Mtoto wa Nyani aanza kujitetea Mahakamani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,472
2,000
Mshtakiwa Baraka Joshua(23) maarufu kwa jina la mtoto wa Nyani, anayekabiliwa na shtaka la kubaka na kulawiti mtoto wa miaka tisa, ameieleza mahakama kuwa yeye hajahusika katika ubakaji wa mtoto huyo.

Joshua ameeleza hayo leo (Jumatano) wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya utetezi baada ya mahakama hiyo kumkuta na kesi ya kujibu.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Ester Kyara, mbele ya Hakimu Catherine Kiyoja, mshtakiwa huyo alidai Mei 17, 2016, saa nne asubuhi alikuwa eneo Shule ya Msingi Tabata Kimanga akiuza vitu mbalimbali ikiwamo ‘chips snack’ maarufu kama chama.

“Nikiwa nauza chips hizo zinazopendwa na wanafunzi pamoja na vitu vingine kama pipi, alitokea mwalimu mmoja akisema nimebaka mwanafunzi hadi amechelewa kuingia darasani,”amedai mshtakiwa huyo.

Joshua alidai kuwa mwanafunzi huyo alimweleza mwalimu wake kuwa amebakwa baada ya kulazimishwa aeleze alipotishiwa fimbo.

Ameieleza mahakama kuwa mwalimu alimtishia mwanafunzi kumpiga fimbo kwa nini amechelewa kuingia darasani.

“Hapo ndipo mwanafunzi huyo alipodai kuwa nimembaka, wakati mimi sijafanya hivyo,” aliendelea kudai.

Kutokana na hali hiyo, mwalimu huyo alipiga simu polisi na polisi walipofika walimchukua mwanafunzi huyo na kumpeleka hospitali kwa ajili ya vipimo.

“Niliomba na mimi wanipeleke hospitali nikapimwe ili wajue kama nilishiriki kufanya mapenzi na mwanafunzi huo, lakini walinikatalia na badala yake nilikamatwa na kupelekwa polisi” amedai.

Baada ya kumaliza kujitetea mshtakiwa huyo, Hakimu Kiyoja aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 6, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuulizwa maswali na upande wa Jamhuri.

Katika kesi hiyo, Joshua, maarufu kama Mtoto wa Nyani, anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 9, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kimanga.

Joshua anadaiwa kuishi na nyani baada ya kuzaliwa na kutupwa porini lakini aliokotwa na kuanza kuishi na msamaria mwema miaka minane iliyopita.

Moja ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ulieleza kuwa, Joshua anadaiwa kumwingilia kinyume na maumbile, mtoto huyo mara kwa mara.

Shahidi huyo, Eveline Nzagwi (42) ambaye ni Daktari Msaidizi kutoka Zahanati ya Tabata Shule, alidai kuwa alibaini misuli inayokaza sehemu ya haja kubwa ya mlalamikaji ikiwa imelegea kutokana na kuingiliwa mara kwa mara.

“Tulimuuliza yule mama mwenye mtoto kuwa ilikuaje mpaka mtoto wake amebakwa na kulawitiwa? Na yeye alitujibu kuwa kuna kijana mmoja ambaye anauza pipi katika Shule ya Tabata ambaye humchukua binti yake na kwenda kumfanyia vitendo hivyo na kisha kumpa pipi,” amedai Nzagwi.

Chanzo: Mwananchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom