCM.

  “Hana jukumu la kusimamia, tumeweza kuunda mfumo wa kamati ndogo za utekelezaji zipo tano, nyingine ni kama ya Vyuo Vikuu, Sheria, kazi yao kubwa ni kushirikiana na Sekretarieti kwa kuleta mapendekezo yao,” alifafanua.

  Alisema Ridhiwan hahusiki na shughuli za utendaji wa kila siku kwa kuingilia mamlaka ya Katibu Mkuu, wao wafanyakazi kwa mujibu wa katiba na mamlaka ya mali zote za UVCCM iko chini ya Baraza la Udhamini.

  Masauni alisema si Ridhiwan pekee bali wapo wenyeviti wengine wa kamati hizo ndogo kama James Millya, ambaye ni mwenyekiti wa UVCCM Arusha.

  Kiongozi huyo wa UVCCM, alisema Sekretarieti ina uwezo wa kukataa mapendekezo yanayotokana na kamati ndogo ikiwemo hiyo inayoongozwa na Ridhiwan.

  “Siyo kila wanachoshauri kinaweza kupita, kamati zina shauri tu, ushauri wao unaweza kukubaliwa au kukataliwa na Sekretarieti au Kamati Kuu,” alisisitiza.

  Akifafanua, Masauni alisema UVCCM ina matatizo madogo ya mfumo ambao tayari alipopewa wadhifa huo aliyazungumza na kwamba ndiyo maana aliunda kamati hizo ili zisaidie kusukuma mbele umoja huo.

  Hata hivyo, wakati Masauni akisema hayo, habari zilizopatikaa zinaeleza kuwa ndani ya umoja huo kuna msuguano wa kimamlaka ambao unatokana na baadhi ya watu kutaka kufanya maamuzi kwa shinikizo kutoka kwa viongozi wa juu wa chama.

  Kwa mujibu wa habari hizo, hivi karibuni UVCCM ilitaka kukopa fedha kutoka benki moja (jina tunalo) lakini mmoja wa viongozi wake kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi akaweka pingamizi ambalo lilifanya umoja huo ukose mkopo huo.

  Baadhi ya watu ndani ya umoja huo wamekuwa wakishinikiza uongozi wa juu akiwamo Mwenyekiti kutoa maamuzi ambayo yanawanufaisha hasa katika masuala yanayohusu usimamizi wa mali za UVCCM.

  Hata hivyo, inaelezwa kwamba watu hao wamekuwa wakipambana na Masauni ambaye hupenda kufuata kanuni, katiba na taratibu za chama bila kuogopa vivuli vya mamlaka nyingine.

  Ridhiwani alipotafutwa wiki hii kuzungumzia baadhi ya mambo ndani ya umoja huo, alijibu: “Siwezi kufanya interview (mahojiano) wewe kama unataka kuandika kitu kaandike.”

  UVCCM imekuwa katika kipindi kigumu cha mpito tangu kuibuka makundi na wakati kupata safu mpya ya uongozi uliowaingiza madarakani Masauni na Makamu Mwenyekiti, Beno Malisa.

  Hivi karibuni pia umoja huo ulikumbwa na mgogoro wa uendelezaji wa mradi wa ujenzi kwenye kiwanja chake jijini Dar es Salaam ambao mkataba wake ulikuwa na utata ambao uliibuliwa na mwanasiasa machachari, Nape Nnauye mwaka jana. Hali hiyo ilisababisha Kamati Kuu (CC) ya CCM yenye wajumbe watatu, Andrew Chenge, Pindi Chana na Abdalah Kigoda ili kuchunguza mkataba huo.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Usikute mzee kashtuka watu wanataka kuimaliza uvccm
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Huyo dogo sio mwizi labda wamfundishe tu,but kama baba yako ni rais na unataka kuwa tajiri kuna milions ways of how to be rich............than kuwa mlezi wa mali za uvcmm..........labda hajagundua tu.
   
 4. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa hii ina u Breaking news gani??
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Sasa hii ina u Breaking news gani??

  THOUGHT UNACHANGIA MADA KUMBE UKO KUJIBU LATEST AMA BREAKING....NEWS
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  BASI CHANGIA HIYO UJIRIDHISHE NKUU  Dawa ya Mama Mkwe!

  [​IMG]

  Hapo zamani za kale huko China, Binti aitwaye Li-Li aliolewa, yeye na mume wake wakaenda kuishi kwa mama wa mume wake yaani mama mkwe.
  Kwa muda mfupi tu walioishi Li-Li aligundua kwamba yeye na mama mkwe hawaendani kabisa, walitofautiana kwa kila kitu na Li-Li alikasirishwa sana na tabia za mama mkwe wake kwani mama mkwe alikuwa anamlaumu (criticize) muda wote.

  Siku zilipitia, wiki zikapita na miezi ikapita kila siku Li-Li na mama mkwe ni kuzozana na kushambuliana, kibaya zaidi ni kwamba kutokana na traditions za Uchina ilimpasa Li-Li kumpigia goti kila lile ambalo mama mkwe alihitaji afanye na ukweli hali mbaya ya mahusiano kati ya Li-Li na mama mkwe ilimfanya hata mume wake Li-Li kujisikia vibaya sana.

  Mwisho Li-Li hakuweza tena kuvumilia tabia mbaya na utawala wa imla wa mama mkwe hivyo akaamue kufanya kitu, hivyo akafunga safari kwa rafiki wa baba yake ambaye alikuwa anaitwa Mzee Huang ambaye alikuwa anauza dawa za kienyeji (herbs).

  Alipofika kwa mzee Huang akamweleza yote anayokutana nayo na kwamba anaomba msaada kama anaweza kumpa sumu ili aweze kumuua yule mama mkwe na kuondokana na lile tatizo milele (once and for all)


  Mzee Huang akafikiria kwa muda na mwisho akamwambia Li-Li atamsaidia kulimaliza tatizo lake ingawa Li-Li alitakiwa kusikiliza kwa makini na kutii kile ataambiwa akafanye.

  Na Li-Li naye kwa furaha akajibu kwamba nitafanya chochote utaniambia nifanye.
  Ndipo Mzee Huang akaingia ndani na kutoka na mfuko uliosheheni dawa (herbs) na akaanza kumpa maelezo Li-Li:

  "Huwezi kutumia sumu ya haraka kumuua mama mkwe wako kwani kila mmoja atakutilia mashaka (suspicious) wewe hivyo nimekupa kiasi cha kutosha cha dawa (herbs) ambayo itatumika kidogo kidogo na kujenga sumu ya kutosha na hatimaye kumaliza.

  Hivyo kila siku tengeneza mlo safi na weka dawa kidogo kwenye hicho chakula.
  Sasa, ili kila mtu asikutilie mashaka wewe hasa akifa lazima uwe makini sana kujifanya rafiki kwake, usibishane naye na kubali chochote anakwambia na umuhudumie kama vile ni malkia, si unajua ipo siku atapotea kabisa”.

  Li-Li alikuwa na furaha ya ajabu, akamshukuru mzee Huang na akaenda nyumbani kuanza shughuli ya kumuua mama mkwe wake.

  Miezi ikapita, wiki zikapita na siku zikapita, Li-Li aliendelea kumpa mama mkwe chakula chenye ile sumu na alikuwa anakumbuka sana jinsi Mzee Huang alivyokuwa amemweleza jinsi ya kuepuka kutiliwa mashaka, hivyo aliweza kujizua hasira zake na alimtii mama mkwe kwa kila kitu na alimhudumia kama mama yake mzazi (malkia)

  Baada ya miezi sita, nyumba nzima ilibadilika baada ya Li-Li kuweza kizishinda hasira zake kwa mama mkwe na kumtii na wakajikuta hawagombani tena na hawakuweza kuzozana au kubishana kwa miezi sita mfululizo na wakajikuta wanaelewana na kuishi vizuri.
  Pia mtazamo wa mama mkwe nao ulibadilika na alianza kumpenda Li-Li kama binti yake mwenyewe na akawa anawasilimua rafiki zake mwenyewe kwamba Li-Li alikuwa ni binti mzuri mwenye tabia njema ambaye hakuna mama mkwe duniani anaweza kumpata. Li-Li na mama mkwe wakawa ni kama mama na binti yake.


  Pia mume wa Li-Li alikuwa na furaha ya ajabu alipoona kile kinatokea katika familia.
  Ndipo Li-Li akarudi kwa mzee Huang kuomba masaada tena, akamwambia mzee Huang;
  “Tafadhari nisaidie jinsi ya kuiondoa ile sumu isimuue mama mkwe kwani amebadilika na amekuwa mwanamke mwema sana kwangu na ninampenda kama mama yangu mzazi na sitapenda afe kwa sababu ya sumu niliyompa”.

  Mzee Huang akawa anatabasamu huku anatikisa kichwa.

  “Li-Li huna haja kuwa na mashaka au kuogopa, sikukupa sumu yoyote, dawa niliyokupa ilikuwa ni vitamins kwa ajili ya kuimarisha afya. Sumu kubwa iliyokuwepo ilikuwa kichwani mwako (mind) na mtazamo wako kuhusu mama mkwe na hiyo sumu yote imesafishwa na upendo ambayo umeutoa kwake”.

  Je, msomaji wangu umegundua kwamba jinsi unavyowahudumia wengine ndivyo na wao watakavyokuhudumia wewe.

  Kuna msemo wa kichina ambao unasema:
  "The person who loves others will also be loved in return."

  Inawezekana ni kweli unasuguana sana na mama mkwe au mume wako au mke wako au mpenzi wako na tatizo kubwa ni mtazamo wako kuhusu yeye na ungeamua kumpenda na kumhudumia kama malkia au mfalme mambo yangebadilika.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  safi sana. nimeipenda
   
 8. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakuna shida ridwani kuwa overseer wa hizo mali,namfahamu ni mwaminifu pia anaogopa na kuheshimu sheria kwa sana tuu,sasa nchi inahitaji watu waaminifu na wenye integrity kuinusuru nchi,wazee hawana mpya!!
   
 9. J

  Jews4ever Member

  #9
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu dogo riziwani ana usafi gani?
  Baba yake ni fisadi period
  Toto la joka ni joka tuu, tabia zao ni moja
  NB:
  Tabia ni kama ngozi ya mwili.
   
 10. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pdidy,

  Hadithi yako nimeipenda.

  Ahasante.
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  CCM imeisha kuwa SACCOS....!
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tunaweza kuita walio mpa cheo ni kujipendekeza machoni mwa rais na ni sifa za kijinga pia.
   
 13. K

  Kachero JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huko kumpa hiyo nafasi Ridhiwan hakuna maana yoyote,inavyoelekea sasa ndani ya chama hakuna mtu anayemuamini mwenzake hivyo ni kulinda kila kona.Lakini wakiweka utaratibu unaofaa na kupata viongozi waaminifu na wanaofaa pengine wanaweza kupunguza tatizo sasa, lakini tukumbuke kuwa dalili ya mvua ni mawingu...ndani ya chama watu hawaaminiani lazima kila kambi iweke walinzi wake amasivyo wajanja watalamba dume.
   
 14. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na mama aangalie mali za UWT
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  to be honest...........
  ''the boy is so clean''!tuache izo hesabu za ''linear interpolation'' wakuu
  thanks,na mbarikiwe
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Licha ya kuwa safi, sijaona wale wanaouangalia uteuzi huo kwa jicho la husuda wana kitu gani cha kikanuni au kisheria kinachozuia kijana kupewa nafasi hiyo
   
 17. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145

  Mkuu Geoff,

  Sina uhakika kama kweli huyu kijana ni msafi, si alikuwa mfanyakazi wa Kampuni ya sheria ya akina Masha (IMMMA)wakati wa wizi wa pesa za EPA kupitia Deep Green?

  I am conviced he is not that much clean.

  Tiba
   
 18. Mdumange

  Mdumange JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 485
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 80
  Aaaah kaka,kuwa na heshima kidogooo,watu wanaomjua wamekwambia yuko safii na hana tone la ufisadi sasa shida yako ni nini.
  Dogo namfahamu toka huku UK ni mtu wa watu,hana majivuno kama watoto wengine wa wakubwa na anapenda kujichanganya na wote masikini kwa matajiri.Ngoja niweke story iwe short, Dogo hana hata chembe moja ya UFISADI na kama ni uangalizi wa mali ya vijana hamna shida kabisa hizo zote ni harakati za kuufukuza mkono wa mafisadi UVcmm.
  KUDOS RIDHIWANI.
   
 19. RADIKALI

  RADIKALI Member

  #19
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amepewa wadhifa nyeti ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), mali na miradi yote ya umoja huo zitakuwa chini yake.

  Ridhiwan amepewa nafasi hiyo wakati baba yake akiwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, huku UVCCM yenyewe, ikiwa katika msuguano wa chini chini wa kuhusu ubadhirifu wa mali za jumuia hiyo.

  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, ingawa mali za UVCCM ziko chini ya Baraza la Udhamini ambalo kwa sasa linaongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Ridhiwan ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi inayoangalia mali na kutoa ushauri namna ya kuzitumia.

  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Hamad Yusuf Masauni, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alithibitisha, lakini akasema si Ridhiwan pekee bali kwa mamlaka yake, aliunda kamati ndogo tano za utekelezaji.

  Kwa mujibu wa Masauni, Ridhiwan kama walivyo wenyeviti wa kamati nyingine ndogo, hana mamlaka zaidi ya kuishauri Sekretarieti na Kamati Kuu namna bora ya kuendeleza au kubuni miradi mipya ambayo itakuwa na tija kwa UVCCM.
  “Hana jukumu la kusimamia, tumeweza kuunda mfumo wa kamati ndogo za utekelezaji zipo tano, nyingine ni kama ya Vyuo Vikuu, Sheria, kazi yao kubwa ni kushirikiana na Sekretarieti kwa kuleta mapendekezo yao,” alifafanua
  Soma zaidi hapa http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=14400
   
 20. Alai

  Alai Member

  #20
  Sep 9, 2009
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ndivyo wote huongoza kutoka Obama mpaka Gaddaffi. Wote ni ndugu na marafiki na mimi huamini kwamba ili uwe na nguvu za kuongoza na upate kutimiza mipango za kitaifa kama wewe ni rais, lazima uweke watu wanaukuamini na sioni ubaya wowote ila tu wanapoanza kuifanya kupita kiasi
   
Loading...